NYUMBANI KITAIFA

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BIASHARA

Ulimwengu wa habari.

MATAIFA MENGINE

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BURUDANI

Ulimwengu wa habari.

MAAJABU DUNIANI

Ulimwengu wa habari.

Sunday, May 24, 2015

ZIFAHAMU CATEGORIES ZOTE ZA 'MAMA' MTV AFRICA MUSIC AWARDS 2015 HAPA!!!

mama
MTV Africa Music Awards 2015 zinarudi tena kwa msimu wa tano.

Tujiandae kuwaona mastaa kwenye Red carpet South Africa ambako Tuzo za MTV zitakuwa zinatolewa pale Durban International Convention Centre July 2015.
Hapa nina categories zote zilizotambulishwa.
 MTV
Tuna mastaa wetu ambao Afrika inawajua kabisa kwenye muziki.. wewe unadhani nani na nani watatuwakilisha hapa?

MANDHARI MWANANA YAWAVUTIA WATALII WA NDANI HIFADHI YA TAIFA YA MLIMA KILIMANJARO

Baadhi ya watalii wa ndani wakiwa katika gari kuelekea kilele cha Shira katika hifadhi ya mlima Kilimanjaro.
E86A7743 (800x533)
Kundi la Pili la watalii wa ndani wakiwa katika eneo la uwanda wa Shira mara baada ya kufika kwa usafiri wa gari hadi katika eneo hilo.
Afisa Masoko wa Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro akizungumza na watalii wa ndani kabla ya kuendelea na safari ya kutembelea vivutio mbalimbali viyoko katika uwanda wa Shira yakiwemo mapango ya Shira Caves.
Safari ya kuelekea katika vivutio vya asili katika uwanda wa Shira ,hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro.
Makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika na Biashara (MOCU),Faustine Bee akitizama mandhari katika uwanda wa Shira wakati akipanda mlima huo kuelekea katika mapango ya Shira.
Raia wa kigeni wakipata kumbukumbu katika maeneo mbalimbali ya hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro.
Watalii wa ndani wakichukua taswira mbalimbali mara baada ya kufika kilele cha Shira ndani ya Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro.
Makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika na Biashara (MOCU) Faustine Bee akichukuliwa taswira na kijaa wake baada ya kufika eneo la Shira hut.
Safari ya kuelekea kutizama mapango ikiendelea.
Watalii wa ndani wengine waliweka kumbukumbu.
Safari ikaendelea.
Baada ya kupanda vilima watalii wa ndani pia walipata nafasi ya kupumzika.
Watalii wa ndani wakiwa katika mapango ya Shira ambayo yalitumiwa na wapagazi wakati wa zoezi la kupandisha watalii wakati wa safari ya kuelekea kilele cha Uhuru.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika na Biashara (MOCU) Prof. Faustine Bee akifurahia mara baada ya kuingia katika mapango ya Shira.
Makamu mkuu wa Chuo kikuu cha Ushirika Prof. Faustine Bee akizungumza jambo kuhusu miamba iliyoko katika mapango hayo.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Mwanga wakiongozwa na meneja wao, Innocent Silayo(wa pili toka kulia) wakishuka mara baada ya kutembelea vivutio  katika uwanda wa Shira.
Mmoja wa watalii wa ndani, Dkt Gaspaer Mpehongwa ,(Kulia) akizungumza jambo na wageni wakati akiwaonesha moja ya picha inayoonesha namna ambavyo volcano ilivyo ripuka na kutengenza uwanda wa Shira.
(Picha na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya Kaskazini).

ANGALIA *VIDEO* YA MTOTO WA SIKU MBILI ALIYEFANYIWA UNYANYASAJI WA KUTISHA

2day

JAMII nyingi kila moja imekua na imani tofauti juu ya jambo fulani lakini baadhi ya imani hizo hufanana kutokana na tukio husika.
Hii tunaweza kuita moja ya tukio la unyanyasaji kwa mtoto, baada ya mama mmoja Rakesh Kumar, ambaye  ni mganga wa kienyeji huko India kumlazimisha mtoto wa siku mbili kutembea akiamini atapona.
Mtoto huyo alikuwa akisumbuliwa na homa kali na wazazi wake kuamua kumpeleka kwa mganga huyo ambaye alimchukua na kumlazimisha kutembea akiwa uchi huku akiwa amemkaba koo.
Pamoja na watu wengi kushuhudia tukio hilo hakuna aliyetokea kumsadia mtoto huyo ambaye alikuwa akilia sana baada ya kulazimishwa kutembea.
Baada ya tukio hilo mama mzazi pamoja na mganga huyo walifunguliwa mashtaka huku mtoto huyo akipelekwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Monday, May 18, 2015

WATATU MBARONI KWA UVUNJAJI NA WIZI MKOANI DODOMA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME
Malializokamatwa nazo mtuhumiwa ONESMO S/O LUPILI YEYO
Baadhi ya vifaa alivyokuwa anatumia 
Na: Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
******
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia mtu mmoja aliyekamatwa huko katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Yarabi Salama (Yarabi Salama guest house) katika Manispaa ya Dodoma.
Aliyekamatwa anafahamika kwa jina la MASAGARA S/O MESO, Mwenye miaka 40, Kabila Mzanaki wa Butiama, akiwa na funguo bandia 19, Master key 2, Bisibisi 2, Kisu kimoja, Tupa moja, Mikasi mitatu mikubwa ya kukatia vyuma, Msumeno ya kukatia vyuma mitano, Mitalimbo ya kuvunjia miwili, Adjustable spanner 1, Kipande cha bomba, Biti za kutobolea vyuma na mbao 8, Simu mbili aina ya Tecno na Nokia, Simu ya bandia ya Nokia, Pochi za mfukoni mbili, Hati ya dharura ya kusafiria, Betri ya simu moja, Nyenzo moja ya mbao, Nguo za kubadilisha, Madawa mbalimbali ya kienyeji, Kipande cha nondo kimoja na Irizi moja aliyokuwa amefunga sehemu ya juu ya mkono wa kushoto akiwa amehifadhi kwenye begi lake kwa maandalizi ya kufungua vyumba vya wapangaji wengine na kuvunja mita ili aibe.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema baada ya mahojiano na mtuhumiwa huyo, amekiri kufanya uhalifu wa kuvunja nyumba mbalimbali za kulala wageni na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu huko Mikoa ya Mwanza, Geita, Shinyanga, Tabora na hapa Dodoma. Uchunguzi zaidi unaendelea ili kubaini watuhumiwa wengine anaoshirikiana nao pamoja na matukio aliyofanya.
Kamanda MISIME amesema nimuhimu kwa wenye nyumba za kulala wageni kuwa makini na wageni wanaowapokea kwani baadhi yao wanapanga vyumba kwa lengo la kufanya uhalifu wa kuwaibia wateja wengine au vifaa vya hoteli kama TV, DVD Player, Ving'amuzi n.k na wakati mwengine hufanya vitendo vya wizi mitaani.
Pia Kamanda MISIME amesema katika hatua nyingine Jeshi hilo linamshikilia ONESMO S/O LUPILI YEYO Mwenye miaka 22, Muha, Mwenyeji wa Mkoa wa mwanza ambaye alikuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) Kitivo cha Sayansi ya Jamii mwenye namba za usajli T/UDOM/2013/01760 kozi ya Uhasibu mwaka wa kwanza ambaye alisimamishwa masomo baada ya kukosa sifa ya kuendelea na masomo chuoni hapo. Baada ya wanafunzi kulalamika mara kwa mara kuibiwa mali zao ndipo tulipofanikiwa kumkamata.
Mtuhumiwa huyo baada ya kuhojiwa alikiri kufanya uhalifu wa uvunjaji na wizi wa laptop na simu, alieleza kuwa mpaka anakamatwa na kuhojiwa alikuwa ameshaiba laptop zaidi ya 40 pamoja na simu zaidi ya 80 chuoni hapo.
Kamanda MISIME ameendelea kusema kuwa baada ya ufuatiliaji katika kumbukumbu za Polisi, jumla ya matukio 30 yameripotiwa katika kituo cha Polisi UDOM na jumla ya Laptop zinazokadiriwa kuwa zaidi ya 60 zimeibiwa katika vitivo mbalimbali ndani ya chuo hicho ikiwemo kitivo cha Sayansi ya Jamii na Elimu.
Mtuhumiwa huyo alipohojiwa zaidi alikwenda kuonyesha kwa mtu aliyemuuzia vitu hivyo baada ya kuiba, mtu huyo alibainika kuwa ni ISSACK S/O LEMA Mwenye miaka 29, Mkazi wa Airport ambaye ni fundi wa kutengeneza komputa maeneo ya Mtendeni Street Dodoma pembeni ya jingo la Bima.
Polisi walifika kwa mtu huyo na alipohojiwa alikiri kupokea Laptop zaidi ya 19 kutoka kwa mtuhumiwa ONESMO na imebainika fundi huyu mara baada ya kuletewa laptop na mtuhumiwa anazifungua na kuuza kifaa kimoja kimoja.
Kamanda MISIME ametoa wito kwa wanafunzi wa vyuo mbalimbli kuwa makini na baadhi ya wanafunzi waliosimamishwa na kufukuzwa chuo kwani imebainika ndio wanaoshikiana na wahalifu wengine kuiba vitu mbalimbali katika vyuo, pia wananchi nao wasinunue vitu bila ya kupewa risiti au kuandikishiana kwa mujibu wa sheria ili kujenga uaminifu kwa anayenunua na anayeuza mali la sivyo unaweza kushitakiwa kwa kukutwa au kupokea mali ya wizi.

RAIS WA MSUMBIJI FILIPE JACINTO NYUSSI AWASILI NCHINI KWA ZIARA RASMI YA SIKU TATU

NU1
Rais Kikwete akimpokea Rais Filipe Jacinto Nyusi uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo. Rais huyo anayefanya ziara yake ya kwanza nje ya nchi kama rais wa Msumbiji yuko katika ziara rasmi ya siku tatu.
NU2
Rais Kikwete akimpokea Rais Filipe Jacinto Nyusi uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo. Rais huyo anayefanya ziara yake ya kwanza nje ya nchi kama rais wa Msumbiji yuko katika ziara rasmi ya siku tatu.
NU3
Rais Filipe Jacinto Nyusi akipokea shada la maua baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo. Rais huyo anayefanya ziara yake ya kwanza nje ya nchi kama rais wa Msumbiji yuko katika ziara rasmi ya siku tatu.
NU4
Rais Filipe Jacinto Nyusi akikagua gwaride la heshima baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo. Rais huyo anayefanya ziara yake ya kwanza nje ya nchi kama rais wa Msumbiji yuko katika ziara rasmi ya siku tatu.
NU5
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgteni wake Rais Filipe Jacinto Nyusi wakiangalia ngoma baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo. Rais huyo anayefanya ziara yake ya kwanza nje ya nchi kama rais wa Msumbiji yuko katika ziara rasmi ya siku tatu.
NU6
Rais Filipe Jacinto Nyusi akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Ikulu jijini Dar es salaam katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kwanza nje ya nchi kama rais wa Msumbiji yuko katika ziara rasmi ya siku tatu.
NU7
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Filipe Jacinto Nyusi wakishangiliwa na mamia ya wakazi wa Dar es salaam waliojitokeza kwa wingi kumlaki Rais huyoanayefanya ziara yake ya kwanza nje ya nchi kama rais wa Msumbiji yuko katika ziara rasmi ya siku tatu
NU9
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Filipe Jacinto Nyusi na ujumbe wake katika mazungumzo rasmi Ikulu jijini Dar es salaam leo
NU10
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe na Waziri wa Masuala ya Ndani wa Msumbiji wakitiliana saini mkataba wa makubaliano mbele ye marais Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Filipe Jacinto Nyusi wa Msumbiji.
PICHA NA IKULU

FLAVIANA MATATA AONGOZA MAMIA YA WANAMITINDO WA BONGO KUJIUNGA NA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF

Balozi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Flaviana Matata.
Wanamitindo wakiwa kwenye foleni ya kupiga picha tayari kujipatia vitambulisho baada ya kukamilisha zoezi la kujaza fomu za kujiunga na mpango wa PSS wa Mfuko huo.
Wanamitindo wakijaza fomu za kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari PSS.

ZILIZOSOMWA ZAIDI