Sunday, June 29, 2014

SSEBO AHAMIA DIGITALI "E FM"

D4S_3487
MTANGAZAJI maarufu nchini wa vipindi vya Radio na Television Dennis Busulwa a.k.a Ssebo (pichani)amejiunga na Radio ya E FM ambayo imekwishajizolea umaarufu mkubwa jijini Dsm kwa kipindi kifupi tu kutokana na staili yake tofauti ya urushaji matangazo nchini.
Ssebo mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka mitano kwenye vituo mbalimbali vya Radio na TV amejizolea sifa na mashabiki lukuki katika tasnia hii ya utangazaji kutokana na staili na vituko vyake awapo hewani. 
“Mashabiki wangu watarajie mengi mazuri kutoka kwangu nikiwa na E FM”,alisema Ssebo.Ssebo anakutana na timu ya watangazaji wengine wakongwe kama Dj Majey, Dizzo One na Sos B waliokwisha anza kusikika Radioni hapo.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI