Wednesday, April 9, 2014

AJABU NA KWELI: KUTANA NA MDOLI MTU 'BARBIE DOLL' - ANASTASIYA SHPAGINA

NI MWANADADA aneyejulikana kwa jina la Anastasiya Shpagina ambaye ni mmoja tu kati ya wasichana wengi kutoka Ukaraine ambao wamejibadilisha miili yao kwa kufanyiwa plastic surgery na kuwa katika miundo ya midoli na wenyewe hujiita 'Anime'…. 
...Usijedhani ni mdoli tu na si mtu kweli, amini usiamini dunia hii haiishi vijimambo, huyu ni mtu kweli na si feki ambaye ameamua kujibadilisha na kuonekana hivi...
Anastasiya alifanyiwa upasuaji na kupunguzwa kiuno chake, hali nyama…
cha kushangaza mwanadada huyu anataka kufanyiwa upasuaji zaidi kukipunguza zaidi kiuno chake na kuyafanya macho yake yaonekane makubwa zaidi ya yanavyoonekana kwa sasa, 
Haya yote yanatokea akiwa na umri wa miaka 19
Akiwa na doll mwingine aitwaye Valeria Lukyanova (kushoto)
Daaaaaah! wangekuwa dada zako ungefanyaje sasa….!!!!??? 
Ndo Basi tena..
Huyu ni Venus Angelic kutoka London….
Wanadada hawa wan a ukurasa wao wa Facebook uitwao HUMAN DOLLS.... Waweza pia utazama na kushuhudia yote haya.
Ukiacha na upasuaji huo waliofanyiwa, wanadada hawa hutumia muda mwingi kukaa katika vioo vyao kufanya make up kwaajili ya kutengeneza macho yao yawe na muonekano wa midoli hiyo maarufu kama 'Barbie' Barbie Dolls, kwa mfano Anastasiya yeye hutumia zaidi ya dk 30 kwa jicho moja, kulichora na kulipaka vitu anavyovijua yeye ili apate muonekano huo wa mdoli.
Ukitembelea katika vyanzo mbalimbali utagundua kuwa watu wengi wanashauku ya kujua hali za afya za akina dada hawa ambao wameona wajibadili maumbo yao ya kawaida na kuwa midoli watt. 
Ambapo dada mmoja ajulikanaye kama Valeria anasema anatarajia kujibadili kwa kupigwa na mionzi ili awe anachajiwa kama vile unavyochaji simu na kuitumia badala ya kula kama kawaida kwani anaona kula ni shida sana….. Anamaanisha anataka kuwa mdoli kabisaaaa. Daaah sasa huyu ndio shida kabisaa.
Hapa chini ni Anastasiya Shpagina akifanya mahojiano na kituo kimoja nchini Ukraine. Hebu nawe shuhudia maajabu haya!!!
                       
Haya sasa kwa wale dada zetu wa kibongo wanaopenda kuiga kila kitu, nadhani hili mmeliona, jamani ni vyema vingine ukaangalia tu kisha ukaishia kushangaa lakini si kuiga, likiwemo hili. 

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI