Thursday, July 17, 2014

IJUE FAIDA YA KUJAMBA, KUTOA USHUZI KUNAZUIA MAGONJWA YAFUATAYO, YASOME HAPA…!

KILA mmoja wetu kwa wakati fulani huhisi kuvimbiwa na gesi nyingi tumboni.
Suluhu ya pekee hapa huwa ni kujamba ili kupunguza gesi hiyo tumboni
Sasa Wanayansi katika chuo kikuu cha Exeter, nchini Uingereza, wanasema kuwa wamegundua harufu mbaya kama vile ya kujamba japo inachukiza kwa pua, ina manufaa makubwa kwa afya ya binadamu.
Wanasayansi hao wanasema kuwa harufu hiyo mbaya inaweza kuwa kinga dhidi ya magonjwa ya moyo na akili na hata Saratani.
Gesi au harufu mbaya ambayo hutokana na chakula kinachosagwa tumboni mwako inaweza kulinda baadhi ya viungo vya mwili wako.

Utafiti huo uliochapishwa katika mtandao wa chuo kikuu cha Exter uligundua kuwa gesi hiyo inayojulikana kama Hydrogen Sulfide ambayo pia hupatikana katika Mayai yaliyooza, inaweza kuwa muhimu katika kutibu baadhi ya magonjwa.
"Ingawa gesi ya hydrogen sulfide inajulikana kuwa na harufu mbaya na hupatikana katika Mayai yaliyooza pamoja na harufu ya mtu kujamba, hutengezwa mwilini na inawezekana kuwa tiba kwa magonjwa fulani,'' anasema Daktari Mark Wood, Profesa wa chuo hicho cha Exeter.

Gesi hiyo ina athari mbaya ikiwa katika viwango vikubwa , kwa mujibu wa utafiti huo.
Watafiti wanasema licha ya harufu hiyo mbaya ya kujamba kuchukiza, ina uwezo mkubwa wa kupunguza uwezekenano wa mtu kupatwa na magonjwa kama vile, Saratani,Kiharusi, mshtuko wa Moyo na kuumwa na mifupa
Chanzo: BBC

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI