Thursday, November 27, 2014

SOMA KWA MAKINI KUHUSU MWANAUME ANAYETEKA WASICHANA, KUFANYA NAO MAPENZI KISHA ANAWAUA, JIJINI DAR

POLISI kanda ya Dar es salaam wametoa tahadhari kwa wanawake kuacha kushiriki mapenzi na watu wasiowafahamu ili kuepuka kuuawa.
Taarifa ya Kamishna wa Kanda Suleiman Kova ilisema wasichana hususani wa jijini Dae es salaam wanatakiwa kuwa makini na wanaume wasiowajua kwa sababu wengi wameishia kuuawa kikatili huku miili yao ikitelekezwa hovyo.
“Kuna taarifa ya kuwepo wanaume wawili wanaowashawishi wanawake kufanya nao mapenzi na baada ya muda huwaua,natoa tahadhari kwa wanawake wote kuwa makini na watu hawa”alisema Kova.
Alisema siku za hivi karibuni kumekuwepo na matukio mengi ya mauaji ya aina hiyo ambapo kwa sasa wanawake wapatao sita tayari wameshapoteza maisha.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI