Tuesday, December 30, 2014

CHEKA NA HII: BARUA KWA MCHUNGAJI

th-115

MCHUNGAJI NIRUDISHIE HELA ZANGU MI SIKUBALI 

"Chonde chonde mi staki ugomvi wala nini nadai haki yangu tu. Unakumbuka Januari 2014 nilianza kuja kituoni kwako baada kusikia habari zako kuwa unafanya miujiza mikubwa. 

Nilipokuja kwako nikakueleza matatizo yangu ukanambia nihakikishe ninapanda mbegu kwa kutoa michango mbalimbali ya kituo kufikia mwisho wa mwaka ntakuwa na mke, gari na nyumba nzuri. 

Mkuu tarehe 31 ndio hiyo mi niko palepale sina mke wala mchumba, sina gari wala baiskeli na mama mwenye nyumba kanipa wiki mbili nisipolipa deni hata pakulala ntakuwa sina,  nimeshachangia karibu milioni, nirudishie kuna mahala pengine nataka kuwekeza. Muumini wako."

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI