Tuesday, December 4, 2012

ILIVYOKUA UWANJANI: KILI STARS VS RWANDA , ZANZIBAR VS BURUNDI



Wachezaji wa Bara wakimpongeza Bocco baada ya kufunga bao la pili katika Robo Fainali ya kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge dhidi ya Rwanda. Bocco alishangilia huku akichechemea baada ya kufunga bao hilo kutokana na kuumia, baada ya kugongwa na kipa wa Rwanda, Jean Claude Ndoli wakati anaenda kufunga. Bara ilishinda 2-0 na kutinga Nusu Fainali. 
Mfungaji wa penati ya mwisho na ya ushindi ya Zanzibar, Abdallah Othman akikimbia kushangilia baada ya kumaliza mechi ya Robo Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge dhidi ya Burundi kwenye Uwanja wa Lugogo mjini Kampala - Uganda, Zanzibar ilishinda kwa penati 6 - 5 baada ya sare ya 0 - 0 ndani ya dakika 90.
Kaseja amedaka, huku Yondan akiwa tayari kumsaidia
Manahodha wakisalimiana kabla ya mechi, Juma Kaseja wa Bara kulia na Haruna Niyonzima wa Rwanda kushoto
Kikosi cha Rwanda
Kikosi cha Bara leo
Watanzania waliojitokeza kuisapoti timu yao
Shomary Kapombe akimdhibiti Dadi Birori 
Athumani Iddi 'Chuji' akiruka juu kulia kuokoa
Amri Kiemba akimkokota mchezaji wa Rwanda
Kocha Milutin Sredojevic 'Micho'
John Bocco akiwashughulisha mabeki wa Rwanda
Refa akionyesha mpira kati, kuashiria goli limefungwa, baada ya Kiemba anayekimbia nyuma yake kufunga bao la kwanza
Bao la Kiemba
Mwinyi Kazimoto kulia akimburuza mchezaji wa Rwanda
Ulinzi mkali langoni mwa Rwanda, lakini bado mbili zilipenya
Bocco akisababisha
Jean Claude Ndoli wa Rwanda aliyeruka hewani kudaka moja ya michomo ya hatari iliyoelekezwa langoni mwake
Mwinyi huyooo
Ndikumana chini, shughuli ya Issa Othman Ally kushoto
Aggrey Moris akimdhibiti mshambuliaji wa Burundi
Suleiman Kassim Selembe kulia akikokota ngoma
Abdulaghan Gullam akitafuta mbinu za kumtoka mchezaji wa Burundi
Aggrey Morris akipanda kusaidia mashambulizi baada ya kuokoa
Selembe akipasua katikati ya watu
Issa Othman Ally akiondoka na mpira mbele ya wachezaji wa Burundi
Jaku Juma akipambana na beki wa Burundi
Ndikumana akijuta baada ya kukosa mkwaju wa penati
Balozi wa Tanzania nchini Uganda, kulia akimpongeza kocha wa Zanzibar
Wachezaji wa Zanzibar wakimpongeza Abdallah Othman
Wachezaji wa Zanzibar na baadhi ya viongozi wakimpongeza Abdallah Othman katikati aliyesujudu

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI