Tuesday, March 11, 2014

MALAYSIA YAENDELEA KUITAFUTA NDEGE ILIYOPOTEA

Malaysia_Airlines_image17_553e8.jpg
SHUGHULI ya utafutaji wa ndege ya abiria ya Malaysia imeendelea kushika kasi baada ya kuwepo kwa hali ya sintofahamu na wasiwasi mwingi kutoka kwa ndugu za watu waliopotea katika ndege hiyo.


Mamlaka nchini Malaysia zinasema wameongeza mipaka ya eneo la utafutaji mara mbili Zaidi, huku China ikiwa imepeleka mitambo 10 ya satelaiti kwa ajili ya kusaidia kutafuta ndege hiyo.



Mkuu wa Idara ya anga Azharuddin AbdulRahman amewaambia waandishi wa habari kuwa eneo la kusaka ndege hiyo limeongezeka mara mbili kutoka maili 50 za bahari mpaka maili 100.

Ndege hiyo iliyokua imebeba watu 239 ilipotea bila kutoa taarifa yeyote na hakuna dalili yeyote mpaka sasa ya kupatikana kwa mabaki ya ndege hiyo.

WAKATI HUO HUO
Kampuni ya google imekanusha habari zilizotapakaa kwenye mitandao mbalimbali duniani kwa kuweka picha ya Google Map ambayo inaonesha ndege ya Malaysia Airline ikiwa imedondondoka ndani ya maji. 

Msemaji wa google nchini Malaysia amesema
"Ndio yawezakuwa picha zipo zinaonekana lakini hiyo sio picha ya muda halisi kutokana na picha ya satellite, kwani picha hizo zawezakuwa ni picha zilizowekwa wiki au miezi kadhaa iliopita "

Hii imetokana na kutapakaa kwa picha inayoonesha ndege ya Malaysia Airline imedondoka kwenye maji. (katika picha)

fake_plane_554d0.jpg

Mpaka sasa meli zipatazo 40 na ndege 34 zinazunguka bahari inayizunguka maeneo ya Vietnam na Malysia wakitafuta ndege ya Malaysia Airline iliyopotea toka jumamosi.

Nchi zinazoshiriki kuitafuta ndege hiyo ni Australia, China, Thailand, Indonesia, Singapore, Vietnam, Philippines, New Zealand na Marekani.

Kwa hisani ya mjengwa blog

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI