NYUMBANI KITAIFA

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BIASHARA

Ulimwengu wa habari.

MATAIFA MENGINE

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BURUDANI

Ulimwengu wa habari.

MAAJABU DUNIANI

Ulimwengu wa habari.

Sunday, June 14, 2015

MAPENZI YANA NGUVU: MR BLUE AMSHUKURU MKEWE ‘WAHYDA’ KWA KUMSAIDIA KUACHA KUTUMIA BANGI, SIGARA, MIRUNGI NA POMBE *PICHA*

Mr Blue byser ameamua kuweka wazi ni jinsi gani mke wake amemsaidi katika kuacha kutumia vilevi vya aina yoyote, na ashukuriwe mke wake kwa kuwezesha hilo.
Blue kupitia Instagram yake, hit maker huyo wa ‘Pesa’ amekiri kuwa sasa ana furaha zaidi baada ya kufanikiwa kuacha kuvuta bangi, sigara (fegi) mirungi na pombe. Amemshukuru mama mtoto wake aitwaye Wahyda kwa kumuwezesha kuacha kutumia vilevi hivyo.

http://i1.wp.com/www.bongo61.com/wp-content/uploads/2015/06/Mr-blue.jpg

Hiki ndicho alichokiandika Blue:
“Alhamdulilahi ..nimeamka salama nikiwa mwenye furaha ahsante mungu ..na nashukuru pia kwa kufaulu mtihani ahsante mke wangu@wahyda_bysers_heart kwa kunifanikisha kuacha vilevi vyote..(bangi, fegi, mirungi, pombe) na kuishi km binadamu wa kawaida..nawashauri ndugu zangu kuwa makini na marafiki wengine wapo kwa ajili ya kukuharibia maisha yako ..kuwa  makini

HII NI KOLABO NYINGINE YA AFRIKA MASHARIKI CHEGE, FEZA KESSY, WAHU NA MGENGE NONINI?

Wahu, Chege na Feza Kessy
Unaikumbuka hii Mkono mmoja weka juu temba,chege ft wahu huenda hii ikawa collabo nyingine kubwa ya Afrika Mashariki inakuja.

Mkata Mkaa mwenye roho mbaya, Chege Chigunda aka Mtoto wa Mama Said, yupo Nairobi, Kenya alikoenda kufanya wimbo na Nonini. Lakini kwa mujibu wa picha tunazoziona kwenye Instagram, huenda collabo hiyo ikawajumuisha pia Feza Kessy na Wahu.

Wahu, Nonini na Feza Kessy
“Honored to meet @wahukagwi na @noninimgengetrue grew up looking up to these artists among others yaaaani im on cloud 9 right now. #StudioFlow #TGIF #BlessingOnBlessing,” ameandika Feza kwenye picha aliyoiweka Instagram.
Naye Wahu amepost picha na kuandika, 
 “About yesterday….hanging out with these wonderful peeps @noninimgengetrue @fezakessy huku picha nyingine kuandika, “Great seeing my boy @chegechigunda after such a long time.”

ISIKILIZE NA UIPAKUE TRACK YA BOW WOW - ALL I KNOW *AUDIO*

ANGALIA NA UIPAKUE VIDEO MPYA YA YAMOTO BAND - NISAMBAZIE RAHA

SKENDO ZA UCHAGUZI: *PICHA* YA UTUPU YA MGOMBEA WA URAIS YAIBULIWA

Mwandishi wetu
NIkama kumekucha! Tayari mbinu za kuchafuana na kupakana matope miongoni mwa wanasiasa waliojitokeza kugombea urais kupitia chama kimoja cha siasa zimeanza kujitokeza baada ya hivi karibuni kuibuliwa kwa picha ya mgombea mmoja wa chama hicho aliyetangaza nia akiwa na hawara ndani ya chumba cha hoteli.
Kuibuliwa kwa picha hiyo kumekuja siku chache kufuatia mgombea huyo kutangaza nia huku akianika kipaumbele chake endapo atapata ridhaa ya wapiga kura kuingia ikulu.
MUDA WA PICHA
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichotinga katika Ofisi za Global Piblishers, Bamaga-Mwenge, inadaiwa kuwa, mheshimiwa huyo (jina tunalo) na mwanamke huyo ambaye si mke wake, walipiga picha hiyo muda mrefu lakini kutokana na duru za kisiasa za uchaguzi mkuu mwaka huu, picha hiyo inaonekana kuwa ‘keki’ kwa wapinzani wake.
“Unajua hii picha ni ya muda mrefu. Mheshimiwa alipiga akiwa na uhusiano na huyu mrembo. Sasa mheshimiwa alipotangaza nia tu, wabaya wake wakaona hapa ndiyo penyewe, wakaiibua ili itumike kwenye kampeni yake ya urais kama chama chake kitampitisha yeye kugombea,” kilisema chanzo hicho.
ENEO LA PICHA
Ilizidi kudaiwa kuwa, picha hiyo ilipigwa ndani ya hoteli moja maarufu iliyopo Mwananyamala jijini Dar es Salaam na mpigaji alikuwa mwanamke huyo ambaye hakujulikana jina akitumia simu yake ya mkononi kwa kuishika kwa mkono wake wa kulia (selfie).
SI MKE WAKE
Chanzo kilisema kwa sababu mheshimiwa huyo wa kutoka Kanda ya Ziwa ana mke na watoto na anaheshimika katika jamii, kupiga picha ya namna hiyo kunamuondolea sifa ya kuwa rais wa Tanzania.
“Ingekuwa picha yenyewe ni mheshimiwa na mke wake, sidhani kama wabaya wangeitumia lakini sasa si unajua maadili ya Kiafrika. Nadhani hata wenzetu nje, huwezi kuwa na mke halafu ukawa na hawara wakakupa cheo kikubwa kama cha urais wa nchi,” kilisema chanzo hicho.
HALI ILIVYO KWA SASA
Tayari baadhi ya wagombea wa urais kupitia vyama mbalimbali wameanza kuwalilia baadhi ya wenzao kwamba, wameanza kucheza rafu katika safari ya kinyang’anyiro cha kuusaka urais kwa kuwatafutia skendo chafu, za zamani na mpya ili wachafuke katika jamii na kuonekana hawafai kukabidhiwa ikulu, Oktoba mwaka huu.
ORODHA YA WAGOMBEA
Mpaka sasa, mbali na Chama Cha Cuf ambapo wameshamtaja Profesa Ibrahim Lipumba kugombea urais mwaka huu,  wanachama wenye nguvu walioonesha nia ya kugombea nafasi hiyo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni Edward Lowassa, Benard Membe, Frederick Sumaye, Samuel Sitta, Makongoro Nyerere, Mwigulu Mchemba, Lazaro Nyalandu, January Makamba ambapo baadhi yao picha zao zimetumika ukurasa wa mbele wa gazeti hili.
#GP

LICHA YA KUJIFUNGUA UZURI WA AUNT PALEPALE!!!! *PICHAZ*

KIWANGO! Tofauti na watu wengine ambao maumbile yao hubadilika mara baada ya kujifungua, kwa staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel hali imekuwa tofauti, uzuri na umbo lake limebaki vilevile.
Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel akiwa na mwanaye.
Akizungumza na wahariri sambamba na waandishi wa Global Publishers nyumbani kwake Mwananyamala jijini Dar, Aunt alisema kilichomfanya asinenepe kupita kiasi na kuharibika mwili ni mazoezi sambamba na kufuata ushauri wa vyakula anaopewa hivyo mwili wake kubaki vilevile.
“Nachukia ubonge nyanya, namshukuru Mungu pia kwani wengi wakijifungua huwa wananenepa hovyo lakini kwangu mambo yamekuwa tofauti. Niko vilevile, nafikiri pia ni kutokana na kufuata ushauri mzuri wa kula chakula niliopewa,” alisema Aunt.
Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel.
Mbali na kutobadilika, Aunt alisema kwa sasa muda mwingi anautumia kuwa nyumbani na ubavu wake, Moze Iyobo wakimlea mtoto wao tofauti na zamani alipokuwa na misele ya usiku katika viwanja tofauti vya starehe.

MASIKINI..!! ROSE MUHANDO AMWAGA MACHOZI HADHARANI, KISA KIZIMA KIPO HAPA!!!

Mwimbaji Injili Bongo, Rose Muhando.
*********** 
ROSE Muhando, aliye mwimbaji Injili Bongo, amejikuta akimwaga machozi yaliyojaa uchungu huku akitumia kama dakika 45 kuelezea wazi mateso na manyanyaso ambayo anayapitia kwa sasa ikiwemo kuhusishwa na tuhuma za utapeli na ‘kubwia unga’, Risasi Jumamosi linakupa stori kamili!


ILIKUAJE?
Mwandishi wetu alimtafuta mwimbaji huyo juzi kwa njia ya simu kutoka mkoani Dodoma yaliko makazi yake lengo likiwa kujua maendeleo yake kikazi ndipo kukaibuka mapya mengi.Rose alianza kuporomosha lawama dhidi ya watu wanaomzushia mambo yasiyo ya kweli juu yake:

MSIKIE MWENYEWE
“Aah, mimi nipo tu (Dodoma) nimekaa kimya kwa sababu si mtu wa majibizano na malumbano, nimepakwa uchafu wa kila aina na kutukanwa huku wanaonitukana ni Wakristo wenzangu na mbaya zaidi hadi wachungaji wananisakama kwa maneno makali, nikaona kukaa kimya ni hekima.”

TUENDELEE
Rose alisema, alichukua uamuzi wa kuachana na dini yake ya zamani (Uislamu) na kujiunga na Ukristo kutokana na kuguswa na mafundisho yake baada ya kuhubiriwa upendo wa kweli lakini kwa sasa anakutana na maumivu na kusalitiwa huku wakisahau mema anayofanya kwa kutangaza Injili.

HUYU HAPA TENA!
“Wakristo wamenifundisha ugaidi na ukatili, ndugu zangu ni Waislamu, kila siku hawaachi kunisuta kutokana na matusi ninayotukanwa na Wakristo wenzangu, nakuwa sina cha kusema, kubisha nashindwa, kumkufuru Mungu nashindwa, nabaki kuugua moyoni kwa kiwango kisichotamkika.”

MATUSI YANAHUSU NINI HASA?
“Unakuta mtu amekualika kwenye tamasha. Kwa bahati mbaya ama kwa kusahau ratiba au kuingiliana majukumu, unaposhindwa kufika, inasambazwa kuwa umetapeli. Unapelekwa polisi wakati mwingine nakuwa nimewasiliana na mhusika juu ya kutofika, namuuliza nimrudishie pesa yake au kama ataandaa tamasha jingine nihudhurie, unashangaa maneno ya utapeli yanaibuka,” alisema Rose.

KILIO CHAANZA!
Rose alishindwa kuhimili kiwango cha maumivu ya moyo na kujikuta akiangua kilio hali iliyomlazimu mwandishi kupata wakati mgumu kumtuliza.

“Oke, nikatukanwa kuwa natumia unga. Ngoja nikuulize. Ingekuwa natumia unga, hivi kweli ningeweza kutunga nyimbo, kuimba na kujituma kwa namna hiyo? Nakuuliza, ninge.... (kilio kikubwa).

AKAENDELEA
“Niliowaamini ndiyo wamenigeuka, wamenitumia kwa muda mrefu na wakati mwingine kwa kunifanyisha kazi ambazo sikuwa nazitaka lakini wameona haitoshi, ni haohao waliniteka na kunipeleka porini na kunitishia maisha. Mungu atajibu na mbingu zitasimama (safari hii kwa kilio cha juu zaidi).”


ENDELEA NAYE
“Wengine wamekuwa wakinitaka kimapenzi (akataja jina), lakini kwa kutumia pesa zao nikikataa wananitishia maisha, wana wake na watoto, nabaki najiuliza kwani mimi ni kafara ya waume za watu? Eeh? Kweli jamani? Nimepelekwa porini, nikapigwa, nikaoneshwa mambo ya ajabu kweli, ili nitoe penzi kwa nguvu, yote hayo nasingiziwa makubwa na kunenewa mabaya, nina moyo wenye nyama, naumia.


“Nimewakosea nini walimwengu? Tatizo ni kuimba? Hivi hawa Wakristo hawaoni kwamba nimekuwa biashara yao nzuri kwa kuimba nyimbo nyingi zinazopendwa na wengi? Hawalioni hata hilo? Nitende wema gani wa kupitiliza hapa?”

YOTE TISA, KUMI HII HAPA!
“Wameninyang’anya vitu vyangu vingi ikiwemo vya ndani, viwanja, na wote ni waume za watu walionitongoza na kuwakataa, wengine nilifanya nao kazi kwa ukaribu, mfano... (akataja jina) na wametumia nafasi hiyo kunipokonya vitu hivyo na wanajua kwa undani uhalali na umiliki wake. Hii ni haki kweli?

“Watu wanaposikia tu Rose Muhando tapeli sasa waelewe napitia mateso magumu yanayoumiza mno, wasisikie tu naimba hivi na kudhani nina furaha ya maisha, nateseka nafsini! (kilio cha kwikwi).

AWEKA NUKTA
Katika kumalizia mazungumzo na mwandishi wetu, Rose alisema: “Waniache na safari yangu ya kumtumikia Mungu, ninachojua yeye (Mungu) atashughulika na watesi wangu na kila nafsi itayaonja mauti.”

Risasi Jumamosi linafanya juhudi za makusudi kuwasaka watu waliotajwa kwenye sauti ya Rose ili kuwasomea madai yake. 
#GPL

ZILIZOSOMWA ZAIDI