Tuesday, July 29, 2014

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AONGOZA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI KATIKA MAZISHI YA MAREHEMU DR. IRENEUS KAPOLI

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza katika mazishi ya Mhadhili wa zamani wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Chuo Kikuu cha Tumaini, Dr, Ireneus Joseph Kapoli, nyubani kwa Marehemu, Mbezi Maramba Mawili jijini Dar es salaam Julai 28, 2014.
Waomboleaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mhadhili wa zamani wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Chuo Kikuu cha Tumaini, Dr, Ireneus Joseph Kapoli, katika mazishi yaliyofanyika nyubani kwa Marehemu, Mbezi Maramba Mawili jijini Dar es salaam Julai 28, 2014.
Mwili wa aliyekuwa Mhadhili wa zamani wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Chuo Kikuu cha Tumaini, Dr, Ireneus Joseph Kapoli, ukitemswa kaburini katika mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa Marehemu, Mbezi Maramba Mawili jijini Dar es salaam Julai 28, 2014.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Marehemu Dr. Kapoli enzi za uhai wake, ambapo alikuwa ni mhadhiri katika vyuo kadhaa hapa nchini kikiwemo Chuo kikuu cha Dsm, Chuo cha Ardhi, Chuo cha Tumaini, UDSM-SJMC School of Journalism and Mass Communication.

Na mwandishi Maalumu
ILIKUWA ni majonzi katika kumuaga mpendwa wao, Dk Ireneus Kapoli ambaye alikuwa ni mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, lakini pia baba wa watoto watano na wajukuu saba.
Katika msiba huo, Waziri Pinda amewaasa wana familia na wana ndungu kwa ujumla kutumia muda huu, kumrudia mungu kwani hawajui siku wala saa, hivyo hawana budi kujitakasa muda wote.
Dr Ireneus Kapoli alizaliwa mwaka 1946 na kufariki dunia Jumamosi (25/07/2014) alfajiri katika hospitali ya Tumbi huko Kibaha kwa ghafla tu, bila kuugua ugonjwa ambapo alikimbizwa hospitalini lakini uhai wake ukawa umeshatoweka duniani.

WASIFU WA MAREHEMU DR. KAPOLI  
Dr Kapoli alikuwa mtaalam wa lugha ya Kiingereza na alipata PHD yake nchini Uingereza, alianza kufundisha Chuo kikuu Campus ya Mlimani, na kustaafu kisheria mwaka 2006 baadaye kuajiriwa kwa mkataba katika Shule Kuu ya Uandishi wa habari na Mawasiliano ya Umma (SJMC).
 Alifundisha kwa muda huku akiwa katika idara ya Lugha na kuachana na mkataba na SJMC mwaka jana, akajiunga na chuo cha TUMAINI mwaka huu (2014)
Kozi alizopata kuzifundisha katika chuo hicho enzi za uhai wake ni "Communications Skills (English for Journalists/Media),"Critical Discourse Analysis" na "Critical Thinking and Argumentation"
Kwa mujibu wa Melkizedeck karol na Ochieng Ogweno ambao walikuwa ni wanafunzi wa marehemu Dr. Kapoli kwa mwaka 2010/2013 wanamzungumzia kuwa:
"alikua ni mwalimu bora aliyependa haki na usawa kwa wanafunzi wake, mshauri mzuri, mwenye msimamo".
Mkurugenzi wa mtandao huu ndg. Frank "Samfrod' Mavura naye pia ni miongoni mwa waliowahi kufundishwa na marehemu Dr. Kapoli ambapo pia atamkumbuka kwa mengi.
Mtandao huu wa ULIMWENGU WA HABARI unatoa salamu za pole kwa Mke wa marehemu na wanae pamoja na wajukuu wa marehemu, familia kwa ujumla, jumuiya ya wanafunzi wa UDSM, Chuo cha Ardhi, Tumaini na mheshimiwa Mizengo Pinda ambaye ni comred wa marehemu kwani walisoma wote na kuwa ni kama ndugu.
Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Dkt Kapoli. Amina!

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI