Friday, August 8, 2014

FURSA YA KUPATA RUZUKU YA KUFANYA HABARI ZA UCHUNGUZI YAWAFIKIA WAANDISHI WA HABARI MKOANI MBEYA

MKUTANO NA WAANDISHI WOTE MKOA WA MBEYA
Salamu nyingi kutoka Tanzania Media Fund.
Napenda kuchukua nafasi hii kuwaalika rasmi waandishi wote wa habari jijini Mbeya kwenye mkutano wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania, maarufu kama TMF utakaofanyika tarehe 22 Agosti 2014 kwenye ukumbi wa GR Hotel, Soweto jijini Mbeya.
Mkutano utaanza saa mbili na nusu.
Lengo la ujio wa timu ya TMF jijini Mbeya inatokana na ukweli kwamba kumekuwa na maombi machache sana ya ruzuku ya vijijini kutoka kwa waandishi wa mkoa wenu. Kwa maana hiyo basi, TMF inakuja na utaratibu wake wa 'Ideation' ambao humpa nafasi mwandishi wa habari mmoja mmoja kuelezea wazo lake la habari za kiuchunguzi kwa magwiji wa TMF (mentors) ambao hulitafakari na kuamua kama linastahili kupewa ruzuku ya TMF.
Hivyo basi, TMF inakuomba uwataarifu waandishi wote mkoani kwako, pamoja na wilaya zake kuhusu ujio huu na kwamba kila mwandishi ajiandae na wazo lake la habari la kiuchunguzi ambalo 'ataliuza' kwa magwiji wa TMF. 
Msisitizo ni kwamba wazo hilo liwe lenye kulenga kuleta uwajibikaji au mabadiliko katika jamii husika.
Napenda ieleweke kwamba TMF itagharamikia malipo ya ukumbi, chai ya saa nne, chakula cha mchana na chai ya saa kumi jioni. Hakuna malipo mengine yoyote kwa waandishi.
Ni hayo tu kwa leo.
Au wasiliana na Gordon Kalulunga 0754 440749
kalulunga2006@gmail.com
Wasalaam,
Japhet Sanga,
Communications/Individual Grants Officer
Tanzania Media Fund,
Dar Es Salaam.
+255 787 465 762
TMF Info <info@tmf.or.tz>
Hivos Tanzania/Tanzania Media Fund.
We have moved from 127 Mafinga Street,
Kinondoni to Kalenga/Uluguru Street, Plot 550A,
Upanga Area (Near Muhimbili National Hospital Exit Gate).

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI