Sunday, June 22, 2014

MARTHA JOHN NDIE REDDS MISS IRINGA 2014

IMG_3895
Martha  John katikati akiwa na  washindi  wa nafasi ya pili na ya tatu baada ya kutangazwa mshindi wa taji la Redds Miss Iringa 2014 jana  katika ukumbi wa St Dominic huku mshindi wa  pili ni Elizabeth Titus na mshindi  wa tatu ni Foe Mkuchu.
(Picha na Francis Godwin)
…………………………………..
Na Francis Godwin blog, Iringa
MREMBO Martha  John kuuwakilisha mkoa  wa Iringa katika mashindano ya Redds Miss kanda ya nyanda  za  juu kusini baada ya kufanikiwa  kutwaa taji la Redds Miss Iringa 2014 baada ya  kuwashinda washiriki  wenzake nane  waliojitosa katika  kinyang’anyiro  hicho .
Martha alitawazwa  kuwa mrembo  wa mkoa  wa Iringa jana  usiku katika ukumbi wa St Dominic shindano  lililoshuhudia na kaimu mkuu wa mkoa wa Iringa Gerald Guninita .
Kutokana na ushindi  huo Martha kwa  sasa  ndie atakayeuwakilisha  mkoa wa Iringa katika  shindano la kumsaka Redds Miss Kanda ya  nyanda za juu  ,onyesho  linalotarajia  kufanyika  ijumaa ya  wiki ijayo mjini Iringa.
Jaji  mkuu  wa  shindano hilo Dosi Magambo  mbali ya  kumtangaza Martha  kuwa mshindi  wa kwanza katika kinyang’anyiro  hicho pia  alimtangaza  mshindi wa  pili kuwa ni   Elizabeth Titus na mshindi  wa tatu ni Foe Mkuchu
Akikabidhi  zawadi kwa  washindi  hao kaimu mkuu wa mkoa  wa Iringa Bw Guninita  alisema kuwa  ni imani yake na ya  serikali ya Rais Dr Jakaya  Kikwete  kuona wasanii na washiriki wa  michezo mbali mbali  wanaendelea  kufanya  vema katika nafasi  zao  ili kuiwezesha nchi kupiga hatua katika sanaa mbali mbali.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI