Friday, September 18, 2015

BAADA YA KUWA MPWEKE MUDA MREFU PENNY AIBUKA NA KUSEMA AKIPATA MWANAUME BORA ANAZAA SOON


Na imelda mtema
Hosti wa Kipindi cha Bongo Star Search, Penniel Mingilwa ‘Penny’ amefunguka kuwa suala la kupata mtoto lipo kwenye akili yake lakini litatimia tu endapo atapata baba bora.

Akizungumzia maisha yake ya kimapenzi kwa sasa Penny alisema kuwa, hawezi kuyaanika kwa sasa ila ukweli ni kwamba hamu ya kuitwa mama anayo na anaamini akimpata mwanaume sahihi anayeweza kumudu jukumu la kuwa mzazi, atazaa na kuyaacha maisha yaendelee.

“Kwa maneno haya mtu anaweza kudhani nabagua lakini ninachotaka mimi ni kuwa na baba wa mwanangu anayejua maana ya familia nisije kumuumiza mtoto wangu bure,” alisema Penny.
Source:GPL

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI