WASWAHILI wanasema ukiona umeanza mwaka kwa mambo mazuri ujue mwaka huo wote utakuwa mzuri kwako, Lady Gaga hakuingiza pesa nyingi kihivyo kwa mwaka 2014, muziki haukumlipa sana hivyo hii deal mpya huenda ikamuongezea kipato 2015.
Lady Gaga amepata deal la kutangaza bidhaa mbalimbali za kampuni ya Shiseido inayouza bidhaa za urembo pamoja na bidhaa zinazotumika saluni, amepiga picha kadhaa ambazo zitaanza kutangazwa kwenye magazine ya Kampuni hiyo mwaka 2015, Gaga hakusubiri mwaka uanze, ameanza kushare kama picha hamsini hivi kwenye ukurasa wake wa Instagram (@ladygaga).
Picha hizo zitatumika pia katika Magazeti mbalimbali mwaka 2015 kwa ajili ya kutangaza bidhaa za kampuni hiyo, hapa kuna baadhi ya picha hizo lakini ukitaka kuzitamama nyingine zipo kwenye ukurasa wake wa Instagram (@ladygaga).
0 comments:
Post a Comment