Saturday, September 6, 2014

AMNG'ATA MIDOMO MPENZI WAKE WAKATI WANAKISS KWA KUHISI ANA MCHEPUKO WA FACEBOOK *PICHAZ*



HABARI hii ni kutoka Uingereza ambayo ni ya kusikitisha ya kijana Rhys Culley kumng’ata vibaya midomo mpenzi wake Chanttelle Ward mwenye umri wa miaka 18 wakati anamkiss baada ya kuwa na ugomvi unaohusisha na wivu wa mapenzi.
Kijana huyo wa miaka 23 alikuwa na wasiwasi baada ya kuhisi kuwa mpenzi wake alikuwa anachat na mwanaume kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook akimsaliti.
Akisimulia mkasa huo mbele ya jopo la majaji, Chanttelle ameeleza kuwa baada ya kutoka kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa ya mama yake msichana huyo walielekea nyumbani kwao ambapo Rhys alianzisha mzozo akimtuhumu kuwa anamsaliti kupitia Facebook.
Kijana huyo alichukua simu ya Chanttelle kwa makubaliano ya kuangalia jumbe alizokuwa anatuma Facebook lakini hakukuta mawasiliano kati ya msichana huyo na mwanaume aliyekuwa anamhisi. 
Moja kwa moja akaanza kupaza sauti kwa hasira akidai kuwa amezifuta.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI