Wednesday, May 21, 2014

CITY KUNUNUA WACHEZAJI

Manchester City kununua licha ya faini ya UEFA
MWENYEKITI wa Manchester City Khaldoon Al Mubarak amesema kuwa mabingwa hao wapya wa ligi kuu ya Uingereza wataimarisha kikosi chao licha ya marufuku waliopigwa na shirikisho la kandanda barani ulaya UEFA kwa kukiuka kanuni za matumizi ya fedha.
City ilipigwa faini ya pauni milioni £49m, mbali na kuruhusiwa kuwasajili wachezaji 21 pekee katika msimu huu mpya kushiriki katika ligi kuu ya mabingwa barani ulaya.
Kanuni hiyo inamaanisha kuwa Mabingwa hao watatumia pauni milioni £49m kuwanunua wachezaji mbali na idadi yeyote itakayopatikana kutokana na mauzo ya wachezaji.
City kununua Wachezaji licha ya vikwazo vya UEFA
Manchester city walitwaa ubingwa wa ligi msimu huu baada ya kukamilisha msimu wakiwa na pointi mbili zaidi ya wapinzani wao wa karibu Liverpool.
Kutokana na faini hiyo ya Uefa Manchester City wameshurutishwa kutotumia mshahara unaozidi ule waliotumia msimu huu katika msimu ujao wa 2014-15 .
Licha ya hayo Mubarak, amesema kuwa wamiliki wa klabu hyo wanafahamu fika matakwa ya UEFA na kuwa watamuunga mkono kwa hali na mali kocha Manuel Pellegrini wakati wa usajili msimu ujao.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 60 kutoka Chile mwaka 2013 baada ya Roberto Mancini kufutwa kazi.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI