NYUMBANI KITAIFA
Ulimwengu wa habari.
KATIKA BIASHARA
Ulimwengu wa habari.
MATAIFA MENGINE
Ulimwengu wa habari.
KATIKA BURUDANI
Ulimwengu wa habari.
MAAJABU DUNIANI
Ulimwengu wa habari.
Sunday, August 31, 2014
MAKAVU LIVE: PICHA TATA ALIYOTUPIA LINAH YAMPONZA.. APEWA ZA USO NA MAFANS WAKE!
4:53 AM
No comments
MSANII wa bongo flave lina sanga masaa mawili yaliyopita amepost picha instagram ikimuonyesha yupo beach lakini nguo aliyovaa ikiwa inaonyesha hadi chup*** yake aliyovaa miongoni mwa mashabiki wamefurahia na wengine wameboleka sana na kuamua kumchana live hapo chini ni baadhi ya comments za fan wake.
Wilbatyamisa Unajizalilisha Dada angun siyo wa kuvaa hivyo. Umeboa.
Marimmwakalinga11 Cjapenda best ur xo cuty but hilo vazi bad!!!
Annanold Hata kama ndio uzungu jamani ....Tako nje! Hapana bwana
Kipazalishuka sheeeeda!
Scolaenna Chupi ileeeeeeeeee!
Ziggydedon bongo kweli ulaya
Gracevenance Hata kama ni beach ndo uvae hivo kweli? Nyie vioo vya jamii mmezidi bana halafu mtu akikwambia ukweli mnamind na hao wafuasi wenu. Hebu jiheshimu na watu tutakuheshim bana, heshima haiuzwiiiii
Boazanna28 asa si ungetoa tu kinguo cha juu ili ulimwengu wajue kuwa umeumbika mxiuuuuuuu
Ashakhamisi41 Mh jamani hii dunia imeisha kwa hiyo kama anakaka zake na wao wanaona
adelterpaulsupertall Mi nakupenda lina ila ulivovaa leo
ishairl kama kutembea uchi ndo kupendeza poleni
mwanajmax mmmmh chup yote nje
mursalthebest upumbavu tu na ujinga.,
UJENZI WA KIWANJA CHA NDEGE ZANZIBAR UMEANZA TENA KWA KASI
4:41 AM
No comments
Ujenzi ukiendelea sasa wa jengo la airport nchini Zanzibar
Hivi ndivyo jengo litavyokua Bada ya kumaliza.
*******
HATIMAYE ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zanzibar uliokua umekwama kwa muda mrefu, umeanza kwa kasi huku ujenzi huo ukitarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kisauni nje kidogo ya mji mkuu wa nchi ya Zanzibar, Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, Dk. Juma Malik Akil, alisema hitilafu zilizotokea hapo awali tayari zimeshafanyiwa kazi na ujenzi unaendelea.
Alisema mradi huo uliosita miaka miwili iliyopita kwa sababu mbali mbali unaendelea tena chini ya kampuni ya Kichina ya BCEG ikisimamiwa na Mshauri Elekezi Kampuni ya ADPI kutoka Ufaransa.
Alisema juhudi za serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi wake ikiwa na pamoja na kuwajengea miundombinu muhimu ambayo itakuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa nchi ya Zanzibar itaendelea.
Alisema lengo la serikali kujenga uwanja huo ni kufikia hadhi ya kimataifa ambayo itaweza kuitangaza nchi ya Zanzibar na kuongeza idadi ya watalii.
Uwanja huo hadi kumalizika kwake utagharimu dola za Marekani milioni128 ambazo ni mkopo wakutoka benki ya Exim ya China na unategemewa kuchukuwa abiria milioni 1.6 kwa mwaka na kutua ndege kubwa ikiwemo Airbus
A340 na Boeing 777.
Mratibu wa mradi huo,Yassir Dicosta, aliwaomba Wazanzibari kutoa hofu kuhusu jengo hilo.
Mshauri elekezi kutoka kampuni ya ADPI ya Ufaransa, Jean Mare, alisema kazi yake kubwa ni kuangalia ujenzi huo unavyokwenda.
Chanzo: Free Zanzibar Blog
NDOA YA ANGELINA NA BRAD PITT: BRAD PITT AONESHA PETE YA NDOA
4:06 AM
No comments
BRAD Pitt na Angelina Jolie walifunga ndoa Jumamosi iliyopita nchini Ufaransa na taarifa za ndoa yao zilitolewa wiki hii na msemaji wao.
Kwa mujibu wa E!News , tukio hilo lilihudhuriwa na watu 22 tu na inaelezwa kuwa Angelina Jolie alivaa gauni jeupe ya kitamaduni iliyomfanya aonekane mwenye mvuto zaidi katika siku hiyo maalum kwao.
Chanzo kimeiambia MailyOnline kuwa Angie na Brad waliamua kufunga ndoa katika jumba walilolinunua mwaka 2011 baada ya Angelina kumuahidi mama yake kuwa atafunga ndoa nchini Ufaransa.
Chanzo hicho kimeongeza kuwa ndoa hiyo ni sehemu ya kumbukumbu ya miaka 10 tangu walipokutana wakati wa kushuti filamu ya Mr. and Mrs. Smith na kuanzisha uhusiano wao.
Brad Pitt ameonesha pete ya ndoa:
Eneo linaloaminika kuwa wawili hao walifungia ndoa
MWANAAFA NDIYE MSHINDI WA MILIONI 50 ZA TMT
3:59 AM
No comments
Mwanaafa ndiyo mmbabe wa TMT na ndiyo alikuwa mdogo kuliko wato katika kinyang'anyilo hicho za Mil 50.
MSHIRIKI kutoka Kanda ya Kusini, Mwanaafa Mwinzago amefanikiwa kuibuka kidedea na kutwaa shilingi milioni 50 za shindano la Tanzania Movie Talents (TMT).
Mwanaafa ambaye ndiye mshiriki aliyekuwa na umri mdogo kuliko wote ameshinda kitita hicho katika fainali iliyofanyika usiku huu katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
ANGALIA PICHASERENGETI FIESTA MJINI MOSHI
3:55 AM
No comments
Chegge (kulia) na Mhe. Temba wakilishambulia jukwaa la Serengeti Fiesta Moshi.
Nyomi baada ya kukongwa nyoyo na burudani za Serengeti Fiesta mjini Moshi.
Mwanadada Feza Kessy akifanya vitu vyake stejini katika Serengeti Fiesta mjini Moshi.
Watangazaji wa Clouds FM, DJ Fetty na B12 wakionyesha mbwembwe zao wakati wa tamasha hilo mjini Moshi.
Msanii Maua akifanya yake stejini.
(Picha zote na Musa Mateza / GPL, Moshi)
PICHA ZA RED CARPET KATIKA FAINALI YA SHINDANO LA TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT) LILILOFANYIKA TAR 30/08/2014
3:53 AM
No comments
Wadau wa TMT wakiwa kwenye Red Carpet ndani ya Ukumbi wa Mlimani City katika FAinali ya Shindano la Kusaka Vipaji vya Uigizaji lijulikanalo Kama Tanzania Movie Talents (TMT) ambapo Mshindi amepewa Shilingi Milioni 50 za Kitanzania.
Ceaser Daniel akiwa na Jaji wa Tanzania Movie Talents (TMT) Single Mtambalike
Kikundi Cha TMT Survivor kikitoa Burudani
Kumi Bora ya washiriki Wakiwa katika Picha ya Pamoja na Mkuru
Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin Bw Johnson Lukaza akiwa na Mkewe Marian Johnson katika Dhuria Jekundu usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa Mlimani City Ambapo Fainali ya Shindano la TMT lilipofanyika na Mshindi Kupatikana.
Aliyekuwa Mshiriki wa TMT na kufanikiwa kuingia hatua ya ishirini Bora na hatimaye kutolewa kwa Uchache wa Kura, Shiraz Ngasa akiwa katika picha ya Pamoja na Jaji Vyonne Cherrie au Monalisa katika zuria Jekundu
Majaji Wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) Wakijadiliana jambo kabla ya Mtanange Wa TMT uliokuwa ukirushwa live kupitia Kituo Cha ITV.
Subscribe to:
Posts (Atom)
ZILIZOSOMWA ZAIDI
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) jana, Jumamosi, Me...
-
ZILE picha za mahaba za msanii wa Hip Hop Bongo, Nay Wa Mitego akiwa na msichana kitandani zimezua balaa kwa mama mtoto wake Siwema Eds...
-
Katika pitapita zangu huko instagram nkakutana na picha hii ya msanii wa kizazi kipya Shishi Baby au mamaa ya Mziwanda. Haaa...
-
Hanging With The Bro! Diamond Platnumz & Kanye West Take A Selfie In L.A. Tanzanian music sensation Chibu Dangote also known has Diam...