Sunday, June 29, 2014

MJAMZITO WA MIEZI NANE ASHIRIKI MASHINDANO YA RIADHA MITA 800, MAREKANI

MJAMZITO Alysia Montano amekimbia mbio za mita 800 za US Track na Field Championships jana, ingawa mamba yake imetimiza wiki 34.
Bingwa huyo mara tano wa taifa alitumia muda wa dakika mbili na sekunde, 32.13 kumaliza na kufuzu hatua nyingine, akiwa amebakiza wiki saba tu kabla ya kujifungua. 
Alysia Montano, mwenye mimba ya wiki 34 akishindana katika mbio za mita 800 za US Track na Field Championships.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 28, nyota wa zamani Chuo Kikuu cha California kumaliza wa mwisho haikumuumiza mbele ya umati Uwanja wa Hornet. 
Alianza kwa kasi na kuongoza kwa umbali wa mita 120 kabla ya kuanza kuishiwa nguvu.
Montano akiwa kwenye mashindano mjini Sacramento.
Montano akisubiri mbio kuanza katika siku ya ufunguzi wa USATF Outdoor Championship.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI