Monday, April 7, 2014

KINANA AJITWISHA MGOGORO SUGU WA SHAMBA LA TAASISI YA EFATA NA WANANCHI SUMBAWANGA MKOANI RUKWA

Sehemu ya umati wa wananchi ukimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa CCM, NduguKinana (katikati) alipokuwa akiwahutubia katika Kijiji cha Mawenzusi,wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa.
Kinana alisema kitendo cha Serikali kuchukua shamba hilo na kulibinafsisha kwa Efatha bila kuwapa taarifa wanakijiji ni kuwadhulumu wanakijiji hao. "Tutakwenda kulifanyia kazi suala hili haiwezekani shamba la zaidi ya ekari 10,000 likae tu bila shughuli yoyote, Nawaambieni hivi. shamba lenu mmedhulumiwa na Serikali, hili wala haliitaji digrii 4 kujua mtu ameporwa ardhi. 
"Hapa hakuna muwekezaji kunawanyonyaji, tumeurudisha ukabaila kwa mlango wa nyuma. Ukabaila ni mtu kuchukua ardhi na kukodishia wengine", alisema Kinana. Alisema wakati Serikali inalibinafsisha shamba hilo kwa Efatha ilitakiwa wawaombe radhi wanakijiji na kuitisha mkutano wa hadhara kuwa wao wameshindwa kuliendesha shamba hilo sasa wanalirudisha kwao
"Hao unaowaita wawekezaji wanachukua ardhi ili wakakope benki na mwisho wa siku wanawageuza wenye ardhi manamba kwa kuwakodishia mashamba", alisema. Pia,alisema Serikali imekuwa ngumu kwa kutoa uamuzi, wakati Rais Kikwete alishatoa uamuzi kuwa shamba hilo lirudi kwa wananchi jambo ambalo bado halijatekelezwa.
Alisema atahakikisha shamba hilo linarudi kwa wananchi kutokana na agizo alilolitoa Rais.Mkuu wa Mkoa aliunda tume kutokana na mgogoro huo, ambapo walibaini kuwa watu wanafanyiwa vitendo vya kikatili na kuwa shamba hilo linakaa bila shughuli yoyote na pia, ni shamba la wananchi
"Baada ya tume hiyo kumaliza utafiti katika shamba hilo nakupitia mikataba,walipeleka maombi Serikali Kuu kuwa eneo dogo achukue muwekezaji na eneo kubwa wapewe wananchi,nitahakikisha hili linatekelezwa kwa sababu Serikali ni ngumu kutoa uamuzi", alisema.
Ndugu Kinana amemaliza ziara yake ya siku sita mkoani Rukwa kwa kutembelea wilaya zote za mkoa huo na kujionea shughuli mbalimbali za maendeleo ya wananchi,kukagua na kuhamasisha utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya chama hicho,ikiwemo na kusikiliza matatizo ya wananchi,Kinana anaelekea mkoani Kigoma ambako pia atafanya ziara.
Mkazi wa Kijiji cha Mawenzusi, Kata ya Molo, Nuru Togwa akionesha jinsi masikio yake yalivyokatwa na anayedaiwa kuwa mwekezaji wa shamba lililokuwa la wananchi na kumilikishwa na Shirika la Chakula la Taifa (NAFCO) na baadaye shamba hilo kuuziwa mwekezaji huyo Taasisi ya EFATHA.Kulia ni Mbunge wa jimbo la Sumbawanga Mjini,Mh.Aesh Hilary.
Sehemu ya Wananchi na msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana wakielekea kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mawenzusi,kata ya Molo wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na mmoja wa wanakijiji cha Mawenzusi alipowasili katika kijiji hicho, akiwa katika ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM.Mwanakijiji huyo ameshika karatasi lenye maandishi yenye kilio cha kutaka wanakijiji hao kurejeshewa shamba hilo lenye ukubwa wa hekari 10,000. Kinana ameahidi kulitafutia ufumbuzi suala hilo ili wananchi warejeshewe haraka shamba hilo.
Baadhi ya Wananchi na mabango yao.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Mbunge wa jimbo la Sumbawanga Mjini,Mh.Aeshi Hilary wakipokelewa na wananchi wa kijiji cha Mawenzusi,kata ya Molo wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa.
Kinana (hayupo pichani) akiwa na wananchi wakiwasili kwenye mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mawenzusi.
Wanachama wa CCM wakila kiapo cha utii wa chama hicho baada ya wanachama wapya zaidi ya 300 kukabidhiwa kadi za CCM baada ya kujiunga.
Mjumbe wa NEC/CCM, Ally Karume akihutubia katika mkutano wa hadhara ambapo aliwataka wananchi kuudumisha muungano wa Serikali mbili badala ya tatu aliyodai kuwa ni mzigo.
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa ,Hypolitus Matete na Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini, Hilary Aeshi katika mkutano huo wa hadhara.
Kikundi cha ngoma za utamaduni cha Kanondo kikitumbuiza katika mkutano huo wa hadhara.
Sehemu ya shamba la Taasisi ya EFATHA. linaliotakiwa kurejeshwa kwa wananchi katika Kijiji cha Mawenzusi, Kata ya Molo, Sumbawanga Mjini.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI