NICKI Minaj alitumia picha kuvuta umakini wa watu ambao walikuwa wakiisubiria kwa hamu video ya wimbo wake ‘Anaconda’ ikiwa pia ni baada ya kutoa kipande cha video kinachoonesha utengenezaji wake.
August 18, Nicki alishare picha kuhusu video hiyo inayomuonesha yeye akiwa amekaa katika mtindo wa mitego tata mbele ya Drake aliyekaa kwenye kiti kama anaesubiri huduma.
Picha za wimbo na video ya Anaconda ya mwimbaji huyo ni kati ya picha zilizozua utata mkubwa kwenye mitandao ya kijamii hadi kufikia hatua ya kutaka kuondolewa kwenye Instagram.
Anaconda ni wimbo mpya unaotoka kwenye albam ya ‘The Pink Print’ na rapper huyo wa Young Money anatarajiwa kuuimba Live wakati wa utoaji wa MTV Video Music Awards, Jumapili, August 24.
0 comments:
Post a Comment