Monday, May 26, 2014

UMOJA WA MATAIFA WAONYA NJAA SOMALIA

Watoto wanaokabiliwa na njaa nchini Somalia.
UMOJA wa Mataifa umeonya kwamba huenda nchi ya SomaLia ikatumbukia tena katika janga la njaa kama lililotokea mwaka wa 2011 kutokana na ukosefu mkubwa wa usalama.
Kilimo cha chakula kimeathirika na mashambulizi ya mara kwa mara yanayotekelezwa na kundi la wanamgambo wa Al shabaab, na kusababisha maelfu ya watu wakimbilie mji mkuu wa Mogadishu kutokana na tishio la njaa.
Nchini Somalia, Umoja wa Mataifa umeonya kwamba huenda nchi hiyo ikatumbukie tena katika janga la njaa kama iliyotokea mwaka wa 2011 kutokana na ukosefu wa usalama uliokithiri.
Maeneo mengi nchini Somalia yamepokea kiwango kidogo sana cha mvua na mengine hayajapata mvua kabisa.
Mapigano yanayoendelea kati ya majeshi ya umoja wa Afrika na wanamgambo wa Al Shabab yameathiri sio tu kilimo lakini pia shuguli za usambazaji misaada katika maeneo mengi ya nchi.
Mashirika ya misaada yanasema Kutokana na hilo watoto wapatao elfu hamsini wanakabiliwa na utapia mlo.
Ukame mbaya zaidi ulikumba Somalia miaka mitatu iliyopita na kusababisha vifo vya watu 260,000.
Hali iliyoshuhudiwa wakati kabla ya ukame huo imeanza kudhihirika katika nchi ambayo zaidi ya watu milioni moja ni wakimbizi wa ndani na mtoto mmoja kati ya watano hufa kabla ya kufikia umri wa miaka mitano.
Umoja wa mataifa unatoa wito kwa wafadhili kutoa fedha zaidi kwani huenda ukosefu wa fedha ukasababisha kusitishwa kwa shuguli za kusambaza misaada.
Awali wito wa dola millioni 940 ulitolewa lakini maafisa wanasema kufikia sasa ni asilimia 17 pekee ya fedha hizo zilizotolewa.
Changamoto nyingine kubwa ni kwamba mzozo wa Somalia unakabiliwa na ushindani kutoka mizozo mitatu mikubwa katika mataifa ya Syria, Sudan Kusini na Jamuhuri ya Afrika ya kati ambako pia misaada inahitajika kwa kiwango kikubwa.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI