Katibu
wa Taswa mkoa wa Arusha, akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana
na tamasha la waandishi Agosti 29 uwanja wa kheikh Amri Abeid mgeni
rasmi mkuu wa mkoa wa Arusha, Filex Ntibenda, kati kati mwenyekiti wa
taswa mkoa Arusha, Jamila omar, Meneja matukio ya kampuni ya bia nchini
TBL Chris Sarakana ambao wadhamini wakuu, na makamu Mwenyekiti wa Taswa
Arusha, Andrea Ngobole
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Felix
Ntibenda, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tamasha la 10 la vyombo
vya habari vya mkoa wa Arusha. Ambalo litafanyika Agosti 29 katika
uwanja wa sheikh Amri Abeid.
Akizungumza na waandishi wa
habari Palace hoteli mwenyekiti wa TASWA mkoa wa Arusha, Jamila Omar
na Katibu wa TASWA Arusha, Mussa Juma walisema maandalizi yote muhimu
yamekamilika ikiwepo ujio wa timu ya TASWA kutoka jijini Dar es Salaam.
Omar alisema Kauli mbiu ya
Mwaka huu ya Tamasha hilo ni kuwa,Uchaguzi bila vurugu inawezekana na
timu zitachuana katika michezo ya Soka, mbio zamagunia, kuvuta kamba,
kukimbiza kuku na mpira wa pete.
Alisema mdhamini Mkuu wa
Tamasha hilo ni Kampuni ya Bia nchini(TBL), ambapo wadhamini wengine ni
TANAPA, Faidika, Mega Trade Investment,na SBC(T) Ltd.
Omar aliwataja wadhamini wengine kuwa ni, Shilika na nyumba nchini(NHC), Kampuni ya Tanzanite One,Coca cola na Big Expedition.
Akizungumzia tamasha hilo,
Afisa matukio ya TBL Arusha, Chris Sarakana aliwataka wanahabari na
wakazi wa mkoa wa Arusha kujitokeza na kuahidi TBL itaendelea
kushirikiana na wanahabari.
Awali Katibu wa TASWA mkoa wa
Arusha,Mussa Juma alitaja timu nyingine zitakazoshiriki ni TASWA Arusha,
AJTC. Habari Maalum,Radio 5, Radio ,Faidika,Mj radio, Arusha one na ORS
kutoka mkoa wa Manyara.
Alisema kabla ya Tamasha
wanahabari watatembelea hifadhi ya Taifa ya Arusha vile vile kiwanda
cha Bia nchini(TBL) mkoa wa Arusha na viwanda vya Mega Trade na Pepsi
mkoani hapa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 ya bonanza hilo
0 comments:
Post a Comment