Thursday, September 11, 2014

BIBI ALIYEJITENGENEZEA JENEZA LAKE ATUMIWA MSAADA WA BAISKELI YA WALEMAVU

Baiskeli ya walemavu iliyotolewa na msamaria mwema wa Maryland Marekani, Joyce Rwehumbiza kwenda kwa Bibi Scholastica Mhagama mkazi wa Kijiji cha Lundusi Kata ya Peramiho wilayani Songea Mkoa wa Ruvuma.
Bibi Scholastica Mhagama (76) ambaye amejiandalia jeneza lake litakalotumika kumzikia.
Bibi Scholastica Mhagama akiliangalia jeneza lake.
Bibi Scholastica Mhagama akiwa ndani ya nyumba anayoishi.
*****
MSAMARIA mwema mmoja ametoa baiskeli ya walemavu kwa Bibi Scholastica Mhagama (76)  mwenye ulemavu wa miguu aliyeamua kijitengenea jeneza lake atakapozikwa baada ya kuishi maisha ya dhiki na kunyanyaswa bila msaada kutoka kwa jamii anayoishi.

Bibi huyo mkazi wa Kijiji cha Lundusi, Kata ya Peramiho wilayani Songea Mkoa wa Ruvuma anaishi peke yake katika kibanda kilichoezekwa kwa nyasi.

Msamaria huyu kutoka Maryland, Marekani anaitwa Joyce Rwehumbiza na aliguswa na stori iliyoandikwa na gazeti la Global Publishers ambapo stori yake iko hapa:  BIBI KIZEE AJIANDALIA JENEZA!
Joyce Rwehumbiza ameishatuma baiskeli  hiyo na imefika Dar es Salaam Ahamisi ya  Septamba 11, 2014.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI