NYUMBANI KITAIFA

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BIASHARA

Ulimwengu wa habari.

MATAIFA MENGINE

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BURUDANI

Ulimwengu wa habari.

MAAJABU DUNIANI

Ulimwengu wa habari.

Friday, December 7, 2012

WANAHABARI WAMJULIA HALI MWANDISHI SHAABAN MATUTU


 Mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima, Shaaban Matutu akiongea na waandishi wa habari na wadau mbalimbali waliofika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam baada ya kutolewa risasi kifuani aliyopigwa na Polisi nyumbani kwake Tegeta.
 Mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima, Shaaban Matutu akisalimiwa na wadau na waandishi mbalimbali waliofika kumjulia hali akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam baada ya kutolewa risasi kifuani aliyopigwa na Polisi nyumbani kwake Tegeta.
Mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima, Shaaban Matutu akionyesha sehemu aliyojeruhiwa na risasi baada ya kujuliwa hali na waandishi wa habari katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam baada ya kutolewa risasi kifuani aliyopigwa na Polisi nyumbani kwake Tegeta.
(Picha zote na Francis Dande)

Kamanda Suleiman Kova akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani)
Ambapo jana tu, kamanda Suleiman Kova amesema kuwa uchunguzi juu ya jambo hili unafanya na jeshi la polisi, na kuwachukulia hatua wote watakao kuwa wamehusika na tukio hili kwa namna moja ama nyingine.

‘’Yeyote Yule ambaye ataonekana kuwa amehusika kwa namna moja ama nyingine atachukuliwa hatua’’ Hayo ni maneno aliyoyasema kamanda Suleiman Kova katika mkutano na waandishi wa habari.

Kwa mujibu wa kamanda Suleiman Kova askari mmoja ameshakamatwa akihusishwa na tukio la mauaji ya marehemu John Paul ambaye inasemekana alijeruhiwa na kitu kinachodaiwa kuwa ni bomu wakati polisi walipokuwa wakiwatawanya wananchi waliokuwa wakipinga kukamatwa magari yaliyopaki sehemu isiyoruhusiwa eneo la Tegeta kwa ndevu jijini Dar es salaam wiki iliyopita.

MNYIKA ASHINDA KESI YA UBUNGE - UBUNGO

Mhe. John Mnyika ambaye kwa sasa tangu kutangazwa kwa shauri hilo, ni mbunge halali wa jimbo la Ubungo mara tu baada ya kutoka makamani hapo, na kuongea na wananchi kupitia vyombo vya habari, huku wanaomzunguka wakiwa ni wafuasi wa chama hicho.

(Habari na Picha kwa hisani ya mlimanimedia.blogspot.com)

Na Amini Mgheni

MAHAKAMA ya rufaa imetupilia mbali rufani dhidi ya ubunge wa jimbo la ubungo, ambapo awali waliofungua kesi hiyo alieyekuwa mgombea kupitia chama cha mapinduzi, waliwasilisha dhamira yao mbele ya mahakama hiyo ya kutaka kufutwa kwa kesi hiyo kulingana na ridhaa yao wenyewe.

Kama mwandishi wa mtandao huu napata fursa ya kukutana na Mhe. John Mnyika baada ya shauri la kesi hiyo kumalizika naye akaeleza jinsi kesi hiyo ilivyomalizika.

‘‘Masuala ya kesi dhidi ya ubunge wetu, na kura zetu tulizopiga leo ndo yaamefikia hatma, kwahiyo hakuna tena kupingwa kwa namna yeyote ile, jambo hili limemalizika na sasa tunaweza kuendelea na kazi bila kuwa na kesi au mashauri yeyote mahakamani’’ alisema Mhe. John Mnyika

Mhe. John Mnyika akiongea na wananchi waliofika mahakamani hapo kusikiliza shauri hilo.
Kwa muda mrfu mbunge wa jimbo la ubungo amekuwa akiendelea kufanya kazi licha ya mapingamizi kadha wa kadha ambayo yote ameshinda.

Lakini pia kama mwandishi wa mtandao huu wa mlimanimedia.blogspot.com nikataka kujua endapo kesi hii imeondolewa katika ngazi ya rufaa, je watadai fidia kama kesi nyingine wanavyofanya? Mnyika akawa na haya ya kuzungumza;

‘‘Tukubali kwamba kama wametoa kesi katika ngazi ya rufaa basi nasisi tusamehe’’ alisema Mnyika.


Baadhi ya wakereketwa wa CHADEMA wakishangilia baada ya Mhe. John Mnyika kushinda kesi hiyo.
Kufutwa kwa kesi hiyo kunafanya ubunge wa jimbo la ubungo kutokuwa na shaka yeyote, ambapo mpaka hivi sasa hakuna kesi yeyote mahakamani, jambo linalotoa fursa kwa mbunge huyo kutekeleza majukumu yake mengine ya kitaifa kama alivyowaahidi wananchi wa jimbo la ubungo.

UZINDUZI KITABU CHA SHERIA ZA ARDHI



WITO umetolewa kwa wadau wa sheria kujitokeza na kuandika vitabu vitakavyowawezesha wananchi kuzifahamu sheria mbalimbali za ardhi ikiwa ni kuhakikisha wananchi wanakuwa na uelewa mpana juu ya umuliki wa ardhi yao.

Wito huo umetolewa na Prof. Anna Tibaijuka katika uzinduzi wa kitabu kinachozama kwa kina kuhusu sheria ya ardhi, Abdon Rwegasira kiitwacho ''LAND as a human right''
Waziri wa Ardhi, nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka akiwahutubiwa wanazuoni na baadhi ya wanafunzi wa vyuo mbalimbali waliojitokeza katika uzinduzi wa kitabu hicho.


Kubwa lililoongelewa katika uzinduzi huo na Prof. Anna Tibaijuka ni kuwa wadau wajitokeze kwa wingi kwani watanzania wengi wangependa kupata jumbe nyingi zilizo katika vitabu mbalimbali vinavyoelezea sheria ya Ardhi hasa ya Tanzania, lakini kwasababu vingi vimeandikwa kwa lugha isiyo ya kiswahili hivyo inakuwa ni changamoto kwao, lakini kutona na ujuio wa kitabu hicho, kitawapa wengi hamu ya kukisoma kwasababu kipo katika lugha wanayoielewa, licha ya kuwa lugha ya kiingereza bado ni changamoto.
Waziri wa Ardhi, nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka akisaidiwa na Prof. Rwekaza Mukandala (kushoto kwake) na Abdon Rwegasira kusoto (kulia kwake) kukata utepe, ili kukifungua rasmi kitabu hicho kilichoandaliwa na Abdon Rwegasira kinachozungumzia masuala ya Ardhi nchini Tanzania.

Kitabu hicho kilichoandaliwa kwa kipindi cha miaka mitatu, kimechapishwa na kusambazwa na mchapishaji mahiri nchini, Kampuni ya Mkuki na Nyota.

MASHINDANO YA UHURU MARATHON YAZINDULIWA DAR


Mgeni Rasmi katika Hafla ya Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon), Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenela Mukangara akikata utepe kuashiria kuwa tayari mashindano ya Uhuru Marathon yamezinduliwa rasmi.
WADAU wa michezo wametakiwa kujitokeza na kuanzisha mashindano ya michezo mbalimbali kwa lengo la kuongeza fursa za ajira na kuitangaza Tanzania Kimataifa.

Akizindua  mashindano ya Riadha  ya Uhuru Marathoni Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na michezo Dakta Fenella Mkangara amesema kuwa mashindano ni muhimu yakawa endelevu kwa mustakabali wa kuenzi Uhuru wa taifa hili.
Dkt. Fenela Mukangara amesema mbali na kuenzi uhuru wa Tanzania mashindano hayo yatatoa fursa kwa vijana kujipatia ajira kwa kushiriki katika michuano ya Uhuru Marathoni ambayo itafanyika Desemba 8 kila mwaka ambapo kwa kuanzia itafanyika hapo mwakani.
''Tunaka kuona mpango huu unawanufaisha wanariadha na kuwa nafasi ya ajira kwao kwa kuwaingizia kipato, na sisi kama wananchi, wadau tunaopenda michezo tuhakikishe tunawaunga mikono'' Alisema Dkt. Fenela Mukangara.
UHURU WETU, AMANI YETU, UMOJA WETU. Ni kauli mbiu inayoyaongoza mashindano hayo ambapo yataanza hapo mwakani.
Waziri Mukangara pia amesema ni vyema michuano hiyo ikawa endelevu kwa minajili ya kuenzi malengo yake ambayo mafanikio ya Uhuru ikiwemo amani, umoja na mshikamano wa Tanzania tulionao hadi leo.
Mgeni Rasmi katika Hafla ya Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon), Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenela Mukangara akisoma hotuba yake aliyoiandaa wakati wa Uzinduzi wa Uhuru Marathon.
Naye Mkurugenzi wa Intellectual Communications Innocent Melleck amesema michuano hiyo itaweza kuitangaza Tanzania katika utalii kwa kutumia Tovuti rasmi iliyozinduliwa na wanamichezo kutoka nje ya nchi watakaoshiriki katika michuano hiyo.
Mkurugenzi wa Intellectual Communications Bw. Innocent Melleck akieleza nia na madhumuni ya kampuni yake kuanzisha mashindayo hayo ya Uhuru Marathon.

Uzinduzi huo ulisindikizwa na burudani mbali mbali, akiwemo mrisho mpoto ambaye aliwavutia wengi kwa tungo zake mahiri.

FIFTH GAV PARTNER'S FORUM MEETING WAZINDULIWA



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akihutubia wadau kutoka nchi mbalimbali, waliohudhulia mkutano huo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete amefungua mkutano wa kimataifa wa chanjo duniani GAVI. Mkutano ulizikutanisha nchi za Afrika 73.

Huku Tanzania ikipomgezwa kwa mafanikio makubwa ya utoaji wa huduma za chanjo kwa watoto na mama wajawazito licha ya changamoto zinazowakabili kinamama wajawazito na watoto.

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pia amewaahidi wadau waliokuwepo katika mkutano huo kuwa Tanzania itaendelea kujikita katika kukabiliana na changamoto zinazowakumba wanawake wajawazito na watoto wadogo, ili kupunguza tatizo hilo.

‘’Tunajitahidi kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto wadogo kwa kuongeza utoaji wa chanjo’’ Alisema Mhe. Jakaya Kikwete.
Kwa kuongea hayo Mhe. Rais Kikwete akafungua rasmi mkutano huo wa tano unatambulika kama Fifth Gavi Partner’s forum meeting. Huku akiwatakia mafanikio mema katika harakati na shughuli zao.

Wednesday, December 5, 2012

VIDEO MPYA YA DULLY NA DIAMOND

A/MASHARIKI: WAKENYA WAONYWA JUU YA WASHUKIWA WA MAHAKAMA YA UHALIFU

Aliyekuwa katibu wa Umoja wa mataifa, Kofi Annan, amewaonya wakenya kuhusu hatari ya kuwachagua wagombea uarais ambao wanakabiliwa na kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita iliyopo the Hague.

Akizungumza mjini Nairobi, Annan amesema kumchagua Uhuru Kenyatta na William Ruto katika uchaguzi wa mwakani utatatiza uhusiano wa Kenya na ulimwengu mzima.

Mwandishi wa BBC mjini Nairobi anasema huenda wagombea hao wakajibu onyo alilotoa Annan kwa hasira.
Ingawa hakuwataja kwa majina, naibu waziri mkuu Uhuru Kenyatta na William Ruto, bwana Annan aliambia BBC kuwa kiongozi yeyote anapaswa kuwa na uwezo wa kusafiri na kukutana na viongozi wengine wa kimataifa.

"wakati unapomchagua kiongozi ambaye hawezi kufanya hivyo, ambaye hatakuwa huru kufanya hivyo au kupokelewa , sio kwa manufaa ya nchi na nadhani watu wote wataweza kuelewa hilo,'' alisema Annan.
Wanasiasa hao wawili wanatakikana katika mahakama ya ICC kuhusiana na jghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007
 
Uhuru Kenyatta na William Ruto wanatakikana na mahakama ya ICC kuhusiana na ghasia za mwaka 2007
Duru zinasema kuwa serikali nyingi hazipendi kujihusisha moja kwa moja na wanasiasa ambao ni washukiwa wa uhalifu na ambao wanatakikana katika mahakama ya ICC.

Anasema kuwa matamshi ya Annan huenda yakawaghadhabisha sana Ruto na Uhuru lakini haijulikani ni kwa kiasi gani yataweza kuwashawishi wapiga kura kutowapigia kura wawili hao.

Ingawa Koffi Annan anaheshimiwa sana, wakenya wengi bado wana mazoea ya kupiga kura kwa misingi ya kikabila.

ZILIZOSOMWA ZAIDI