Sunday, August 24, 2014

NICK MINAJ AVUNJA RECORD YOUTUBE ILIYOKUWA IKISHIKILIWA NA MKALI WA KUTWERK 'MILEY CYRUS'


VIDEO mpya yenye utata kwa kwa baadhi ya nchi fulani kuzuiliwa kupigwa “Anaconda”, imevunja record ambayo mara ya mwisho ilikuwa inashikiliwa na video za mwanamuziki Miley Cyrus za ku-twerk stejini.
 Video ya anaconda inashikilia record mpya kabisa kwa kuangaliwa na watu milioni 19.4 duniani nzima ndani ya masaa 24 tu toka ilipoachiwa hewani kwenye mtandao wa Youtube.
Na kwa sasa video hii imeshapata zaidi ya hits million 58 na inaendelea kupata watazamaji wapya kila iishapo siku.
Hii ndio inasemekana moja ya video zenye picha za wakubwa zaidi mwezi huu, wengi wanadhani kuwa kutokana na kupewa promo nyingi katika mitandao mbali mbali kabla haijatoka ndio imesababisha kuvunjwa kwa record hii, ila wadau wa muziki wanasema kuwa video hii ni nzuri na imegusa haswa maudhui ya mwandishi na ndio maana imepokelewa vizuri na wapenzi wa muziki.
TUNAOMBA RADHI:
KUTOKANA NA MAUDHUI YA PICHA ZA VIDEO HIYO HATUTAWEZA KUIWEKA KATIKA MTANDAO HUU. UNAWEZA KUIANGALIA KUPITIA YOUTUBE.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI