MAREKANI imesema inaendesha mapambano ya anga dhidi ya kikundi cha kiisilamu cha Alshabab Nchini Somalia ambalo limekuwa likifanya mashambulizi ya mara kwa mara.
Kwa mujibu wa Idara ya Ulinzi nchini Marekani lengo lao ni kumkamata kiongozi wa kundi hilo katika eneo la Seakow.
Mpaka sasa haijafahamika endapo kuna majeruhi ambao wameathirika na mapambano hayo.
Marekani ilivisaidia vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Africa AU kuwaondoa wanamgambo wa Alshabab katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu na katika miji mingine tangu mwaka 2011.
Mwezi September Kiongozi wa Alshabab Ahmed Abdi Godabe aliuawa kufuatia mashambulizi ya anga yaliyofanywa na marekani
Mashambuliz hayo yamekuja siku chache baada ya kiongozi wa juu wa kundi hilo Zakariya Ahmed Ismail Hersi kujisalimisha mikononi mwa polisi
0 comments:
Post a Comment