Paka mweusi akikatiza Uwanja wa Camp Nou.
BARCELONA imeanza vyema La Liga kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Elche Uwanja wa Camp Npu usiku wa kuamkia leo.Katika mchezo huo, kiungo wa Barca Javier Mascherano alitolewa nje kwa kadi nyekundu kipindi cha kwanza, kocha mpya Luis Enrique akiiongoza timu kwa mara ya kwanza, alionyesha mwanzo mzuri.
Mchezaji wa timu gani? Paka huyu alisababisha mechi isimame ili kwanza apite
Lionel Messi kushoto akifurahia baada ya kufunga mabao mawili.
***********
LIONEL Messi aliifungia Barca bao la kwanza baada ya kuwazidi ujanja mabeki sita Elche, kabla ya kinda Munir El Hadaddi kufunga la pili, mabao yote kipindi cha kwanza.
Nyota wa Argentina, Lionel Messi alifunga bao lake la pili na la tatu la kuhitimisha ushindi wa Barca baada ya jitihada binafsi kipindi cha pili.
|
Paka mweusi alikatiza Uwanja wa Camp Nou mwanzoni tu mwa mchezo na kusababisha mechi isimame kwa muda ili aondoke.
0 comments:
Post a Comment