NYUMBANI KITAIFA
Ulimwengu wa habari.
KATIKA BIASHARA
Ulimwengu wa habari.
MATAIFA MENGINE
Ulimwengu wa habari.
KATIKA BURUDANI
Ulimwengu wa habari.
MAAJABU DUNIANI
Ulimwengu wa habari.
Thursday, April 30, 2015
Wednesday, April 29, 2015
SHAMSA FORD: MNIKOME KUANZIA LEO NAISHI NITAKAVYO MIMI NA KUFANYA KILE AMBACHO NAHIC KINAFAIDA KWANGU
4:31 AM
No comments
BAADA ya kuchoshwa na maneno ya watu kuhusu maisha yake binafsi, staa mrembo wa Bongo Movies, Shamsa Ford ameamua kuweka wazi msimamo wake kwa mashabiki zake wote.
“Siku zote nimekuwa muoga kuishi maisha yangu kwa kuogopa watu but hao watu naowaogopa hata siku moja hawajawahi kuogopa kuishi maisha yao kwa kuniogopa mm.. from today nitaishi nitakavyo mimi na kufanya kile ambacho nahic kinafaida na kunifurahisha katika maisha yangu. Mashabiki wangu wa ukweli kabisaa alionipangia Mungu hata niweje hawawezi Kunitoka na nitaendelea kuwapenda na kuwaheshimu kila siku..
I love my family….”
–Shamsa ameandika hayo leo kwenye ukurasa wake mtandaoni.
Friday, April 24, 2015
JOH MAKINI AACHIA VIDEO MPYA - NUSU NUSU
10:08 AM
No comments
JOH MAKINI amekuwa ni mmoja wa wasanii ambao wamekuwa wakifanya kazi zao vizuri ili 'kutusua' kimataifa ambapo kwa sasa msanii huyu mahiri ameachia kichupa kingine cha ukweee sana 'Nusu nusu' kupitia kituo cha kimataifa cha MTV Base 'Spanking New'
Joh ameutaarifu ULIMWENGU WA HABARI kuwa Video hiyo imeongozwa na Justin Campos muongozaji aliyeongoza ile Video ya Vanessa na K.O - 'No body but me' ambayo mpaka sasa inafanya vizuri tu katika vituo mbalimbali vya kimataifa kama vile Trace Urban, MTV Base na Sound City ya Nigeria.
Video hiyo mpya ya Joh Makini utaiona kupitia MTV Base na katika mitandao mbali mbali ya kijamii.
BIBI WA MIAKA 54 ALIA BAADA KUTOROKWA NA MCHUMBA WAKE WA MIAKA 25 *PICHA*
10:01 AM
No comments
HARUNI SANCHAWA NA MAKONGORO OGING, PWANI
LILE sakatala lililotamba kwenye vyombo vya habari la bi harusi, Bahati Mwakambonja (54), kutaka kufunga ndoa na kijana wa miaka 24, Isiaka Jeremiah limechukua sura mpya baada ya bwana harusi huyo kutoweka nyumbani Mkuranga, Pwani na kwenda kusikojulikana huku bibi huyo akishinda analia.
Bibi Bahati Mwakambonja anayedai kutorokwa na mchumbaake.
Timu ya Amani hivi karibubni ilifika nyumbani kwa mwanamke huyo mjini Mkuranga na kumkuta katika lindi la mawazo.Akizungumza na gazeti hili kwa masikitiko makubwa, Bahati alisema: “Mchumba wangu kakimbia jamani. Niliwashangaa sana viongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Kurasini (Dar) kukwamisha ndoa yangu na yule mchumba wangu, nimehuzunika kwa kiasi kubwa hadi sasa.
“Kwanza nikiri kwamba mimi sizai, hiyo ni mipango ya Mungu, huwezi kulazimisha hali niliyonayo. Tumekaa kwa muda mrefu bila kufunga ndoa lakini ilifikia hatua tukaamua kitu ambacho hata kwa Mungu ni baraka kwetu lakini matokeo yake imekuwa kinyume,” alisema mwanamke huyo.
Bibi huyo alisema kama kuolewa na huyo kijana alishaolewa kwa sababau walishaenda sehemu zote mbili, yaani nyumbani kwa mwanaume na kwa mwanamke.“Mume wangu alifanya mazungumzo na familia yangu na kuhojiwa maswali kadhaa ambayo aliyajibu na kuambiwa atoe mahari kitu ambacho alifanya kwa kutoa sehemu ya mahari.
“Hatua tuliyokuwa tunakwenda ndugu waandishi ya kukamilisha taratibu za ki-Mungu ambapo tunajua kila mtu ana sehemu anayoiabudu hapa duniani na mimi nilikwenda pale kwa sababu ni eneo ambalo nilikuwa nikipata huduma kabla ya kuhamia hapa Mkuranga.
“Lakini baada ya kufika eneo lile nikaambiwa mambo ambayo nilikuwa siyategemei hata siku mmoja, likiwemo la kuwasilisha barua ya talaka au cheti cha kifo cha mume wa kwanza.“Mimi niliachana na mume wa kwanza kwa muda mrefu sana na alinikataa kwa sababu sizai na kuwaambia wale waliosimamia ndoa ya awali kuwa anawaruhusu kama nikipata mchumba niolewe,” alisema Bahati.
Aidha, alisema kuna watu waliwafuata wakiwaahidi watawasaidia ili kufanikisha kufungwa kwa ndoa hiyo lakini matokeo yake baada ya wao kuondoka walishitukia taarifa hizo ziko kwenye magazeti.
Alisema baada ya Isiaka kuona taarifa hizo kwenye gazeti alitoweka na baadhi ya vielelezo kama picha walizopiga siku za nyuma.
“Mimi kama mtu mzima nimechaganyikiwa hasa baada ya ndoa yangu kukataliwa sehemu zote nilizokwenda na kibaya zaidi ni pale mume wangu kuondoka na vitu muhimu kwenda nisikokujua, hana simu.Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kuwa, mama huyo kwa sasa anajitafutia kipato cha kila siku kwa kufundisha watoto wadogo wapatao 8 ambao kila baada ya kufundisha hulipwa shilingi 200 kwa siku. Alisema kuwa hana uchumi mwingine.
Alisema uhusiano wake na kijana huyo ulianza baada ya kukaa kwa muda mrefu bila kuolewa lakini chanzo kikubwa kilichomkutanisha na Isiaka ni ugonjwa wa kisukari uliyokuwa unamsumbua kwa muda mrefu.
Alisema yeye na mume wake wa kwanza walioana mwaka 1992 na kuachana 1995. Alikaa hapo mpaka Januari 2003 alipokutana na kijana huyo.
Aliongeza kuwa walipokutana na kijana huyo hawakuanza uhusiano moja kwa moja lakini baada ya kuona anampa msaada ambao hata mbele za Mungu inakubalika ndipo waliamua kuingia katika uhusiano wa kimapenzi hatimaye kulipa mahari na hatimaye kanisani ambako walikataliwa kutokana na tofauti ya umri.
Baadhi ya majirani waliozungumza na Amani kuhusiana na sakata hilo walisema:
“Ni kweli kijana huyo alikuwa akionekana eneo hilo na kila mtu alijua ni mfanyakazi wa mama huyo.
“Hakuna aliyefikiria kijana huyo ndiye mume wa mama huyo,” alisema jirani mmoja.
Amani lilimtafuta Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ushirika wa Kurasini, Dar, Yusuf Ngelein ambapo alikiri kumfahamu Bahati kama muumini wake.“Alifika hapa na mwenzake kutaka taratibu za kufunga ndoa. Mimi kama kiongozi wa kanisa nilimpa vigezo vya kutimiza lakini hawakurudi maana yake walikuwa na upungufu,” alisema mchungaji huyo
BILIONEA DANGOTE ATUA MTWARA KUCHEKI ENEO ANALOTARAJIA KUTENGENEZA BANDARI
9:56 AM
No comments
Biionea Alhaji Aliko Dangote amekabidhiwa hekari 2,500, katika halmashauri ya Wilaya ya Mtwara ili ajenge bandari itakayotumika kusafirisha saruji kutoka kiwandani hapo kwenda maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.
Mfanyabiashara maarufu Afrika, ambaye ni Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote Group of Industries, Alhaji Aliko Dabgote akinyoosha mkono kuangalia eneo la ufukwe wa Bahari ya Hindi katika Kijiji cha Mgao, Kata ya Maumbu, Tarafa ya Mayanga, Mtwara Vijijini, ambapo atajenga bandari yake ya kisasa kwa ajili kusafirisha saruji itakayozalishwa kwenye kiwanda chake kikubwa kinachojengwa katika Kijiji cha Msijute.
