Thursday, May 29, 2014

KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AENDELEA NA ZIARA YAKE WILAYANI MBULU MKOANI MANYARA

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipokelewa mpakani mwa wilaya ya Hanang na wilaya ya Mbulu, Mkoani Manyara.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Uongozi sambamba na Watumishi wa hospitali ya Rufaa ya Haydom wilayani Mbulu,mkoani Manyara.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana haonekani pichani akitoka kukagua na kuzindua mradi wa ujenzi wa jengo la Upasuaji na wodi ya aki Mama na Watoto hospitali ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pichani kulia akiongozwa na mmoja wa Wauguzi hospitali ya Wilaya ya Mbulu wakielekea kukagua na kuzindua mradi wa ujenzi wa jengo la Upasuaji na wodi ya akina Mama na Watoto hospitali ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara.
Wananchi wakiwa wamemezuia gari la Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu kinana wakitaka wasikilizwe changamoto walizonazo ndani ya kata ya Keshkesh wilayani Mbulu mkoani Manyara.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na Diwani wa kata ya ya EShkesh kupitia chama cha CUF,Ndugu Naftari Kitandu alipohudhuria mkutano wa hadhara wa CCM,katika shule ya sekondari ya Yaeda chini,wilayani Mbulu mkoani Manyara.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisaidia kuweka zege kweye renta,ikiwa ni sehemu ya ushiriki wa ujenzi wa jengo la nyumba ya Mwalimu shule ya sekondari ya Yaeda chini Wilayni Mbulu mkoani Manyara. 
Sehemu ya daraja hilo la Haydoma kama lionekanavyo ujenzi wake ukiendelea
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (anaendesha mashine ya kushindilia) akishiriki ujenzi na ukaguzi wa daraja la Haydom wilayani Mbulu mkoani Manyara.
Nape Nnauye akishiriki ujenzi wa daraja la Haydom wilayani Mbulu mkoani Manyara.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizawadiwa meza yenye ramani ya Tanzania na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya rufaa ya Haydom,Dkt.Olav Espegren

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakaji wa mji wa Mbulu na vitongoji vyake,kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Mbulu,Kinana aliwataka wananchi wa mji huo kuachana na siasa zisizo na tija badala yake wajikite katika miradi mbalimbali ya kujiletea maendeleo na si vinginevy.Katibu Mkuu Ndugu Kinana ameambatana na Katibu wa NEC Itikad,siasa na Uenezi Nape Nnauye,wakiwa mkoani Manyara kwenye ziara ya Kukagua kuhimiza na kusukuma miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Chama,kukagua maandalizi ya uchaguzi ya serikali za mitaa,kusikiliza kero za wananchi na kuzitafututia ufumbuzi.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akimshukuru Diwani wa kata ya EShkesh kupitia chama cha CUF,Ndugu Naftari Kitandu alipohudhuria mkutano wa hadhara wa CCM,katika shule ya sekondari ya Yaeda chini,wilayani Mbulu mkoani Manyara.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa ameongozana na viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Mbulu na Mkoa wa Manyara wakiwasili kwenye mkutano wa hadhara uliofamyika ndani ya uwanja wa Haydom,wilayani humo.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa mji wa Haydom Wilayani Mbulu mkoani Manyara katika mkutano wa hadhara uliofamyika ndani ya uwanja wa Haydom. 
Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye akihutubia umati wa watu katika viwanja vya Mbulu mjini,wilayani Mbulu mkoani Manyara.
Sehemu ya umati wa wakazi wa mji wa mbulu wakishangilia jambo kwenye mkutano wa hadhara wa CCM,uliofanyika mjini Mbulu mkoani Manyara.
Sehemu ya umati wa wakazi wa mji wa mbulu wakishangilia jambo kwenye mkutano wa hadhara wa CCM,wakati Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye alipokuwa akihutubia mjini Mbulu mkoani Manyara.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI