Wednesday, August 6, 2014

SHIJA NAE HOI AFRIKA KUSINI

STAA wa filamu za Kibongo, Deogratius Shija ameugua ghafla na kulazwa katika hospitali moja jijini Johannesburg, Afrika Kusini alipokwenda kwa mapumziko mafupi.
Akiwasiliana na mwandishi wetu kupitia mtandao mmoja wa kijamii, rafiki wa karibu wa Shija aliyeomba hifadhi ya jina lake alithibitisha kuhusu kuugua kwa msanii huyo.
Ni kweli Shija amelazwa hapa Kwazulu Natal, aligua ghafla kutokana na mbadilishano wa hali ya hewa.
"Hapa Sauzi kipindi hiki kuna baridi kali sana. Kwa huko Bongo, unaweza kufananisha na Mufindi, lakini hali yake siyo mbaya sana, anaendelea vizuri"
alisema rafiki huyo ambaye ndiye mwenyeji wa Shija.
Siku ya pili, mwandishi wetu alifanikiwa kuwasiliana na Shija kupitia mtandao mwingine wa kijamii ambapo alisema:
"Ni kweli kaka nilipata dhoruba la afya kidogo, lakini nashukuru sasa nipo poa na nimeshatoka hospitalini".

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI