NYUMBANI KITAIFA

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BIASHARA

Ulimwengu wa habari.

MATAIFA MENGINE

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BURUDANI

Ulimwengu wa habari.

MAAJABU DUNIANI

Ulimwengu wa habari.

Monday, March 2, 2015

RAIS KIKWETE AONGOZA MAELFU YA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA KAPTEN JOHN KOMBA *PICHAZ*

Rais Kikwete akitoa salamu za mwisho mbele ya Jeneza lililobeba mwili wa Marehemu John Komba.



Viongozi mbali mbali wakiomboleza kwa kuondokewa na kiongozi mwenzao.

AZAM FC YAMTIMUA KOCHA WAKE BAADA YA KIPIGO CHA BAO 3 UGENINI

Na Bertha Lumala, Dar es Salam 
KIPIGO cha mabao 3-0 ugenini dhidi ya El-Merrikh ya Sudan, kimemponza kocha Joseph Omog baada ya uongozi wa Azam FC kuamua kumtimua.
Kwa mujibu wa taarifa iliyowekwa kwenye mtandao wa facebook wa Azam FC muda mfupi uliopita, Uongozi wa Azam FC umetangaza kumtimua raia huyo wa Cameroon.
Taarifa hiyo inasomeka:
“Uongozi wa Azam FC unatangaza kuachana na kocha wake mkuu Joseph Omog baada ya kuwa naye kwa miezi 14.
Omog aliyeipa Azam FC ubingwa wa kwanza msimu uliopita ameondoka pamoja na msaidiI wake Ibrahim Shikanda.
Kwa sasa timu itakuwa chini ya George Best Nsimbe.”
#ShaffiDauda.

Sunday, March 1, 2015

MFAHAMU IRENE SANGA; MCHEZA SINEMA, MUIGIZAJI, MWANDISHI NA MWANAMUZIKI


MSANII mwenye kariba ya kimataifa Irene Sanga anasema bado hajaachana na sanaa na kwamba zipo kazi nyingi amezifanya na nyingine zipo katika hatua mbalimbali na kwamba mashabiki wake watarajie kazi njema na zenye maana katika maisha yao. Beda Msimbe  amefanikiwa kuzungumza anaye Msanii huyu ambaye kwa sasa anatamba na mchezo wa jukwaani wa Africa Kills Her Sun ambao tayari umeoneshwa nchini marekani na Uganda. Fuatilia mahojiano haya:


SWALI:

 Ghafla haupo katika ulimwengu wa muziki wala sinema nini kimetokea? au majukumu ya uzazi yamezidi?
JIBU:
Hapana watoto wameshakuwa wakubwa ,mimi nafanya sanaa kama kawaida. Siku hizi naandika filamu. Nimeandika, Mikono salama ameprojuzi JB, nimeandika Kutakapo Kucha ameprojuzi Malalo na kuchezwa na Kitime; nimeandika Nyuma ya Pazia anaprojuzi Mtitu na ninafilamu inaitwa Mjomba ndio naendelea kuiandika pamoja na Nguvu ya Msamaha ipo katika drafti ya pili. Pia nina projekti ya Afrika inaua mwangaza wake ambayo tutaanza kuifanyia mazoezi kw amaonesho ya hapa nyumbani .Mara ya kwanza tulionesha Uganda Novemba mwaka jana
Aidha naandika  telebision series za Ubongo kids na kila kilenga. Pia nimeandika skripti za Babu Mbuyu za watoto bado zipo njiani kutoka chini ya kampuni ya Tanarea.

SWALI:
 Kumbe mwenzangu unahangaika katika sanaa mimi nadhani umetulia.
JIBU:
kweli kaka nipo sana na naandikaa vitu vingi mpaka muziki. kama unavyojua muziki upo damuni.

SWALI:
Naam naelewa mashairi yako huwa yanakuwa na moto mkali hasa katika jamii. Lakini kimya kirefu.
JIBU:
Si kirefu hivyoo.Ninamiziki miwili ipo Irie Production bado sijaimaliza ,mmoja unaitwa Enjoy mwingine unaitwa Africa Bara langu.Kiufupi bado nafanya sanaaaaaa tena sanaaaaa.

SWALI
Mengi tumeyaona lakini sikuwa najua kwamba wewe umo namna hii ndio maana nikauliza. Kuna vitu watu wanavifanya halafu wanapozungumza hawasemi kuhusu wamepata wapi vitu hivyo ili watu wajue kwamba katika sanaa mtu kutengeneza chakula kilichoandaliwa na mwingine. Haya reponse (Muitikio) ya filamu ulizoandika ( Je ni simulizi au andiko lenyewe ) ipi imeleta heshima sana mjini .Na hapo hapo nikuulize kwenye muziki tutarajie kama Mjomba au safari hii mapenzi hewani?
JIBU: 
Mvuto uko katika Mikono salama.Watu wengi walinipigia simu na kusema wameipenda. Kutakapokucha pia, lakini unajua sisi waandishi huwa hatujulikani sana,watanzania hawana utamaduni wa kusoma washiriki ,filamu ikiisha tu televisheni huzimwa na wasanii wakisifiwa hawana utamaduni wa kumsifia mwandishi nadhani ni Tanzania tu ambayo ipo nyuma kwa vitu kama hivyo,watu hawapendi kumpa credit, mtu sijui ilitokea wapi hata sijui siku zote anayepika hasifiwi ila aliyenenepa baada ya kula (anacheka).Kitu kingine ni Nyuma ya pazia ninadhani itakuwa nzuri zaidi kwa sababu napenda sana kuzungumzia habari za ukweli na zinazoendelea nchini kwetu,hiyo inahusu rushwa na uadilifu kazini

SWALI:
Naam kwahiyo mwaka huu ni mwaka wetu.Haya kampuni yako inaendeleaje?
JIBU:
Namshukuru Mungu inaendelea vyema ,japo changamoto ni nyingi,kufanya kazi bila meneja ni ngumu sanaaaa

SWALI:
Hata mimi naamini hivyo lakini kwanini humtafuti meneja?
JIBU
Sijui nianzie wapi kila mara na wish (natamani) ningekuwa naye kwa sababu kazi zote hizo nilizo kwambia hakuna hata moja nilioitafutia wateja bali watu wananitafuta na ninajisikia vibaya kukaa na idea ( mawazo)  huku  sina wa kusaidia kuzipush (kufikia walengwa) ,unajikuta umekaa tu huna cha kufanya wakati nilitakiwa kuwa busy(anacheka).

SWALI
Lazima kuna kasoro. Ninavyokujua wewe ungelikuwa na nafasi kubwa ya kumpata mtu wa kufanya naye kazi au watu wa hapa wamejawa na Longolongo ?
JIBU
Kaka Msimbe  ukipata meneja niambie nikae naye tuweke miradi hadharani,namiss sana sanaa ya jukwaani nataka kuifanyia mkakati sana

SWALI:
Je kama leo mtu angelikuuliza una miaka mingapi katika sanaa na nini umekiona Tanzania ungelisema vipi?Yaani kama kioo msanii wa tanzania anakosa kitu gani 
JIBU
Nina mika 15 katika sanaa. Ninavyoona mimi sanaa ya Tanzania imeingiwa na dosari ya kibiashara kuliko ubora. Kila mtu ni msanii,kila mtu anasaka pesa ,ukisimamia ubora inakula kwako.Sanaa mbovu zimejaa mtaani huku zikinunua airtime ili ziwe maarufu hasa upande wa muziki,upande wa filamu bila skendo hujawa msanii,utandawazi uhuru wa vyombo vya habarii umeifikisha sanaa hapa,tofauti na wenzetu nchi jirani mfano Kenya na Uganda pamoja na utandawazi sanaa yao inaubora sana.

SWALI:
ulizungumzia mchezo wa Afrika inaua Mwangaza wake, je hauna mpango  hasa wa kuonesha kwa watanzania katika matamasha makubwa ya sanaa?
JIBU: 
Niliongea na Dk Martin Mhando wa tamasha la nchi za Majahazi nahisi naweza kuperfome Africa kills her sun ZIFF bado tunaangalia jinsi ya kufanya.

SWALI:
Hii naipenda zaidi ya kuonesha ZIFF, kuna haja kubwa ya sisi kuona kazi za wazawa wa nchi hii kwani wana mengi wanayasema.sasa nikuulize kuhusu msimamizi meneja anatakiwa awe na sifa zipi au meneja anatakiwa aweje, sifa zipi na yukoje. 
JIBU:
Meneja anatakiwa auze mawazo kwa wadau mabalimbali wa sanaa,mfano tukifanya mazoezi ya mchezo ajue watazamaji watatoka wapi na kuwasaka na kutangaza kwa nguvu zote:kuwasiliana wa wafanya biashara ili waweze kuwekeza katika sanaa yetu na kadhalika. Tunafasi ndogo sana imaana tunahitaji mameneja ili wapigekelele watu waje waone ukweli ni kwamba hakuna sanaa nzuri kama ya jukwaani hasa ikuchanganywa na muziki, ngoma na ucheshi .

SWALI:
Swali hili ni la kizushi .Ulizaliwa wapi, ulisoma wapi, ulijifunza sanaa wapi, Nani role model, na kubwa zaidi mashabiki wako wategemee nini?
JIBU

Nimezaliwa hapahapa Dar, nimesoma Iringa girls na Ruvu ,nimesoma sanaa Chuo cha Bagamoyo na warsha katika nchi mbalimbali. Nampenda sana Kalola Kinashe,wanaonikubali waendelee kunikubali bado nakaza buti katika sanaa sijakata tamaa.

SWALI 
bnado hujasema miaka yako?

JIBU
kaka beda nawe! Wanawake hatutaji miaka ya kuzaliwa ila kwetu Makete ,Mwenge ndio hasa nilizaliwa Ocean road hospital .
mwisho

RATIBA YA KUUAGA MWILI WA MAREHEMU KAPTENI JOHN DAMIANO KOMBA


JENERALI ULIMWENGU: "KISWAHILI SI LUGHA YA TAIFA, NI MANENO YA KUUZIA MANDAZI NA POROJO ZA SIASA"

Na Jenerali Ulimwengu, 25 Feb 2015
MWAKA 2011 wakuu wa nchi yetu waliamua kwamba watasherehekea miaka 50 ya uhuru wa kitu fulani, lakini wakashindwa kusema ni kitu gani walikuwa wanasherehekea.
Baadhi ya maandiko yaliyotangazwa wakati huo yalisema kwamba ni sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Tanzania, lakini sote tunajua kwamba hakuna nchi iliyoitwa Tanzania iliyopata uhuru wake mwaka 1961. Baadhi yakasema kwamba ni miaka 50 ya uhuru wa “Tanzania Bara”, lakini tunajua vile vile kwamba hakuna nchi iliyoitwa Tanzania Bara iliyopata uhuru mwaka 1961.

wamba wakuu wetu walishindwa kusema ni kitu gani kilitokea tarehe 9 Desemba 1961 ni kielelezo cha tatizo kubwa tulilonalo katika kujenga utaifa wetu. Tunajifunga ndani ya ujinga tunapokataa kusema ukweli kwamba mwaka 1961 hakukuwa na nchi iliyoitwa Tanzania. Kilichokuwapo ni nchi iliyoitwa Tanganyika ikiwa chini ya himaya ya Uingereza kwa niaba ya Umoja wa Mataifa.
Tanganyika ilipata uhuru mwaka 1961 na miaka mitatu baadaye ikaungana na Zanzibar kuunda kile klichokuja kuitwa Jamhuri ya Muungano wa (ya) Tanzania.
Hili nalisema ili kuondoa utando uliofunika tafakuri zetu, utando ambao unatuelekeza kujifanyia mambo kwa kubabaisha tu, bila kujisumbua kufikiri angalau kidogo. Tungewekeza kidogo katika tafakuri kuhusu historia yetu, tungekuwa na nia ya kweli ya kuienzi nchi yetu na watu wake, tungekumbuka kwamba nchi hii (angalau ile sehemu ya nchi yetu inayoitwa ‘Bara’) ilikuwa inaitwa Tanganyika na ilikuwa na utambulisho wake katika jitihada za kujenga taifa huru na linalojiheshimu.

Katika utambuzi huo tungewatambua mashujaa wetu wa kweli na kuwatuza kwa nishani wanazostahili. Kwa kuwa hatuko tena katika ujenzi wa utaifa ila kila mmoja wetu anatafuta kujijenga yeye na familia yake, haya tumeyasahau na sherehe zetu za kuadhimisha hiki au kile zinakuwa ni fursa nyingine za watu kujitajirisha kwa kujipatia tenda za kutengeneza fulana au vitenge, ama za kuandaa hafla hii au ile.
Katika utafutaji huu, maana ya kweli ya shughuli yenyewe inakuwa ni ya mwisho kufikiriwa. Ndiyo maana katika kuwakumbuka wakuu mbalimbali, watu muhimu katika maisha yetu kama taifa lililokuwa likijijenga, tulijikuta tunatenda dhambi nzito. Inawezekana vipi, kwa mfano, kuwakumbuka ma-spika wa Buge letu waliopita, kisha ukawataja Pius Msekwa na Anne makinda, lakini tukamsahau Adam Sapi Mkwawa? Mimi sina ugomvi na waungwana hawa wawili, lakini katika kuwapima watu na mchango wao, tunaweza kweli tukatetea jambo kama hili? Kama si kukosa haya ni nini?
Tungekuwa tuna uwezo wa kuangalia tumefanya nini huko tulikotoka na kujifunza kutokana na makosa yetu ili tusiyafanye tena, tungejifunza kwamba hivyo sivyo mataifa yanavyokumbuka historia zake. Tungekuwa na busara za kuwakumbuka na kuwatunuku nishani watu waliofanya kazi ya kweli katika kutoa mchango wao katika ujenzi wa taifa tunalotaraji kujenga. Kumbuka nimesema mara kadhaa kwamba tunaweza kuwa na nchi lakini tusiwe na taifa.
Watu ambao nasema tungewakumbuka ni pamoja na hayati Shaaban Robert, ambaye katika kusherehekea miaka 50 (ya kitu fulani) hatukumsikia kabisa. Pamoja naye hatukuwasikia akina Kaluta Amri Abedi, Mathias Mnyampala, Akilimali Snowhite, Joseph Kiimbila na wengine waliochangia katika makuzi na maendeleo ya lugha ya Kiswahili.
Najua kwamba si waandishi wa Kiswahili tu waliosahauliwa katika maadhimisho hayo ya miaka 50 (ya kitu fulani).
Hatukuwasikia wanamichezo,wasanii, waalimu mashuhuri, wakulima mahiri. Lakini kutokuwapo kwa jina la Shaaban Robert miongoni mwa watu waliokumbukwa katika sherehe hiyo kulidhihirisha kwangu maana halisi ya sherehe hizo kama mahali pa kujikweza kwa baadhi ya watu na kutengeneza faida ya fedha kwa baadhi ya wengine. Ni sherehe zilizonyimwa heshima ambayo zingestahili.

Kwa nini Shaaban Robert si muhimu? Hivi tunaweza kufikiria kwamba Waingereza wanaweza kuadhimisha karne kadhaa za utaifa wao halafu wakawatunukia nishani wanasiasa na majemadari kadhaa waliopita lakini wakamsahau William Shakespeare, Goeffrey Chaucer au William Wordsworth?
Au Wafaransa wamsahau Moliere au Balzac, au Victor Hugo? Au Warusi wamsahau Alexander Pushkin au Lev Tolstoy ? Au Marekani wamsahau Mark Twain au John Steinbeck au James Fenimore Cooper ? Haiwezekani.
Kwetu sisi inawezekana, kwa sababu waandishi wetu hawana umuhimu kwetu. Tungekuwa tunajenga taifa, kundi moja ambalo lingekuwa mstari wa mbele kabisa katika utambulisho wa utaifa huo lingekuwa ni kundi la waandishi wa lugha ya taifa.

Tungewatambua kama viongozi wa utamaduni na fikra za kitaifa. Tungewaenzi. Hatuwaenzi kwa sababu hatujengi taifa, tunakubali na kufurahia kubaki tukiwa ni nchi tu, na kwa sababu hiyo hatuna lugha ya taifa. Kama hujengi taifa, huhitaji lugha ya taifa na usipokuwa na lugha ya taifa huwezi kuwa na taifa.
Jinsi tunavyokitumia Kiswahili ni kama misemo inayotufanya tuwasiliane na kubadilishana mawazo katika shughuli nyepesi nyepesi, katika biashara ndogo ndogo, masihara, mzaha na utani, na siasa za porojo. Katika matumizi ya Kiswahili hakuna jambo makini linalofanyika ambalo tunalijadili kwa makini.
Siasa ndicho kielelezo kikuu cha nafasi ya Kiswahili katika nchi yetu. Siasa yetu ni uwanja wa masihara, upuuzi na vichekesho vya wasanii wachovu. Tumekwishakuacha kutumai jambo la maana kutoka kwa wanasiasa isipokuwa kutufanya tucheke kwa huzuni. Hakuna wazo linalosanifiwa na kupangiliwa kwa weledi na likawasilishwa kwa werevu katika siasa zetu, kiasi kwamba siasa imekuwa na maana ya tamthilia isiyotarajiwa kuchukuliwa kwa uzito wowote.
Lugha ya taifa haina budi kutumika katika kuliendeleza taifa husika. Kuliendeleza taifa ina maana, kwanza ya kulifanya taifa liendelee kuwapo, lijiimarishe, lijiongezee uwezo wa kielimu, kisayansi, kiuchumi na kiutamaduni. Kwa maana hiyo, lugha ya taifa haina budi pia kuwa lugha ya elimu na sayansi na tafakuri.
Hivyo ndivyo ilivyokuwa huko tulikotoka kwa maana kwamba taifa la Wasukuma liliwafunza vijana wa Kisukuma kwa Kisukuma. Viwango vya sayansi ya Kisukuma ya wakati huo ndivyo vilivyokuwa, na uwezo wa Wasukuma wa kuielewa dunia ndivyo ulivyokuwa, lakini kila walichojua walikirithisha kwa vizazi vipya kupitia lugha ya taifa lao, yaani Kisukuma.
Haiwezi kuwa tofauti katika taifa la kisasa. Hatuwezi kuwa na lugha ya taifa kwa sababu tu eti tuna Katiba inayotamka kwamba Kiswahili ni lugha ya taifa, au sheria iliyotungwa na Bunge. Lugha ya taifa hujengwa kwa vitendo, hususan kwa kuitumia katika shughuli nzito kama elimu, sayansi teknolojia na tafakuri za kina.
Kiswahili, kama tunavyokitumia hivi sasa, ni ‘lingua franca, ’ lugha nyepesi ya kuelewana katika mambo madogo madogo yasiyokuwa na umuhimu mkubwa. Ni lugha ya kuuza na kununua mandazi na njugu.
Kuna wakati Kiswahili kilikuwa kwa kasi kubwa, na kikaimarika katika medani ya siasa. Kiswahili kilikuwa ndiyo nguzo kuu katika kujenga utaifa wa Watanganyika wa wakati wa kudai uhuru, na katika kujenga utaifa wa Watanzania kama mataifa mawili yaliyoungana. Lakini kwa sasa, Kiswahili kimedumaa na kinazidi kudumaa kwa sababu hakina jukumu la msingi la kutekeleza; tumekitelekeza.

Ndiyo maana tunaweza kukusanyana na kupeana nishani za miaka 50 (ya kitu fulani), lakini tukamsahau Shaaban Robert.

Wasiliana na mwandishi
Jenerali Ulimwengu
ulimwengu@jenerali.com au www.jenerali.com
Jenerali Ulimwengu ni Mwanajopo la Wataalam la Baraza la Habari Tanzania (MCT).

RAIS KIKWETE AFIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU KOMBA, SOMA HISTORIA FUPI YA MAREHEMU *PICHAZ*

 













 HISTORIA YA MAREHEMU JOHN DAMIANO KOMBA 
1954 Alizaliwa 1963-70 Shule ya Msingi Lituhi 1971-74 Shule ya Wavulana Songea 1975-76 Chuo cha Ualimu Kleruu 1988-90 Chuo cha Magdeburg path 1978-79 Chuo cha Kijeshi Monduli 1978-92 Ofisa wa JWTZ 2006-08 Chuo Kikuu cha Washington 2005-15 Mbunge Mbinga Magharibi.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Amen! 

KANYE WEST & DIAMOND WANAONGOZA WANAVYOWASHIKA…WAPENZI WAO *PICHAZ*

Diamond na Zari
Kanye west na Amber, Kim ambapo wasanii hawa wamekuwa wakiwashika makalio wapenzi wao hadharani….!
Shuka koment yako hapo chini mdau…!

ZILIZOSOMWA ZAIDI