Saturday, March 8, 2014

WAUMINI WANYWESHWA MKOJO WA NG'OMBE, SOMA UJUE CHANZO.

            

Kwa mujibu wa Daily Mail, Waumini wa Hindu wanaamini kwamba Ng'ombe ni mnyama aliyebarikiwa na wanasema mkojo wake unasaidia kuponya vitu mbalimbali. Japokuwa wanasisitiza kwamba mkojo wa ng'ombe mtu anaotakiwa kunywa ni ule wa ng'ombe bikira yaani watanzania wenzangu ni yule ng'ombe ambaye hajawahi kuzaa. 

Pia, mkojo unatakiwa kuchukuliwa kabla ya jua kutoka na hapo ndipo mkojo huo unapokuwa na matokeo mazuri.

Chanzo hicho kimeongeza kwamba unywaji wa mkojo wa ng'ombe ndio njia bora ya kuondoa vipara kwenye kichwa kwa wale walio na vipara.

 
Jairam Singhal (miaka 42) ambaye amekuwa akinywa mkojo wa ng'ombe kwa zaidi ya muongo mmoja ametoa ushuhuda juu ya faida za kiafya zinazosababishwa na mkojo huo, hapa anasema:
    ‘Nilikuwa na kisukari, ila toka nimeanza kunywa mkojo wa ng'ombe, kiwango cha kisukari nimeweza kukikabili. Mtu mmoja aliniambia kunywa mkojo wa ng'ombe ni mzuri kwa afya. Tumekuwa na ng'ombe hapa kwa zaidi ya miaka 12, hivyo kitu cha kwanza kukifanya asubuhi ni kuchukua mkojo wa ng'ombe na kuunywa.’



Tupunguziane kidogo… mmmmh!

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI