NYUMBANI KITAIFA

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BIASHARA

Ulimwengu wa habari.

MATAIFA MENGINE

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BURUDANI

Ulimwengu wa habari.

MAAJABU DUNIANI

Ulimwengu wa habari.

Tuesday, March 3, 2015

VGMA YAMPAMBANISHA DIAMOND PLATNUMZ NA VICHWA HIVI HATARI *PICHAZ*

DIAMOND Platnumz ametajwa kwenye orodha wa wasanii wanao wania tuzo za 16 za Vodafone Ghana Music Awards. VGMA 2015.
Diamond ametajwa kuwania tuzo hizo kwenye kipengele cha msanii bora wa Africa - Africa Artist of the Year na anagombania tuzo hio na wasanii Tiwa Savage wa Nigeria, AKA wa Africa Kusini, Don Jazzy na kundi la the Mavin Group, Patoranking wa Nigeria na Yemi Alade wa Nigeria

Vigezo vya kushinda ni lazima mshindi apatikane kwa kupigiwa kura na raia ambazo zinachukua asilimia 40, Kura za Academy ni asilimia 30 na asilimia 30 ni za Board yao.
Wafahamu kwa picha hapa:

Tiwa Savage toka Nigeria.
AKA toka Africa Kusini.
Don Jazzy na Mavins toka Nigeria.
Patoranking toka Nigeria.
Yemi Alade toka Nigeria.

LUDACRIS NA MKEWE WANATEGEMEA MTOTO *PICHAZ*

LUDACRIS na mke wake Eudoxie Mbouguiengue wametangaza rasmi kuwa wanategemea mtoto baada ya miezi miwili kwenye ndoa.
Picha walioshare na mashabiki inamuonyesha Luda akibusu tumbo la mke wake Eudoxie huku ujumbe ukisema; “Beautiful day on the beach,’Beautiful day indeed“
Mwezi uliopita Luda alipewa haki zote za malezi za mtoto wake wa mwaka mmoja “Cai Bella” after a court battle with the child’s mother, baada ya kushinda kesi dhidi ya mama yake Tamika Fuller.
Album ya tisa ya Ludacris  “Ludaversal” imetajwa kutoka March 31 na Fast 7 itatoka April 3

ICHEKI TATTOO MPYA KWENYE MIKONO YA KANYE WEST NA MAANA YAKE

RAPPA Kanye West amechorwa tattoo mpya kwenye mikono yake miwili, Tattoo hizo amechorwa Ijumaa Feb. 27 akiwa mjini London na mke wake Kim Kardashian.
Kanye amechorwa siku za kuzaliwa za marehemu mama yake Donda na mtoto wake  North West.

Tattoo zimechorwa kuwa lugha ya kirumi , tunaona tarehe June 15, 2013 birthday ya North na July 12, 1949 birthday ya marehemu mama yake Donda aliyefariki mwka 2007.

DANIEL GIBSON ATHIBITISHA UKARIBU WAKE NA KEYSHIA COLE *PICHAZ*

BAADA ya usaliti wake kwa mke wake ‘Daniel Bobby Gibson’ ameweka wazi kuwa bado anamtaka mke wake ambaye ni Keyshia Cole.
Bobby amesema “atakama tumepitia mambo mengi pamoja na nimemuangusha mara kwa mara, bado Keyshia ni rafiki yangu ”.
Bobby pia amekanusha uhusiano ulioripotiwa mwaka jana kati ya Keyshia Cole na boss wa Cash Money Birdman.

MAJANGA: MUME WA MTU AMCHOMA KISU HAWARA, NAYE AJICHOMA HADI UTUMBO WAMWAGIKA

Habari zilizolitikisa Jiji la Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita ni pamoja na ile ya mkazi wa Chamazi, Hussein Mfaume, kumchoma visu hawara yake,  Ester Thomas Ungele (30), naye kujichoma mpaka kujitoa utumbo, Uwazi limeichimba kwa kina.
Hawara akipelekwa hospitali baada ya kuchomwa kisi.
Habari zilidai kuwa, kisa hasa cha mwanaume huyo kujichukulia uamuzi huo wa kikatili ni madai ya  mwanamke huyo  kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine anayedaiwa kuwa ni dereva wa teksi.

MANENO YA SHUHUDA MKUU
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio  hilo ambaye ni mtoto wa Ester, Sarah siku hiyo, yeye na mama yake  walikuwa kwenye eneo lao la biashara ya Mama Lishe, nje ya  Ukumbi wa Vijana, Amana uliopo Ilala, Dar.
“Ghafla nilimwona Hussein akija huku usoni akionekana mtu mwenye hasira. Alimfuata mama alipokuwa na kumuuliza ni kwa nini anamfanyia dharau?”
Mume akiwa taabani baada ya kujichoma kisu.

MALUMBANO YAANZA, WAKIMBIZANA
Sarah anaendelea: “Niliona kama malumbano ya kawaida nikawa nawaangalia lakini nikashangaa kumuona Hussein akimsogelea mama na kutoa kisu.“Mama alianza kukimbia naye Hussein akamkimbiza huku bado ameshika kisu mkononi. Niliogopa sana, nikatetemeka. Nilipiga mayowe kumuombea msaada mama.
“Mama alikimbia uelekeo wa kuingia kwenye Ukumbi wa Vijana lakini kabla hajafika, Hussein alimchota mtama mama akaanguka. Ndipo Hussein alipoanza kumchoma visu mama sehemu mbalimbali za mwili na kisha kumkita nacho kichwani.”

KISU MWILINI MWAKE
Sarah tena:
“Baada ya kumchoma mama visu hivyo, nilishangaa kumuona Hussein na yeye akijichoma visu sehemu mbalimbali za mwili wake lakini mwisho alijikita nacho tumboni na kuanza kukitikisa kama vile alikuwa anauchanachana utumbo wake, akaishiwa nguvu na kuanguka. Ndipo wasamaria wema wakaanza kuwasogelea.”
Sarah alisema hata yeye alisogea eneo hilo na kuwakuta wote wamepoteza fahamu huku utumbo wa mwanume ukiwa nje na damu chapachapa ikiwa imetapakaa mwilini. Wakachukuliwa na kukimbizwa Hospitali ya Mkoa wa Ilala, Amana, Dar ambapo ni mita chache tu kutoka eneo la tukio.

MKE WA HUSSEIN SASA
Naye mke wa mtuhumiwa huyo aliyejitambulisha kwa jina la Zubeda Abeid alipopata nafasi ya kuzungumza na Uwazi alikuwa na ya kusema:“Ukweli taarifa hizi nimezipata kwa mshtuko mkubwa sana hali iliyonifanya nipoteze fahamu.
Hussein ni mume wangu wa ndoa, alinioa mwaka 1997 kijijini kwetu, Likombora mkoani Lindi. Tuna watoto wanne.
Hawara aliyechomwa kisu.
”Mwaka 2003 tulihamia hapa Dar kutafuta maisha zaidi ya Lindi, mwenzangu kazi yake ikiwa ni kuuza kahawa pale karibu na huyo hawara yake aliyemchoma visu. Mimi ni mama wa nyumbani tu.
“Sijui walihitilafiana kitu gani na huyo hawara yake maana leo ndiyo nimejua kumbe mume wangu alikuwa na hawara. Lakini hebu soma meseji hii kwenye simu yangu, alinitumia mume wangu mwanzoni mwa mwezi huu (Februari) bila kuhofia kuwa mimi ni mke wake.”

ILIVYOSOMEKA MESEJI
 “MAMA NEEMA NAKUOMBA MESEJI HIYO ISOME PEKE YAKO NA USIMWAMBIE MTU YEYOTE. MIMI NAJIUA KWA SABABU ESTER HANITAKI. WEWE BAKI NA WATOTO,  NIMEVUMILIA KUKUFICHA NIMESHINDWA. KWA HIYO MIMI NAJINYONGA, WEWE BAKI NA WATOTO.”
Baada ya Uwazi kuzungumza na mwanamke huyo, lilibahatika kuzungumza na dalali mmoja wa magari anayefanyia shughuli zake eneo hilo lakini aliomba jina lake lisiandikwe gazetini.
“Hussein alikuwa akimtuhumu dereva taksi mmoja kwamba anaingilia penzi lake na mwanamke huyo aliyemjeruhi na amekuwa akiahidi kulipa kisasi.
Mke wa ndoa.
“Yaani leo kama jamaa angekuwepo hapa basi ndiye angekuwa wa kwanza kuchomwa visu, pengine huyu mwanamke angefuatia,” alisema dalali huyo aliyeshuhudia tukio hilo.

MGANGA MKUU
Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana, Dk. Shaany Mwaruka alikiri kuwapokea majeruhi hao na kusema:
“Kwa sasa hali za majeruhi zinaendelea vizuri ingawa awali hali ilikuwa mbaya na kusababisha wakimbizwe chumba cha upasuaji kutokana na kisu kilichotumika kuingia sana ndani ya miili.”
#GP

MFAHAMU JAMAA PEKEE ANAYEMFAIDI AGNES MASOGANGE *PICHAZ*

Agness Masogange
Agness Masogange and the New Boyfriend
Masogange Did it Again...Showing off  Her Blessed FIGA And the New Boyfriend 

RED BRIGADE WA CHADEMA, WALIPO KULA KIAPO MBELE YA MBOWE, MWANZA *PICHAZ*

Vijana wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, almaarufu kama RED BRIGADE, wakila kiapo cha utii, mbele ya Mwenyekiti wa taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe, jijini Mwanza Jumamosi ya Februari 28, 2-015.
Kiapo hicho kinafuatia kkamilika kwa mafunzo ya kiulinzi na usalama kwa vijana hao, ambapo nchi inaelekea kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu 2015.
Vijana hao wakila kiapo mbele ya Mbowe, (kulia).
Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, Wilfred Rwakatare (kulia), kiasoma taarifa ya mafunzo ya vijana wa chama hicho 'Red Brigedi' huku mwenyekiti wa taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe (kushoto) akisikiliza kwa makini.
Vijana hao wakitoa heshima mbele ya Mwenyekiti wao Mbowe.
#Picha: Kivisblog

ZILIZOSOMWA ZAIDI