Sunday, April 27, 2014

NGORONGORO HEROES YAWAFUNGASHIA VIRAGO VIJANA WENZAO WA KENYA KWA MIKWAJU YA PENATI 4-3

Mshambuliaji wa Ngorongoro, Ally Bilal (kulia) akichuana na beki wa Kenya, Geofrey Shivekwa, wakati wa mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za michuano ya Kombe la Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 20, zinazotegemea kufanyika mwakani nchini Senegal. 
Katika mchezo huo Ngorongoro Heroes imewaondosha mashindanoni majirani zao wakenya kwa mikwaju ya penati, ambapo dakika 90 zilimalizika kwa kutoka suluhu na kuamuriwa kupigwa mikwaju ya penati kutokana na kwamba katika mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Kenya timu hizo zilitoka sare ya 0-0. Kenya wameondoshwa kwenye michuano hiyo kwa jumla ya penati 4-3 na kusonga mbele.
                             
Iddi Suleiman  wa Ngorongoro (kulia) akichanja mbuga.
     

Wachezaji wa Ngorongoro, wakishangilia ushindi baada ya kushinda kwa penati na kusonga mbele.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI