Sunday, March 16, 2014

MANCHESTER UNITED VS LIVER POOL :: ARSENAL VS TOTTENHAM LEO JUMAPILI

1 2297c

SIKU ya leo imekuwa ni siku ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wengi duniani katika uwanda wa soka kwani ni siku inayozikutanisha takribani nne kali na maarufu duniani.

Mechi hizo ni Manchester United dhidi ya Liverpool, na Arsenal dhidi ya Tottenham, ambapo katika mechi ya Manchester United na Liver, kama Man U wanafungwa au wanatoka sare hivi leo, ndoto za kuchukua nafasi ya nne zitakuwa ndogo sana, na wakifungwa watashindwa kuchukua nafasi hiyo ya nne kabisa.

Vile vile mechi hii ni muhimu sana kwa Liverpool. Kama Liverpool wanashinda leo wataweza kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao. Na kama Liverpool wanashinda, Brendan Rodgers atabadilisha lengo lake kwani mwanzoni mwa msimu huu Brendan Rodgers alisema lengo la Liverpool msimu huu ni kuchukua nafasi ya nne.

Lakini, kama Liverpool wanawafunga Manchester United ugenini, bila shaka 'The reds' wana nafasi na uwezo wa kushinda ligi na hii itakuwa lengo la Rodgers, ambapo Arsenal pia wana ndoto ya kushinda ligi msimu huu.

Jana Chelsea walifungwa na Aston Villa kwa hiyo Arsenal wanaweza kupunguza pointi ambazo wanazihitaji kuwafikisha Chelsea. Lakini, kama Arsenal wanafungwa leo, 'The gunners' watakuwa na mlima mkubwa kuwakamata Chelsea, Man City na labda hata Liverpool.

Vile vile kama Manchester United, Tottenham pia wana ndoto na lengo la kuchukua nafasi ya nne. Kwa sasa wameshika nafasi ya tano lakini Arsenal ambao wapo katika nafasi ya nne wamewapita kwa pointi sita na Tottenham wamewazidi Arsenal mechi moja. Kwa hiyo, ni muhimu sana Tottenham kuhakikisha nyavu zao hazitingishwi.

Waingereza wana msemo: 'The ball is round'. Wana maana, kwamba chochote kinaweza kutokea katika mpira. Ama kweli mpira ni dakika 90 hivyo chochote kinaweza kutokea katika mechi hizi.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI