Friday, December 7, 2012

MASHINDANO YA UHURU MARATHON YAZINDULIWA DAR


Mgeni Rasmi katika Hafla ya Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon), Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenela Mukangara akikata utepe kuashiria kuwa tayari mashindano ya Uhuru Marathon yamezinduliwa rasmi.
WADAU wa michezo wametakiwa kujitokeza na kuanzisha mashindano ya michezo mbalimbali kwa lengo la kuongeza fursa za ajira na kuitangaza Tanzania Kimataifa.

Akizindua  mashindano ya Riadha  ya Uhuru Marathoni Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na michezo Dakta Fenella Mkangara amesema kuwa mashindano ni muhimu yakawa endelevu kwa mustakabali wa kuenzi Uhuru wa taifa hili.
Dkt. Fenela Mukangara amesema mbali na kuenzi uhuru wa Tanzania mashindano hayo yatatoa fursa kwa vijana kujipatia ajira kwa kushiriki katika michuano ya Uhuru Marathoni ambayo itafanyika Desemba 8 kila mwaka ambapo kwa kuanzia itafanyika hapo mwakani.
''Tunaka kuona mpango huu unawanufaisha wanariadha na kuwa nafasi ya ajira kwao kwa kuwaingizia kipato, na sisi kama wananchi, wadau tunaopenda michezo tuhakikishe tunawaunga mikono'' Alisema Dkt. Fenela Mukangara.
UHURU WETU, AMANI YETU, UMOJA WETU. Ni kauli mbiu inayoyaongoza mashindano hayo ambapo yataanza hapo mwakani.
Waziri Mukangara pia amesema ni vyema michuano hiyo ikawa endelevu kwa minajili ya kuenzi malengo yake ambayo mafanikio ya Uhuru ikiwemo amani, umoja na mshikamano wa Tanzania tulionao hadi leo.
Mgeni Rasmi katika Hafla ya Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon), Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenela Mukangara akisoma hotuba yake aliyoiandaa wakati wa Uzinduzi wa Uhuru Marathon.
Naye Mkurugenzi wa Intellectual Communications Innocent Melleck amesema michuano hiyo itaweza kuitangaza Tanzania katika utalii kwa kutumia Tovuti rasmi iliyozinduliwa na wanamichezo kutoka nje ya nchi watakaoshiriki katika michuano hiyo.
Mkurugenzi wa Intellectual Communications Bw. Innocent Melleck akieleza nia na madhumuni ya kampuni yake kuanzisha mashindayo hayo ya Uhuru Marathon.

Uzinduzi huo ulisindikizwa na burudani mbali mbali, akiwemo mrisho mpoto ambaye aliwavutia wengi kwa tungo zake mahiri.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI