NYUMBANI KITAIFA

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BIASHARA

Ulimwengu wa habari.

MATAIFA MENGINE

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BURUDANI

Ulimwengu wa habari.

MAAJABU DUNIANI

Ulimwengu wa habari.

Saturday, August 1, 2015

BAADA YA KIMYA KIREFU BABY J KUIBUKA TENA

Mwadada anayefanya vizuri katika tasnia ya muziki Tanzania akiwakilisha visiwa vya Zanzibar Baby J amesema baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu sasa mashabiki wake wakae tayari kwa ujio mpya.
Baby J ambaye muda mwingi yupo maskani yake Zanzibar amesema sababu ya kukaa zaidi ya mwaka bila kuachia ngoma mpaka watu wanadhani ameacha muziki ni matatizo binafsi ambayo yamekwishakaa sawa na sasa anarudi mzigoni.
Lakini Baby J hakutaka kuweka wazi jina la Project anayokuja nayo na kusema sasa yupo chini ya usimamizi ambao unamuongoza kwa hiyo soon mambo yatakua hadharani so funs wake wawe tayari kumpokea.

KASSIM MGANGA: 'NITAMSAIDIA Q CHILA'

Staa wa muziki wa miondokop ya Bongofleva nchini Kassim Mganga amesema kuwa pamoja na maneno ambayo yamekuwa yakimlenga msanii Q Chila kuhusu kiwango chake kuwa si ndivyo, yeye binafsi ataendelea kumsaidia katika muziki.Kassim amesema kuwa huwezi kumzuia mtu kuzungumza kutokana na ukweli kwamba kila mtu anazungumza maneno ambayo hujui yupo katika hali gani, akiweka wazi kuwa Q Chilla ni ndugu yake na atazidi kumpa sapoti katika muziki wake.

WASICHANA WANAPENDA MAGARI KULIKO UNAVYOFIKIRI, TAZAMA HII VIDEO USTAAJABU


WEMA SEPETU AMJIBU DAIMOND PLATINUMZ KWA KUMWAMBIA HIVIII…..!!!! SOMA HAPA.

Wema Sepetu baada ya kushindwa kura za maoni na kuambulia kura 90 dhidi ya wapinzani wake. 
Wema Sepetu aliwasili tokea Dodoma na kupokelewa na umati mkubwa watu na msafara hadi nyumbani kwao Sinza.
Baada ya kufika aliweza kutoa shukrani zake na maneno yake ya hekima.
Kilichokuja kuibuka ni kwamba ilikuwa kama anarusha dongo kwa timu pinzani yani Team Zari na Team Daimond.
”Wanasema watanyoka watanyooka wao, sasa naomba niulize tumewanyoosha au mwanetunyoosha?

BREAKING NEWS… ESTER BULAYA APETA KURA UBUNGE NA CHADEMA KUPITIA KURA ZA MAONI..!


ESTER BULAYA  Ameingia Tatu Bora ...KATIKA WILAYA YA BUNDA NA KUWA MTU WA TATU
MATOKEO YA BUNDA MJINI
PIUS KURA 61
MAGEMBE KURA 40
BULAYA KURA 37
FRANK KURA 35
MAGANJA KURA 5
JANE KURA 0
CHACHA KURA 0
Katika Ukurasa Wake wa Facebook Ameandika Hivi:

CHADEMA tunaendelea tulianza na mungu tunamaliza na mungu, nawashukuru sana wanachadema Bunda kwa kunipokea na kunipa heshima kubwa, mbali ya ugeni wangu ndani ya chama mmeonyesha mnaniamini. mmenipendekeza kwenye majina matatu ili kusubiri uteuzi wa vikao vya kamati kuu vitakavyoamua nani apeperushe bendera katika jimbo la Bunda. Lakini pia mkanipendekeza kuwa namba moja kwenye viti maalum kwa kura nyingi. Nawaahidi sitowaangusha, yeyote atakae pita kati yetu tutashinda Bunda Mjini. Mungu ibariki Chadema ibariki Tanzania.

FAIZA ALLY AWACHANA WANAODHANI AMEPOKONYWA MTOTO NA MBUNGE WA MBEYA MHESHIMIWA SUGU

Haya ndiyo aliyoandika mwanadada huyu katika mtandao wa kijamii…TAHADHALI inatolewa katika lugha endapo itakuudhi kwani ni nukuu ya moja kwa moja ya Faidha na mtandao huu haujaongeza neno lolote.
������ mtoto ninae na hatoki manina zenu- na vivazi ndio hivyo �������� nimecheka sana kuna bwege na mabwege wenzie wanajua mwanangu alichukuliwa eti wanafurahia hahahahaaa mtasubiri na madira sivai������- mwanangu hajachukuliwa n'go na hatachuliwa kamwe!!!!!! Na vimino siachi ndio kwanza usichana unaanza nyie mnao nione mzee mna malienge �������� aka makengeza !!!! Oh yeah mimi mzuri kudadeki!!!!! Kama huamini jiangalie halafu ujifananishe ������ na mie ��

EXCLUSIVE: KURA ZA MAONI NDANI YA CCM UBUNGE NA UDIWANI WAPAMBA MOTO NCHINI KOTE

WANACDBaadhi ya Wana CCM wakiwa katika moja ya mikutaano yao wakati wa kujitambulisha kwa wagombea Ubunge na Udiwani walipotembelea na kujinadi kwao hivi karibuni. Pichani ni wana CCM wa Kata ya Magomeni kama wanavyoonekana hivi karibuni (Picha na Maktba ya modewjiblog).
Na Andrew Chale, modewjiblog
Kura za maoni ndani ya Chama cha Mapinduzi  (CCM) zimeendelea kupamba moto kwa sehemu mbalimbali wana CCM kujitokeza kupiga kura kuchagua kiongozi wao atakaye wafaa ndani ya CCM ambaye  baadae atasimamishwa kuwania kiti hicho katika uchaguzi wa hapo mwezi Oktoba mwaka huu.
Wana CCM  wote wenye kadi kihalali ndio wenye fursa ya kupiga kurfa hizo za maoni  tayari wameanza mchakato huo mapema asubuhi zoezi linaloendelea hadi hivi sasa  na baadae maatokeo yataanza kutaangazwa/ kutolewa kwa kila eneo husika na kisha kutangazwa huku yale ya Udiwani yakitarajiwa kutangazwa katika ofisi za CCM Kata na Ubunge kutangazwa Ofisi za CCM Wilaya.
Awali wagombea hao walipita kila eneo na kujinadi ndani ya wana CCM kwa lengo la kujitambulishwa na kunadi sera zao ilikupata fursa ya kuchaguliwa/kupitishwa huku tukishuhudia mambo mbalimbali kutoka kwa watangaza nia hao. Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na tukio la aliyekuwa Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai kumpiga mtu katika uchaguzi na kumsababishia maumivu makali hadi kupoteza fahamu.
Mbali na hilo la Job Ndugai,  pia baadhi ya taarifa zinaeleza kuwa wapo baadhi ya wagombea Ubunge na Udiwani wakishutumiwa kutoa rushwa kwa wana CCM huku wengine wakikanusha kwa hilo.
Modewjiblog ipo katika mitaa mbalimbali kuanzia asubuhi hii ikikusanyia  matukio ya uchaguzi huu wa kura za maoni ndani ya CCM,  na kisha tutawaletea hapa hapa moja kwa moja ilikujua nani kapenya na nani amebaki….
#Mo Blog

ZILIZOSOMWA ZAIDI