Alhaji Dangote akishuka kwenye ndege na kulakiwa na Mwakilishi Mkazi wake hapa nchini, Esther Baruti
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mgao, Shaa (kushoto) akimuonesha Dangote eneo la uwanja aliopewa na wanakijiji kwa ajili ya ujenzi wa mkazi yake. Kijiji nacho kitanufaika na Dangote ambaye atawajengea shule, hospitali pamoja na miradi mingine ya maendeleo.
Msafara wa Dangote ukitumia magari kutembelea kiwanda cha saruji kinachojengwa.
MHE ANDREW CHENGE AZUA TIMBWILI JIPYA OFISI ZA CHADEMA BARIADI, RISASI TATU ZAFYATULIWA HEWANI
8:13 AM
No comments
Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge.
******
Wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiongozwa na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, wanadaiwa waliingia ‘anga’ za ofisi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilaya ya Bariadi na kusababisha taharuki kubwa, baada ya mmoja wa wafuasi wake kudaiwa kufyatua risasi tatu hewani.
Tukio hilo lilitokea katika ofisi za Chadema juzi saa 1:30 jioni baada ya wafuasi wa Chadema kumsindikiza mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec), John Heche, aliyetoka kumsindikiza Naibu Katibu Mkuu Bara wa chama hicho, John Mnyika, aliyekuwa akienda wilayani Maswa kwa shughuli za kichama.
Msafara wa Chenge ulikuwa ukitokea katika mkutano kwenye kijiji cha Isanga, na wale wa Chadema wakiwa wamerudi toka mkutano uliofanyika viwanja vya Basketi mjini hapa, ndipo walipokutana na msafara wa Chenge jirani na ofisi za Chadema na kuanza mabishano.
Inadaiwa msafara wa Chenge ulisimama katika ofisi hizo ukiwa na magari matano, huku moja ya magari hayo likipiga muziki kwa sauti kubwa, hali iliyosababisha wafuasi wa Chadema kuurushia mawe na kuwazomea.
KAULI YA POLISI
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Gemini Mushi, alisema vyama hivyo baada ya kumaliza mikutano yao, Chadema walianza safari ya kuelekea ofisini kwao katika barabara ya Maswa, huku msafara wa Chenge ukitokea kijiji cha Isanga kurejea mjini.
Alisema baada ya msafara wa Chenge kufika jirani na ofisi za Chadema walikutana na kundi kubwa likishangilia, ndipo mbunge huyo aliposhuka katika gari na kuanza kucheza nao, lakini wakati wafuasi hao wakiendelea kushangilia, walisikia sauti ikisema rusha mawe iliyosababisha mbunge huyo kukimbilia ndani ya gari.
Kamanda Mushi alisema baada ya wafuasi hao wa Chadema kurusha mawe kwa kulishambulia gari la Chenge, ndipo kada wa CCM (jina tunalihifadhi kwa sasa) alipotumia bastola yake kurusha risasi tatu hewani ili kuwatanya watu waliokuwa wamezingira msafara huo na watu hao kutawanyika.
Hata hivyo, kamanda huyo hakueleza kama mtu huyo amekamatwa na kama kuna ganda lolote la risasi ambalo polisi waliliokota.
MASHUHUDA WANENA
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo, walisema wafuasi wa Chadema walianza kurusha mawe ndipo mbunge huyo alipokimbilia ndani ya gari yake.
“Tulishangaa kuona wafuasi wa vyama hivyo wakianza kushambuliana kwa mawe baada ya kutokea kwenye mikutano yao ya hadhara na kufika maeneo hayo,” alisema Mkuba Majaliwa.
VIONGOZI WA CHADEMA
Akizungumzia tukio hilo, John Heche, alisema wafuasi wa CCM walipita katika ofisi za chama chao na kukutana na viongozi pamoja na wafuasi waliotoka mkutanoni huku CCM wakipiga muziki, hali ambayo ilisababisha baadhi ya viongozi kuwazuia kwa madai ya kuwataka kupunguza sauti ya muziki.
“Msafara huo ulifika ofisi ya Chadema baada ya kutoka katika mikutano yao na ulipofika maeneo ya ofisi zetu walisimamisha magari yao na kuanza kupiga muziki na wafuasi wao waliteremka kwenye magari yao na kuanza kucheza hali iliyosababisha wafukuzwe kwa mawe na wafuasi wa chama changu,” alisema Heche.
VIONGOZI WA CCM
Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Wilayani Bariadi, Sai Samba, alisema baada ya kufika jirani na ofisi ya Chadema walikuta kundi la vijana wakiwa wamejipanga barabarani na kuzuia msafara wao kwa kurusha mawe mbele ya gari la Chenge, hali iliyomlazimu mmoja wa wafuasi wa Chenge kurusha risasi hewani kwa lengo la kuwatawanya.
Hata hivyo, NIPASHE ilipomtafuta Chenge kwa ajili ya kuzungumzia tukio hilo, hakupokea simu yake ya mkononi. #NIPASHE
JACK DUSTAN: WAUME ZA WATU WATATUUA
5:12 AM
No comments
STAA aliyepata umaarufu kupitia Shindano la Maisha Plus, Jacqueline Dustan amefunguka kuwa mastaa wamepachikwa nembo ya kuwa ni vinara wa kubeba waume za watu jambo ambalo linawapa sifa mbaya.
Akizungumzia mwenendo wa mastaa wengi kuhusishwa na skendo ya kutembea na waume za watu, Jack alisema:
“Yaani sisi mastaa tumepachikwa nembo ya kupora waume za watu. Imefika wakati hata kama umempata mpenzi wako mtu anakuuliza umempora nani. Huwa inaniuma sana.
“Kimsingi tuna sifa mbaya na tusipobadilika waume za watu hawa watatuua.”
OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAFANYA UCHAGUZI KUMTAFUTA MFANYAKAZI BORA 2015
2:39 AM
No comments
Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakitoa salamu ya wafanyakazi wakati wa uchaguzi wa kumpata mfanyakazi bora wa ofisi kwa mwaka 2015 uliofanyika jana katika ofisi hiyo.
Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakisikiliza maelekezo ya uchaguzi wa mfanyakazi bora wa ofisi kwa mwaka 2015 uliofanyika jana katika ofisi hiyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji wa Maadili Bw. Methew Kirama mwenye Ipad (wa kwanza kushoto) akichukua matukio wakati wa uchaguzi wa kumpata mfanyakazi bora wa ofisi ya Rais – Utumishi kwa mwaka 2015 uliofanyika jana katika ofisi hiyo.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu akimtangaza mfanyakazi bora wa ofisi wa mwaka 2015 mara baada ya uchaguzi kufanyika jana katika ofisi hiyo.
Mfanyakazi bora wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma wa mwaka 2015 Bw. Francis Sangunaa (kulia) akiwashukuru watumishi baada ya kuchaguliwa katika uchaguzi uliofanyika jana.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu akitoa maelekezo ya kumpata mfanyakazi bora wa ofisi kwa mwaka 2015 uliofanyika jana.
Wednesday, April 22, 2015
SIMBA YA EMMANUEL OKWI YAIFUMUA MGAMBO JKT 4-0 LIGI KUU TANZANIA BARA UWANJA WA TAIFA DAR ES SALAAM
9:56 AM
No comments
TIMU ya Wekundu wa Msimbazi Simba SC, leo imefuta machungu ya kupoteza mchezo uliopita jijini Mbeya dhidi ya Mbeya City baada ya kuwashushia mvua ya magoli wanajeshi wa Mgambo JKT kutoka jijini Tanga kwa kuwachakaza magoli 4-0 katika mchezo ulipigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Simba wakiwa katika kiwango cha hali ya juu kabisa hii leo walianza kuliona lango la mgambo JKT mapema kabisa mnamo dakika ya 8 kupitia kwa mshambulizi wao machachari kutoka nchini Uganda Emmanuel Okwi baada ya krosi nzuri kabisa ya Ramadhan Kessy aliyegongeana pasi kwa uzuri na Ramadhan Singano 'Messi'.
Wakiendelea kupekeleka mashambulizi langoni mwa mgambo kama Mvua, Simba walifanikiwa kuandika bao la pili mnamo dakika ya 15 kupitia kwa winga wake msumbufu Ramadhan Singano 'Messi' kutokana na mpira wa adhabu aliouchonga kwa umaridadi wa hali ya juu na kuingia moja kwa moja wavuni huku akimuacha mlinda mlango wa Mgambo JKT Godson Mmasa akiwa hana la kufanya.
Mgambo walijitahidi kufanya shambulizi langoni mwa Simba mnamo dakika ya 26, lakini shuti la mshambuliaji wa Mgambo Malimi Busungu liliokolewa maridadi kabisa na mlinda mlango wa Simba Ivo Mapunda.
Simba waliendelea kulisakama lango la Mgambo JKT na hatimaye katika dakika ya 41 Okwi kwa mara nyingine tena aliweza kuifungia Simba bao la 3 baada ya mabeki Mgambo kujichanganya na yeye kumtoka mmoja wao kabla ya kuachia shuti kali na kutinga kimiani.
Mgambo walijaribu tena kutafuta goli langoni mwa Simba lakini ukosefu wa umakini kwa Salim Azizi Gilla uliwakosesha bao baada ya kufika langoni na kupaisha mpira juu.
Mvua ya ya magoli iliendelea kumiminika langoni mwa Mgambo baada ya Emmanuel Okwi kuifungia Simba bao la nne huku kwa upande wake likiwa ni bao la tatu la mchezo (hat-trck) mara baada ya kuwachambua mabeki wa Mgambo na kufunga goli kirahisi kabisa.
Mgambo walijitahidi kutafuta walau goli la kufutia machozi wakati walipopeleka shambulizi la kushtukiza langoni mwa Simba lakini hata hivyo Ivo Mapunda aliokoa na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.
Ilikuwa almanusura Simba waandike bao la tano baada ya Okwi kuwachambua kwa uzuri mabeki wa Mgambo na kumpasia mpira Jonas Mkude lakini shuti lake lilimlenga mlinda mlango wa Mgambo na kuudaka mpira huo.
Mapaka mwamuzi wa mchezo anapuliza kipyenga cha mwisho Simba waliibuka na ushindi mnono wa mabo 4-0 dhidi ya Mgambo kutoka jijini Tanga huku nyota wa mchezo wa leo Emmanuel Okwi akijiondokea na mpira wake baada ya kukwamisha kimiani mabao matatu (hat-trick).
Ikumbukwe tu hiki ni kigo cha pili kizito ambacho Simba imekitoa kwa Mgambo JKT ikiwa mwaka jana wakiifunga magoli 6-0 katika dimba la Taifa huku Amissi Tambwe ambaye kwa sasa yupo Yanga akipiga hattrick pia.
Tangu ipande daraja timu ya Mgambo JKT imekutana na Simba mara 6 na kushinda mara mbili, huku wao wakipoteza mara tatu na kutoka sare mara moja.
Sio Simba wala Mgambo ambaye amewahi kupata ushindi nyumbani kwa mpinzani wake isipokuwa Mgambo iliwahi kupata sare mbele ya Simba katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo baina ya Polisi Moro SC na Coastal Union umemaliza kwa kushindwa kutambiana.
kutokana na matokea hayo Coastal Unioni imejiongezea pointi moja na kufikisha 28 huku Polisi Moro ikifikisha pointi 25 baada ya kugawana pointi moja moja kufuatia sare tasa ya 0-0 katika uwanja wa jamhuri Morogoro.
Tuesday, April 21, 2015
NDEGE YA KIPEKEE INAYOTUMIA NGUVU YA JUA ILIKWAMIA CHINA, KITU KIMOJA TU KIMEIKWAMISHA *PICHAZ*
12:56 AM
No comments
Ni ndege ambayo ilianza safari yake March 9 2015 Abu Dhabi na ikafanikisha salama safari zake kwa kupaa angani na kupita Oman, India na Myanmar.
Marubani wawili wanaoiendesha wanasema wanataka kuvunja rekodi kwa kuuthibitishia ulimwengu kwamba Ndege inayotumia nguvu ya Jua inaweza kutumika kwenye dunia ya sasa.
Pamoja na hayo, safari yao bado ni ndefu ambapo siku mbili zilizopita waliripotiwa na CNN kwamba safari yao imekwama China kwa zaidi ya wiki mbili baada ya kushindwa kupaa kutokana na hali mbaya ya hewa, hali ikiwa mbaya inavunja masharti ya kuipaisha ndege hii.
Jamaa wamepanga kuzunguka na hii ndege kwenye nchi mbalimbali za dunia lakini bila kutumia hata tone moja la mafuta, yani wanataka itumike nguvu ya jua kama ndege ilivyoundiwa.
DIAMOND NA MPENZI WAKE ZARI WAGOMA KUTAJA JINSIA YA MTOTO WAO MTARAJIWA!!!
12:50 AM
No comments
STAA wa Muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, amefunguka kuwa hayupo tayari kuitaja jinsi ya mtoto wake mtarajiwa kwa kuogopa wafitini.
Akizungumza na mwanahabari wetu, Diamond anayetarajia kupata mtoto kwa mpenzi wake wa sasa, Zarinah Hassan ‘Zari’, alisema anamshukuru Mungu hadi sasa tayari anaijua jinsi ya mwanaye lakini hayupo tayari kuitaja.
“Tayari baby ameshapima na kujua jinsi ya mtoto lakini siwezi kuitaja kwa sasa maana wabaya nao ni wengi sana mjini hapa,” alisema Diamond.
CHEKI NA UDAUNLOD BRAND NEW VIDEO YA BEN POL - SOPHIA
12:46 AM
No comments
NI Bonge la udeo toka kwa mkali wa RNB Ben Pol ambaye ni kipenzi cha kinadada.
Location ni huko kwao Dodoma.
Enjoy ngoma….!
Location ni huko kwao Dodoma.
Enjoy ngoma….!
Monday, April 20, 2015
TAFITI ZINAONESHA ASILIMIA 50 YA WANAUME NI WAGUMBA, FAHAMU DALILI NA JINSI YA KUEPUKA JANGA HILI!
7:49 AM
No comments
WANAUME wengi hapa nchini na nchi nyingi za Afrika bado hawafahamu kwamba tatizo la ugumba si kwa wanawake pekee bali wanaume pia hukumbwa na tatizo hili tena kwa asilimia sawa kabisa na wanawake.Tafiti za kitabibu zinaonesha kuwa matatizo ya ugumba huwakuta wanaume kwa asilimia 50 kama ambavyo 50% inayobaki huwa ni kwa wanawake.
Kutofahamu huku kumekuwa mwiba mkali kwa wanawake pale inapotokea wanandoa wameishi zaidi ya mwaka mmoja bila mwanamke kufanikiwa kushika ujauzito wakati wanashiriki tendo la ndoa bila kinga yoyote.
Ugumba kwa wanaume maana yake mwanaume kupoteza uwezo wake wa kutungisha mimba ambao alikuwa nao awali.
Hii maana yake ni kwamba mwanaume anaweza kuwa na uwezo mzuri wa kushiriki tendo la ndoa lakini hawezi kusababisha ujauzito.
Hili ni tofauti na tatizo la mwanaume kushindwa kabisa kushiriki tendo la ndoa, au lile la wanaume kuwahi kufika kileleni na baada ya tendo hilo moja hupatwa na uchovu mkubwa na kushindwa kurudia awamu nyingine dakika chache kukumbwa na usingizi.
Matatizo yote haya hutibika kama mwanaume ataamua kwa dhati kuchukua jukumu la kutafuta huduma/tiba katika hospitali/kliniki sahihi.
Katika makala haya, nitafundisha dalili, vyanzo, na jinsi ya kujikinga kuingia katika dimbwi la ugumba kwa wanaume.
Dalili za ugumba kwa wanaume.
Mara nyingi wanaume wagumba huwa hawaoneshi dalili za moja kwa moja, jambo ambalo hufanya jamii kuwa na tabia ya kupeleka mzigo wa lawama kwa wanawake. Wanandoa wengi huanza kupatwa na wasiwasi wanapofikisha mwaka mmoja au zaidi bila mama kufanikiwa kushika ujauzito.
Katika kipindi hiki ndipo wanume nao huanza kuwa na mashaka japo wengi wao huwa hawaoneshi mashaka hayo waziwazi mbele ya wenza wao.
Hata hivyo, dalili zifuatazo huashiria tatizo la ugumba kwa wanaume:
•Kushindwa kutotungisha mimba kwa miezi 12 au zaidi
•Kuwa na matatizo ya kufika kileleni kwa mfano kuwahi sana na au kuchelewa sana au kushindwa kabisa kufika kileleni
•Kutomaliza tendo la ndoa na uume kusinyaa wakati wa tendo
•Maumivu ya korodani
•Uvimbe kwenye korodani
•Kupungua kwa korodani au kupotea/kuingia ndani kwa korodani
•Kupungua kwa vinyweleo, ndevu na hata nywele
•Kuwa na korodani ngumu kupita kiasi
•Kupoteza hamu ya kushiriki tendo la ndoa
•Tatizo la mwanaume kushindwa kabisa kuinuka.
Endelea kufuatilia hapa...
HARUSI YA MTOTO WA MIZENGO PINDA ILIVYOMTOA MACHOZI LULU KATIKA HARUSI YAKE *PICHAZ*
7:40 AM
No comments
Ikumbukwe kwamba Chrispine Mizengo Pinda na Adeline Ngugi wote wamehitimu pamoja katika chuo cha kimataifa cha Diplomasia kilichopo kurasini jijini Dar es Salaam amabapo walisoma Post Graduate in Management of Foreign Relations.
Bwana Harusi Chrispine Mizengo Pinda akiingia ukumbini wakati wa Sherehe ya ndoa yake na Bi.Adeline iliyofanyaka katika ukumbi wa JK Hall viwanja vya Saba saba Jijini Da r es Salaam Jana.
Marafiki wa karibu wa Chrispine na Adeline waliowakilisha wanafunzi wa chuo cha Diplomasia katika Hrusi hiyo wakifurahi Pamoja walipokuwa katika sherehe hiyo wakiongozwa na Khadija,Hassan ,Zitta,Lulu,Diana,Kennedy,Ngamanya,Mwanakatwe na Glady
Hassan Abbas kutoka ofisi ya Rais Ikulu ambaye ni mkuu wa mawasiliano wa BRN Tanzania akifurahia Jambo na Kennedy Ndosi wa Masma Blog katika Harusi Hiyo
Binti huyu mwenye gauni la bluu Lulu Rodgers (katikati) ndiye aliyedaiwa kumwaga chozi kwa furaha baada ya kuona wawili hao ambao ni marafiki zake wakifunga ndoa takatifu jana kwani anasema walikuwa wakitaniana sana kiasi kwamba anaamini ndoa yao itakuwa ya furaha na amani sana..
MUME WA SHAMSA FORD AMPOST 'EX' WA NAY WA MITEGO 'SIWEMA' *PICHAZ*
7:14 AM
No comments
Magazeti, Blogs na vituo vya radio vimeripoti mara kadha tetesi za mapenzi ya mastaa Nay wa Mitego na Shamsa Ford wa bongo movie baada ya pciah kadha za Shamsa akiwa nyumbani kwa Nay Wa Mitego kusamba.
Stori hii ilivuma zaidi baada ya picha ya busu la Nay Wa Mitego na Shamsa kuwekwa mtandaoni na Diamond huku Shamsa akisema ni filamu inakuja.
Hivi karibuni mume wa Shamsa ametumia kurasa yake ya Instagram kumpa sifa aliyekuwa mpenzi wa Nay Wa Mitego, Siwema.
FAHAMU KIINGILIO KATIKA WHITE PARTY YA ZARI *ENTRANCE FEES TO DIAMOND PLATINUMZ MAY 1ST, EVENT*
4:25 AM
No comments
WE both heard and saw the pictures about May 1st, the date which promise to bring big things to Dar es Salaam, from Tanzanian sensation Diamond Platinumz. So, the event will take place at Mlimani City and below are the entrance fees as communicated by Diamond and his team;
50,000/=
100,000/= VIP
1,000,000/= VIP Table plus 4 tickets & Drinks Coupon....
3,000,000/= VVIP Table plus 8 tickets & One Million Drinks Coupon... ( for the VIP & VVIP Table booking Call +255755700400 )......
IN SWAHILI-
50,000/=
100,000/= VIP
1,000,000/= Meza ya VIP sambamba na Tiketi Nne na Vinywaji vya Bure
3,000,000/=VVIP sambamba na Ticket 8 na Vinywaji vya Bure vya Milioni Moja...) kwa maelezo na Kuwai Meza piga +255755700400
Subscribe to:
Posts (Atom)
ZILIZOSOMWA ZAIDI
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) jana, Jumamosi, Me...
-
ZILE picha za mahaba za msanii wa Hip Hop Bongo, Nay Wa Mitego akiwa na msichana kitandani zimezua balaa kwa mama mtoto wake Siwema Eds...
-
Katika pitapita zangu huko instagram nkakutana na picha hii ya msanii wa kizazi kipya Shishi Baby au mamaa ya Mziwanda. Haaa...
-
Hanging With The Bro! Diamond Platnumz & Kanye West Take A Selfie In L.A. Tanzanian music sensation Chibu Dangote also known has Diam...