Sunday, August 30, 2015

CHADEMA NA UKAWA WAZINDUA KAMPENI ZAO KWA KISHINDO JANGWANI JIJINI DAR *PICHAZ NA VIDEOZ*

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea mwenza, Mh. Juma Duni Haji wakiwasili kwenye viwanja vya Jangwani Jijini Dar es salaam, kulikofanyika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, Agosti 29, 2015.
 Umati wa wakazi wa Jijini Dar es salaam, ukiwa umefurika kwa wingi kwenye viwanja vya Jangwani kuwalaki Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea mwenza, Mh. Juma Duni Haji, walipokuwa wakiwasili viwanjani hapo, kulikofanyika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, Agosti 29, 2015. 
Wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA wakiwashangilia Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea mwenza, Mh. Juma Duni Haji, walipokuwa wakiwasili viwanjani hapo, kulikofanyika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, Agosti 29, 2015. 
Wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA wakionyesha furaha yao kwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mgombea Urais wa Zanzibar katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad wakati alipowasili kwenye viwanja vya Jangwani Jijini Dar es salaam, kulikofanyika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, Agosti 29, 2015. 
Sehemu ya Wanahabari kutoka Vyombo mbali mbali nchini wakiendelea kuchukua habari za Mkutano huo, uliofanyika jioni ya kwenye viwanja vya Jangwani Jijini Dar es salaam na kuhudhulia na maelfu ya Wakazi wa jiji hilo.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe akimkabidhi, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea mwenza, Mh. Juma Duni Haji, Kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho kwa mwaka 2015/2020 mara baada ya kuizindua, Agosti 29, 2015.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, Mgombea mwenza, Mh. Juma Duni Haji pamoja na Mgombea Urais wa Zanzibar katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad wakionyesha vitabu cha Ilani ya Uchaguzi mara baada ya kuzinduliwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe. 
Viongozi wa Vyama mbali mbali vinavyounda UKAWA wakionyesha Ilani hiyo mbele ya maelfu ya wakazi wa Jiji la Dar es salaam, Agosti 29, 2015.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe (kulia) akiwatambulisha baadhi ya Wagombea Ubunge katika Majimbo mbali mbali ya jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA, Mh. James Mbatia akizungumza kwenye Mkutano huo.
Watu wa Msalaba Mwekundu wakiwa wamembeba mmoja wa wakazi wa Jiji la Dar aliepoteza fahamu kwa kukosa hewa kutokana na uwingi wa watu uliofurika kwenye viwanja vya Jangwani, Jijini Dar es salaam Agosti 29, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye akitoa salamu zake kwa wakazi wa Jiji la Dar es salaam waliofurika kwenye viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam leo Agosti 29, 2015.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiteta jambo na Mgombea Mwenza wake, Mh. Juma Duni Haji, wakati wa Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, uliofanyika Agosti 29, 2015. 
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akihutubia katika Mkutano huo wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, uliofanyika Agosti 29, 2015. 

Mmoja wa wanasiasa wakongwe waliotoka CCM, Tambwe Hiza akisalimia.








Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema kupitia Ukawa, Mh Edward Lowassa akiongea na wakazi wa jiji la Dar waliojitokeza katika uzinduzi wa Kampeni za Ukawa katika viwanja vya Jangwani mapema.
Mh Lowassa amesema kipaumbele chake kimoja wapo ni Elimu huku akisisitiza kuwa kampeni zao zitakuwa ni za busara na hekima bila kutumia matusi.
Mke wa Mgombea Urais kupitia Chadema chini ya mwamvuli wa Ukawa, Mama Regina Lowassa akitoa salamu kwa wakazi wa Jiji la Dar Waliojitokeza katika uzinduzi wa kampeni za Ukawa katika viwanja vya Jangwani.
Mgombea mwenza wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Duni Haji akihutubia maelfu ya wakazi wa jiji la Dar waliojitokeza kushuhudia uzinduzi wa Kampeni za Ukawa katika viwanja vya Jangwani
Mwenyekiti wa Chadema, Mh Freeman Mbowe akiwasalimu wakazi wa jiji la Dar Waliojitokeza katika uzimduzi wa Kampeni za Ukawa zilizofanyika Jangwani.
Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mh Freeman Mbowe (wa kwanza kulia) akiwa na wagombea urais kwa Upande wa Zanzibar na Upande Wa Bara na mgombea mwenza bara wakionyesha Kitabu chao cha Ilani ya Uchaguzi mwaka 2015 katika uzinduzi wa kampeni za ukawa uliofanyika katika viwanja vya jangwani.
Halima Mdee akihutubia
 
 Wagombea Ubunge katika majimbo ya Dar Es Salaam wakitambulishwa mbele ya wakazi wa jiji la Dar waliojitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa Kampeni za Ukawa zilizofanyika katika Uwanja wa Jangwani.
 Mgombea ubunge wa jimbo la Kisarawe kwa tiketi ya CUF Kingwendu akisikiliza hotuba ya mgombea urais kwa tiketi ya Chadema chini ya Mwamvuli ya Ukawa
 Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, Mh James Mbatia akihutubia maelfu ya wakazi wa jiji la Dar Waliojitokeza katika uzinduzi wa Kampeni za Ukawa jangwani jijini Dar
 Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya tatu, Mh Fredrick Sumaye akihutubia wakazi wa jiji la Dar waliofika katika viwanja vya Jangwani wakati wa uzinduzi wa kampeni za Ukawa
 Umati wa watu waliojitokeza katika uzinduzi wa kampeni za Ukawa katika viwanja vya jangwani
 Mgombea Urais kwa tiketi ya Chadema na Mgombea Mwenza wakiwaaga watanzania waliojitokeza katika viwanja vya jangwani katika uzinduzi wa kampeni za Ukawa
Moja ya kifaa cha Kisasa kabisa aina ya Drone ambacho kilikua kikitumika kupiga picha kutoka anagani ambacho kimekuwa kivutio kikubwa kabisa kwa wakazi wa jiji la Dar Es Salaam katika viwanja vya jangwani .
#Picha: Josephat Lukaza wa Lukaza Blog
na
OTHMAN MICHUZI

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI