Sunday, April 27, 2014

WATANZANIA WAISHIO MJINI SHANGHAI WALIVYOSHEREHEKEA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO WA TANZANIA

Baadhi ya Watanzania waishio katika mji 
wa Shanghai nchini China 
wamesherehekea maadhimisho ya 
Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania 
kwa kukutana pamoja na kuzungumza 
mambo mbali mbali ya kimaendeleo. 
Licha ya sherehe hizo za Miaka 50 ya 
Muungano,pia ziliambatana na kuwaaga 
baadhi ya wahitimu kutoka vyuo 
mbalimbali wanaotarajia kumaliza 
mwaka huu.
Baadhi ya Watanzania waishio 
Shanghai wakipiga picha ya 
pamoja katika shamra shamra 
za Maadhimisho ya Miaka 50 
Muungano wa Tanzania,
yaliyofanyika jana.
Baadhi ya Watanzania 
wanaomaliza masomo yao 
mwaka huu wakipiga picha ya 
pamoja mbele ya keki ya 
Muungano.
Mmoja wa wahitimu 
Bi. Hellen Shayo akipokea 
cheti kutoka kwa Mwenyekiti 
wa Watanazania waishio 
Shanghai cha kuwa 
mwanachama hai kwa 
kipindi chote alichokuwa hapa.
Baadhi ya Watanzania 
waliohudhuria sherehe 
za Muungano.
Watanzania wakikata keki ya 
Muungano huku wakiwa wa 
nyuso za bashasha 
zinazodhihirisha umuhimu 
wa siku hiyo adhimu.
Wakipata chakula.
wakiyarudi magoma 
kusherehekea Muungano.
Mdau wako wa nguvu akifurahia 
siku hii adhimu.
Baadhi wageni waalikwa.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI