Monday, April 28, 2014

WANAFUNZI WAPATIWA MAFUNZO YA USALAMA NA AFYA MAHALA PA KAZI NA BARABARANI

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Naibu Kamishna wa Polisi Mohamed Mpinga ( wa pili kulia) akiwasili katika viwanja vya Oyster Bay kushiriki semina ya mafunzo ya usalama na afya mahala pa kazi na usalama barabarani iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania kwa wanafunzi wa shule za msingi Oyster Bay, Msasani na Mbuyuni. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Idara ya Usalama, Afya na Mazingira wa Vodacom Karen Lwakatare.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Naibu Kamishna wa Polisi Mohamed Mpinga akizungumza wakati wa semina ya usalama na afya mahala pa kazi na usalama barabarani iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania kwa wanafunzi wa shule za msingi Oyster Bay, Msasani na Mbuyuni iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Oyster Bay jijini Dar es salaam. Kushoto ni Meneja wa OSHA kanda ya Pwani Jerome Materu na Mkuu wa Idara ya Usalama, Afya na Mazingira wa Vodacom Karen Lwakatare.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Naibu Kamishna wa Polisi Mohamed Mpinga akizungumza wakati wa semina ya mafunzo ya usalama mahala pa kazi na usalama barabarani iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania kwa wanafunzi wa shule za msingi Oyster Bay, Msasani na Mbuyuni. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Usalama, Afya na Mazingira wa Vodacom Karen Lwakatare.
Meneja wa Mamlaka ya Usalama na Afya mahala pa kazi (OSHA) kanda ya Pwani Jerome Materu akizungumza wakati wa semina ya mafunzo ya usalama mahala pa kazi na usalama barabarani iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania kwa wanafunzi wa shule za msingi Oyster Bay, Msasani na Mbuyuni. Kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Naibu kamishna wa Polisi Mohamed Mpinga na Mkuu wa Idara ya Usalama, Afya na Mazingira wa Vodacom Karen Lwakatare(kushoto).
Mfanyakazi wa Kampuni ya Vodacom Tanzania Ammy Mlay akipima uelewa wanafunzi kuhusu amsula ya uslama na afya mahala pa kazi wakati wa semina ya mafunzo ya usalama mahala pa kazi na usalama barabarani iliyoandaliwa na kampuni ya Vodacom kwa wanafunzi wa shule za msingi Oyster Bay, Msasani na Mbuyuni mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Oyster Bay jijini Dra es salaam. Semina hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya usalama na afya mahala pa kazi duniani.
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Happy Paul (kushoto) na Ammy Mlay wakiwaonesha wanafunzi (hawapo pichani)kanuni ya lazima namba nne na sita ya usalama kazini kwa wafanyakazi wa Vodacom ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha wafanyakazi wakati wote wanakuwa salama na wenye afya wanapotimiza majumu yao.Vodacom kwa ksuhirikiana na jeshi la polisi mkoa wa Kinondoni mwishoni mwa wiki waliendesha semina ya masuala ya afya na usalama kazini kwa wanafunzi wa shule za msingi Oyster Bay, Mbuyuni na Msasani.
Meneja wa Masuala ya Sheria Upendo Haji akimuonesha mmoja wa wanafunzi aliyehudhuria mafunzo ya usalama na afya kazini iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi Oyster Bay, Mbuyuni na Msasani jijini Dar es salaam kaununi ya lazima nambari sita ya usalama inayotumiwa an Vodacom kuhamasisha usalma wka wafanyakazi wake wawapo kazini. Vodacom kwa kushirikiana na jeshi la polisi mkoa wa Kinondoni mwishoni mwa wiki waliendesha semina ya masuala ya afya na usalama kazini kwa wanafunzi wa shule za msingi Oyster Bay, Mbuyuni na Msasani.
Mwanafunzi wa shule ya msingi Msasani ya jijini Dar es salaam akizima mota kutumia kifaa wakati wa semina ya uslama na afya kazini iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania kw akushirikiana na jeshi la polisi. Wanaomsimamia mwanafuzni huyo ni Karen Lwakatare (kushoto) na ofisa kutoka kampuni ya ulinzi ya Security Group.

KAMPUNI ya mawasiliano ya simu ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na jeshi la Polisi Kanda ya mkoa wa Kinondoni wamewapatia mafunzo ya usalama sehemu za kazi kwa wanafunzi wa shule za msingi Msasani, Mbuyuni na Oysterbay zote za wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wa Vodacom wao wametoa mafunzo ya usalama sehemu za kazi kwa wanafunzi hao wakiamini kuwa wao ndio wafanyakazi wa baadae ambao ndio tegemeo la kukua kwa uchumi wetu.
Akizungumzia juu ya mafunzo hayo Mkuu wa Idara ya Afya na Usalama,Karen Lwakatare amebainisha kuwa wao watatoa elimu na mafunzo juu ya usalama mahala pa kazi lengo ikiwa ni kufafanua umuhimu wake.
“Mafunzo haya yanalenga kwanza kabisa kuwafafanulia nini maana ya usalama mahala pa kazi, wakishaelewa hivyo basi zoezi la kutoa elimu kwetu litakuwa ni kazi rahisi. Wanafunzi wanauelewa mkubwa na ni rahisi kushika mambo, mbali na hapo wanaishi katika mazingira ambayo ni lazima wafahamu vitu hivi.” Alisema Lwakatare na kuongezea kuwa, “Kwa mfano wanafunzi ambao tunawapa mafunzo hapa shule zao zipo katikati ya jiji na kuzungukwa na barabara kuu hivyo basi lazima wapewe mafunzo haya.”
Lwakatare aliendelea kwa kusema kuwa mafunzo hayo yametolewa kwa wanafunzi wa darasa la tatu, nne na tano kutoka kila shule ambazo zimetajwa hapo awali. Wanafunzi hawa wataelezwa ni kwa nini kuna umuhimu wakuzingatia mafunzo hayo kwani hata wao miaka ya baadae watakuja kuwa wafanyakazi na lazima watakuja kukumbana nazo.
“Tunategemea wanafunzi hawa siku za baadae wamalize masomo yao waje kuwa wafanyakazi na wengine wanaweza kubahatika na kuajiriwa na Vodacom. Mafunzo haya ya mara kwa mara yana faida kubwa na pia nina amini wao ndio watakuwa mabalozi kwa wanafunzi wenzao, marafiki, wazazi na hata ndugu na jamaa huko waendapo.” Alimalizia Lwakatare
Kwa upande wa jeshi la polisi mkoa wa Kinondoni wao watatoa mafunzo kwa wanafunzi hao juu ya kutumia vifaa mbali mbali vya kiusalama na usalama barabarani ili kuwapa uelewa zaidi
Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Kinondoni, Kamanda Mohammed Mpinga amesema kuwa wanafunzi hawa wengi wao wanatumia barabara wakati wa kuja shuleni na kurudi nyumbani.
“Tumeona kuna umuhimu kwa wanafunzi hawa kujua alama mbali mbali za barabarani pamoja na matumizi yake mbali na kuishia kuziona tu kwa macho. Kama suala la usalama barabarani lazima lipewe kipaumbele kwani kama tujuavyo jiji la Dar es Salaam lina changamoto nyingi ukizingatia magari sasa yamekuwa mengi kitu ambacho kunakuwa na mikanganyiko mingi.” Alimalizia Kamanda Mpinga.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI