Wednesday, September 10, 2014

HIZI NDIO FAIDA KUMI (10) ZA KUKUMBATIA (HUGGING)

1.Husaidia uzalishaji wa homoni ya “oxytocin” ambayo husaidia sana mwili kuondoa tatizo la kuhisi upweke, hasira, na kutengwa. 
2.Unapomkumbatia mtu, unaupa mwili hali ya kujihisi salama na huru pia. 
3. Hug hufanya misuli isinyae hivyo kusaidia kuondoa/kupunguza baadhi ya maumivu ya mwili na kuufanya uwe huru. 
4.Huboresha mahusiano ya watu wanaopendana kwani unapomkumbatia mtu unaonyesha hali ya kupenda, usalama, na mapenzi ya dhati.
5.Huondoa uoga na wasiwasi. 
6.Utajikuta unajiona wa thamani kumbuka tulipokuwa wadogo, wazazi wetu walitukumbatia na tukajiona tunapendwa na tuko mahali salama, upendo ule tulioonyeshwa na wazazi wetu, unakuwepo ndani yetu kadri tunavyokuwa watu wazima, na unapomkumbatia mtu inakufanya uhisi kupendwa na wathamani. 
7.Huleta usawa kwenye Mfumo wa fahamu kwani wengi wetu tunaishi katika mazingira yanayoufanya mwili kuwa katika hali ya kujihami muda wote hivyo unapomkumbatia mtu, mwili husinyaa na kurudi katika hali yake ya kawaida. 
8.Hug hutufundisha kutoa na kupokea. 
9.Hushusha shinikizo la damu mwilini, Mgusano wa mwili husababisha neva za kwenye ngozi zinazoitwa “Pacinian corpuscles” kupeleka habari kwenye sehemu ya ubongo (vagus nerve) inayohusika kushusha shinikizo la damu. 
10.Watoto wanaokumbatiwa kwa kiasi kikubwa wakiwa watoto, huwa katika hatari ndogo zaidi ya kupata msongo wa mawazo kuliko watoto wasiokumbatiwa vya kutosha.
Chanzo: Kumi Muhimu

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI