Thursday, September 11, 2014

BREAKING NEWS: MADEREVA WA MABASI YA MIKOANI WAFANYA MGOMO UBUNGO DAR ES SALAAM


KUNA mgomo Mkubwa wa madereva hapa Ubungo bus terminal, huu unafuatia kikao chao SIRI jana kilichowakitanisha na Sumatra pamoja na Traffic makao makuu.

Hadi sasa hatma ya abiria bado haijajulikana na hakuna dereva aliye tayari kuzungumzia nini kilichosababisha huo mgomo.
Tutaendelea kujuzana kinachoendelea!
*****
Madereva hawakukubaliana na amri ya kutembea na vyeti vyao walivyopata baada ya kuhitimu mafunzo ya udereva wa magari ya abiria.
Chanzo: Jamiiforums

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI