Toyota Coster 'Daladala' inayofanya kazi kutoka Buguruni na Temeke likiwa mtaroni baada ya kugongwa na Scania (haipo pichani) ajali hiyo chupuchupu kuua watu na ikawaacha baadhi majeruhi.
Wananchi wakisadia kuondoa daladala kwenye mtaro.
Askari wa usalama barabarani ‘trafiki’ akimhoji konda wa daladala hiyo ambaye amejeruhiwa kichwani.
Lori kubwa aina ya Scania yenye namba za usajili T937 AAP iliyosababisha ajali.
AJALI mbaya imetokea eneo la Matumbi, Barabara ya Mandela leo na imesababishwa na lori kubwa aina ya scania lililokuwa likitokea maeneo ya Ubungo na kuelekea Buguruni.
Lilipofika kona ya Matumbi lilipoteza muelekeo na kugonga kwa nyuma gari la abiria (daladala) na kufanya gari hilo litumbukie mtaroni na kusababisha watu kuumia akiwemo konda wa daladala hilo.
Kwa mujibu wa mashuhuda, ajali hiyo imesababishwa na mwendo kasi wa lori hilo.
0 comments:
Post a Comment