Tuesday, April 22, 2014

LOGARUSIC KURUDI KWAO PASIPO KUSUBIRI MKATABA MPYA

KOCHA wa Simba, Zdravko Logarusic amesema ndani ya siku chache atarejea kwao Croatia.
Loga amesema ameamua kuondoka kabla ya kupata mkataba mpya wa Simba kwa kuwa mambo yanakwenda taratibu.
“Mambo yanakwenda taratibu sana na muda unakimbia, acha nirudi nyumbani kwanza.
“Nafikiri ndani ya siku tatu nitakuwa nimerejea nyumbani. Hivyo mengine tutajua,” alisema.
Klabu ya Simba imesema ina siku kadhaa ya kujadili suala lake na ikaomba subira itangulizwe.
Lakini kocha huyo amesisitiza, ukifika wakati wa kuondoka, hatajali kama tayari kapewa mkataba mpya au la.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI