Tuesday, December 23, 2014

MWANANCHI AFUNGUKA - "MABROGGA NDIO MNAOWAPA VICHWA HAWA WAPUUZ* KWA KUPOST MAPICHA YAO KWENYE MITANDAO YENU"

KATIKA harakati za hapa na pale, nikafanikiwa kupita katika moja ya post iliyotupiwa na mdau huyu kuhusu video hii, tiririka nayo mdau wangu wa kushiba:
"SWALI: Hivi umeshawahi kujiuliza ni kwa nini watu hupendelea au hupiga picha au kuchukua video za namna hii na kuziweka katika mitandao ya kijamii kama facebook, Twitter, Instagram??
Kiukweli majibu tunayo sisi kama raia tunaozishabikia na kuziona hizi picha ni za kipekee na zenye uhai katika macho yetu…Mi naona ni ujinga tu… na kiukweli wanaofanya hivi ni watu wanaotaka umaarufu wa kijinga na hata kama wataupata basi hautakuwa wa kuheshimika. wangapi tumewaona ni mastaa na bado wanafanya upuuzi tu kwa kutumia video kama hizi…Na nyie mabrogga ndio mnaowapa vichwa hawa wapuuzi kwa kupost mapicha yao kwenye mitandao yenu #Acheni mara moja tuone kama watapata huo umaarufu wanaoutaka! Pumbafu kabisa hawa…Ndio kuna uhuru wa mtu kufanya atakalo lakini nahisi hawa wanazidi na hawafikirii kabisa kwa wanachokifanya.
Na hivi Serikali na vyombo husika viko wapi jamani mbona haya mnayafumbia macho????? Kamateni hawa, weka ndani kidogo tuone kama watapata mapozi mazuri na sehemu nzuri za kupiga picha wakiwa Segerea..Aaaaaagh"

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI