Wednesday, July 9, 2014

MAAJABU YA MWAKA!!! MREMBO AKUTWA KWENYE KABATI LA CHIPSI AKIWA AMELALA FOFOFO JUU YA CHIPS NA MISHIKAKI.

TUKIO hili waweza fikiri ni uongo, hii ni kweli kabisa mrembo mmoja amekutwa amelala kwenye kabati la chips maeneo ya Yombo Vituka jijini Dar es salaam asubuhi.
Imeelezwa kuwa usiku Muuza chips alipofunga  kabati na kufunga eneo lake la biashara kwa kufuli kisha akaenda kulala.
Walioshuhudia tukio hilo wanasema muuza chips alipofungua alimkuta mwanadada huyo ambaye hakujulikana jina lake akiwa amelala fofofo juu ya chips na mishikaki akiwa hajitambui.
Hata hivyo bado haijajulikana aliingiaje kwenye kabati hilo la chips maana hakuweza kuongea baada ya kutolewa katika kabati hilo.
Mmmh walimwengu wanamambo kwelikweli… Swali ni je, hizo chips zilitupwa au vipi???

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI