NYUMBANI KITAIFA

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BIASHARA

Ulimwengu wa habari.

MATAIFA MENGINE

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BURUDANI

Ulimwengu wa habari.

MAAJABU DUNIANI

Ulimwengu wa habari.

Monday, June 30, 2014

HEE!!! UNAAMBIWA HIZI NI BAADHI YA TABIA WATU WAZIFANYAZO NDANI YA USAFIRI WA UMMA AMBAZO NI KERO KWA WATU WENGINE HUKO MAJUU!!!

KIUKWELI kama wewe ni mdau na mtumiaji mzuri wa usafiri wa Umma maarufu kama Daladala utakubaliana nami kuwa mtu anapoingia katika basi la abiria na kuanza kuongea na simu kwa sauti kubwaaaa, kama vile amepanda gari hilo peke yake, au mtu anakikwapaaa halafu anakuwekea karibu na pua yako, mmmmh yaani inakeera sana!!!
Kumbe hata kwa wenzetu haya mambo yapo??? Duuuh!!!
Juu na chini ni baadhi ya tabia za watu wazifnyazo wanapotukuwa wanatumia usafiri wa umma ambao hua kero kwa watu wengine.

MATOKEO YA UCHAGUZI WA SIMBA: RAIS NA SAFU NZIMA YA UONGOZI YAJULIKANA!!!

Rage
MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hanspoppe jana aliokoa jahazi baada ya kutoa Sh. milioni 20 na kuwezesha kufanyika kwa mkutano mkuu wa uchaguzi wa uliomweka madarakani Evans Aveva.

Hanspoppe alitoa fedha hizo ili kugharamia uchaguzi baada ya kampuni ya bia Tanzania (TBL), ambao ndio wadhamini wa klabu hiyo, walioahidi kugharamia mkutano huo kushindwa kufanya hivyo kwa wakati.

Habari za ndani zilidai kwamba, rais aliyemaliza muda wake, Ismail Aden Rage alitaka uchaguzi usifanyike kutokana na wadhamini kutotoa fedha hizo.

Hata hivyo, uchaguzi huo uliohudhuriwa na wanachama 2,501 ulifanyika kama ilivyotarajiwa huku Aveva akionekana kukosa upinzani kutokana na kuenguliwa na Kamati ya Uchaguzi kwa aliyekuwa mpinzani mkubwa, Michael Wambura.

Mpinzani aliyesalia wa Aveva, Andrew Tupa hana umaarufu wa kutosha katika klabu hiyo na hivyo kumuacha Aveva katika mbio zilizoonekana za “farasi mmoja”.

Nafasi ya makamu rais ilikwenda Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ aliyemshinda Swedi Mkwabi na Jamhuri Kihwelu ‘Julio’.Mkutano wa uchaguzi huo ulifunguliwa kwa dua maalum saa 4:49.

Wambura alikumbana na balaa jingine baada ya kuzuiwa kuingia katika mkutano huo.Wakati huo huo, wakati kocha mkuu wa klabu ya Simba, Zdravko Logarusic, akisema hajui atarejea lini nchini, Kamati ya Usajili iko katika hatua ya mwisho kumnasa mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uganda, Hassan Waswa.

Kwa mujibu wa habari zilizopatikana jijini Dar es Salaam, Simba iko katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa Waswa ili kuongeza nguvu kwenye safu yake ya ushambuliaji.

Chanzo kilisema kuwa leo baada ya uongozi mpya kuingia madarakani utafanya maamuzi ya mwisho ya kuona ni wachezaji wangapi watabaki kuichezea Simba katika msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara itakayoanza kutimua vumbi Agosti 24 mwaka huu.

“Logarusic anatua keshokutwa (leo) na yeye ndiye ataamua lini mazoezi yaanze rasmi…sisi kazi yetu ya kuimarisha timu tumeifanya kikamilifu licha ya kukutana na changamoto iliyohusicha uchaguzi mkuu,” alisema Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hanspoppe Zacharia.

Hata hivyo, Loga alisema jana kuwa hajui atakuja lini nchini kwani bado hajapata taarifa zozote kutoka kwa Hanspoppe, hivyo anasubiri taarifa hizo.

Logarusic ambaye mkataba wake wa awali wa miezi sita ulimalizika Mei 31 mwaka huu anatarajiwa kuendelea kuliongoza benchi la ufundi la Wekundu wa Msimbazi akisaidiwa na nahodha wa zamani wa timu hiyo, Selemani Matola.

Simba ilimaliza msimu uliopita ikiwa katika nafasi ya nne na kukosa tiketi ya kushiriki mashindano ya kimataifa kwa mwaka wa pili mfululizo.

Source: Nipashe

SHABIKI AFARIKI BAADA YA PENALTY KATI YA CHILE NA BRAZIL

chilee
SHABIKI mmoja wa mpira wa miguu aliyekuwa nchini Brazil wakati mechi kati ya Brazil na Chile ikichezwa amefariki dunia baada ya kupata mshtuko wa moyo wakati wa kipindi cha makabiliano ya penalty.
Shabiki huyo alikua akiangalia mpira kwenye moja ya Baa iliyopo ndani ya Mineirao ambapo baada ya Penalty hiyo alianza kulalamika kuwa hajisikii vizuri na kupelekwa hospitali ambako baadae alipoteza maisha.
Kwa mujibu wa Gazeti la Estado de minas shabiki huyo alikua miongoni mwa watu 98 waliokuwa wakipatiwa huduma ya kwanza kutoka kwa wahudumu wa afya waliokuwa ndani ya eneo lililokuwa na takribani watu 60 waliokuwa wakihudumiwa kwenye viti vyao.
chilee2
Mechi hiyo iliishia kwa sare ya bao 1-1 katika muda wa kawaida na kupelekea kuchezwa kwa muda wa ziada ambao haukuzalisha chochote.
Wakati wa matuta timu ya Brazil ilipoteza mara mbili sawa na Chile jambo lililochangia taharuki miongoni mwa Mashabiki wa timu ya nyumbani ya Brazil.
Baadaye aliyekuwa mchezaji wa West Brom Gonzalo Jara wa Chile aligonga mwamba hivyo kuwapa Brazil nafasi ya kuingia robo fainali.
Mwanaume huyo aliyekufa eneo la kuangalia mpira si wa kwanza kwenye mechi ya kombe la dunia ambapo China mtu mmoja alikufa baada ya kukaa macho siku tatu kushuhudia mechi ya ufunguzi kwenye makundi, ambapo shabiki wa Mexico alijirusha na kufa baada ya timu yake kusajili ushindi kwenye mechi ya ufunguzi.

DUUU!!! CHEKI SUAREZ ANAVYOTESWA MITANDAONI #SUAREZING

suarez
BAADA ya kumng’ata mchezaji mwenzake, Luis Suarez amegeuka kuwa mchezaji anayetrend sana au anayezungumziwa sana kupitia mtandao wa Twitter kwa kutumia hashtag ya #Suarezing huku ikiambatana na picha mbalimbali zilizotengenezwa za kumtania mchezaji huyo kwa kitendo alichofanya.

suarez3
Tangu mchezaji huyo wa Uruguay apewe adhabu ya kufungiwa kwa kumng’ata mchezaji wa Italia Giorgio Chiellini amekuwa akimake headlines kila kukicha katika mitandao haswa Twitter.

suarez2
Ilianza kama utani tu kwa watu kutengeneza picha lakini sasa kimegeuka kuwa kitu kikubwa huku wengine wakijipiga picha hata barabarani kuiga kitendo kilichofanywa na Suarez wakati wa moja ya mechi za kombe la dunia.

ISIS YATANGAZA UTAWALA WAO

Mpiganaji wa kundi la ISIS linalodai kutangaza taifa la kiislamu.
NCHINI Iraq hali inaendelea kuzorota, raia wakiendela kukimbia mapigano .
Sasa wapiganaji wa kiislam wa Kundi la iSIS wamesema kuwa wanataka kuweka utawala wao baada ya kudhibiti maeneo ya Iraq na Syria
Msemaji wa wanamgambo hao wa kiislamu wa ISIS ametangaza kuwa wataunganisha ardhi wanazozidhibiti walizoziteka kutoka Iraq na Syria ndio waunde eneo moja wanalolitaja kama 'Islamic Caliphate' litakalotawaliwa na sheria kali za kiislamu.
Kama vile ilivyotolewa taarifa ya Shami ndivyo ilivyotangazwa kauli ya Shaykh Abu Muhammad al-Adnani, kupitia mtandao wa You Tube.
ISIS wameteka maeneo Iraq na Syria. Serikali ya Iraq ina wakati mgumu kukabiliana nao.
Ameendelea kusema eneo hilo litajumuisha tangu Aleppo huko Syria hadi Diyala mashariki mwa Iraq.
Na kufuatia hali hiyo msemaji huyo amefafanua kwamba sasa kundi hilo badala ya kuwa na kujulikana kwa jina la ufupi ISIS na the Levant sasa watajiita tu "the Islamic State" Taifa la kiislam.Kundi hilo pia limesema limemteua kiongozi wao -- Abu Bakr al-Baghdadi -- kama 'Caliph', wakidai ndio kiongozi wa waslamu wote.Haya yote yanatangazwa baada ya kundi hilo la Isis kupata mafanikio makubwa katika vita vivyo.Wakati huo huo Serikali ya Iraqi imesema vikosi vyake vimepiga hatua kuelekea Tikrit, mji wa kazkazini mwa nchi hiyo uliotekwa na wanamgambo hao wa kiislamu zaidi ya wiki mbili zilizopita.
Msemaji wa jeshi la Iraqi Luteni jenerali Qassim al-Moussawi amesema jeshi lao liko katika awamu ya kwanza ya mapigano hayo ya tangu alhamisi.
Televisheni ya kitaifa ilionesha helicopters zikishambulia maeneo kadhaa huko jangwani lakini hamna ushahidi kamili wa kuaminika kwamba wanajeshi wa serikali wamefanikiwa kuingia mjini.Waasi hao wametega mabomu kando kando mwa barabara kuu kujaribu kuzuia vikosi vya serikali.Hata hivyo mwandishi wa BBC aliyeko Baghdad amesema hii ndio hatua ya kwanza thabiti iliyowahi kuchukuliwa na serikali dhidi ya ISIS tangu waasi hao walipoanza kushambulia na kuyateka maeneo ya nchi hiyo kwa kasi iliyowashangaza wengi.

DIAMOND PLATNUMZ ALIVYOFANYA MAKAMUZI CALIFORNIA SIKU YA JUMAMOSI

Kushoto ni Balozi wa Heshima, Mhe. Ahmed Issa akiwasili ukumbini hapo akiongozana na wanajumuiya wa California.
 Diamond Platnumz mwanamuziki wa bongo fleva asieshikika sasa hivi ambaye ni maarufu zaidi kwenye wimbo wake wa my number one aliyemshirikisha mwanamuziki mwingine wa Nigeria anayefanya vizuri sasa hivi Davido akifanya show kali jijini Los Angeles, California siku ya Jumamosi June 28, 2014.
Ambapo Mgeni wa heshima alikua Mhe. Ahmed Issa ambaye ni Balozi wa Heshima wa Tanzania California.
Mashabiki wa Diamond wakipagawa kwenye showa ya Diamond Platnumz iliyofanyika Los Angeles, California nchini Marekani.

 Diamond Platnumza rais wa Wasafi akifanya vitu vyake.
 Diamond Platnumz akiwachengua mashabiki waliohudhuria showa yake ya California.
 Diamond Platnumz akishambulia jukwaa na kuwapagawisha mashabiki wake wa California nchini Marekani.

IYANYA ATUPIA VIDEO TEASER YA WIMBO ALIOSHIRIKISHWA NA DIAMOND - BUM BUM, ICHEKI HAPA!!!

VIDEO Teaser ya wimbo mpya wa Diamond akiwa amemshirikisha Iyanya kutoka Nigeria imeshatoka.
Na kupitia ukurasa wa Iyanya Instagram, alipost video hiyo ambayo imerikodiwa uingereza.
Diamond alifanya collable hiyo na iyanya alivyokuja Bongo na kuimalizia nchini Nigeria alipoenda kwa ajili ya kuzindua wimbo wa kampeni ya kilimo (One Campaign)
Itazama video hiyo hapa chini..!!!

ZILIZOSOMWA ZAIDI