Thursday, August 27, 2015

RAIS WA SYRIA ALAUMU MATAIFA YA NJE

Akionena katika ofisi ya Rais mjini Damascus, amesema azimio la mgogoro wa kisiasa wa Sryria litafikiwa tu endapo nchi za nje zitaacha juhudi za kukandamiza serikali yake.
Rais wa Syria, Bashar al-Assad amelaumu mataifa ya nje kuingilia vita ya wenyewe kwa wenyewe ya miaka minne nchini mwake kwa kusema hatoruhusu waangalizi wa kimataifa katika uchuguzi wowote ujao.
 Akihojiwa na kituo cha televisheni cha Al-Manar, ambacho kinaendeshwa na kundi la wanamgambo wa Hezbollah, Bwana Asad alisema hapana kwa waangalizi wa kimataifa akidai huko ni kuingilia dola la Syria.
Shirika la habari la Associated Press limeripoti kwamba, Bwana Assad aliongeza kusema kwamba ni chombo gani cha kimataifa ambacho kimepewa mamlaka ya kutoa cheti cha ufanyaji kazi mzuri.

Akionena katika ofisi ya Rais mjini Damascus, amesema azimio la mgogoro wa kisiasa wa Sryria litafikiwa tu endapo nchi za nje zitaacha juhudi za kukandamiza serikali yake.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI