Wednesday, June 4, 2014

WASHANGAZWA NA USHINDI WA HALMASHAURI YA MJI NJOMBE USAFI WA MAZINGIRA

Na James Festo, Njombe.
KATIKA kuelekea siku ya maadhisho ya mazingira ambayo hufanyika june tano ya kila mwaka huku Halmashauri ya mji wa Njombe ikiwa inaendelea kushika nafasi za juu kwa usafi wananchi wake wameendelea kuitupia lawama za kushindwa kuzoa takataka kwenye vizimba hali ambayo inaweza kusababisha magonjwa ya mlipuko.
Hali hiyo inakuja kufuatia kusuasua kwa uzoaji taka katika vizimba vya takataka vikiwemo vilivyopo karibu na maeneo yanayotumika katika uuzaji wa vyakula kitu ambacho kinaweza kusabisha madhara makubwa kwa wauzaji pamoja na wateja wao
Mwandishi wa habari hii alitembelea na kujionea vituo mbalimbali Ndani ya halmashauri ya Mji wa Njombe hali mbaya ya takataka zilizofurika nje ya vizimba licha ya wananchi kuendelea na biashara likiwemo eneo nyuma ya kituo cha mabasi mjini njombe.
Wakizungumza na majira baadhi ya wafanyabiashara hao walisema kuwa tangu kusimama kwa mawakala waliokuwa wakifanya kazi hiyo ya kuzoa takataka kwenye vizimba na Halmashuri kuvaa jukumu hilo mwenendo umekuwa wa kusuasua na kueleza kushangazwa kuona wakilipa ushuru kila uchao wakati taka hazizolewi kwa wakati.
" sasa hivi michango imesitishwa ndio maana ya kwenye vizimba taka ni nyingi.... labda kila mwananchi awe anachangia kila kaya ...tunataka tuchangie..... tukisema tufanye hivi hatufiki ...... wakala ameshindwa kufanya kazi kwa sababu kipato anachopata halmashauri ni kidogo " walisema wafanyabiashara hao.
Aidha Wafanyabiashara hao waliiomba halmashuri kutumia fedha zinazokusanywa katika ushuru wa soko kutumika katika kufanya usafi wa soko hilo na kuwasisitiza watumishi wa sekta hiyo kuacha uzembe wa kukaa ofisini.
Andove Mgani ni mwenyekiti wa soko la wafanyabishara lililopo nyuma ya kituo cha mabasi cha Njombe alisema kuwa tangu Halmashuri ya Mji ianze kusimamia yenyewe zoezi ya utoaji wa taka hizo imekuwa ikizidiwa na kusababisha taka kukaa zaidi ya wiki kitu ambacho ni hatari kwa wananchi mjini hapa.
" ninachojua zamani taka taka na yule wakala alikuwa makini na kazi yake lakini baada ya kusimamiwa na halmashauri vizimba vya hapa mjini vyote vinakaa na takataka muda wote kama wafanyabiashara tungekuwa na uwezo wa kuamua tungemuaomba arudi afanye kazi ya kuzoa takataka" alisema Bw Ndonya.
Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Bw. Venance Msungu alikiri kuwepo kwa tatizo hilo la uzoaji wa takataka alisimama kutokana kiasi cha fedha aliyokuwa akilipwa huku mji wa Njombe ukiendeea kuongezeka kwa uchafu.
Alisema kuwa katika kipindi cha miezi miwili baada ya wakala huyo Halmashauri hiyo imekuwa ikiendelea na zoezi hilo huku wakisubiri mwezi julai mwaka huu wa kutangazwa kwa mzabuni ambaye ataanza kufanya kazi hiyo ambaye atakuwa na vifaa vya kutosha tofauti na Halmashauri ambayo imekuwa ikitumia magari mawili pekee.
" hata waandishi wa habari inayostahili watu wanaongea kwamba uchafu bado tatizo jambo linaonyesha kukosa uelewa wa kulinganisha na sehemu zingine hapa nchini....zabuni zitafunguliwa mwezi huu wa sita na inapoanza mwezi julai tutakuwa na mzabini mwenye vifaa vya kutosha vya kutolea uchafu" alisema bw Msungu.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI