DVJ Penny.
MTANGAZAJI aliyewahi kujiachia kimahaba na Nasibu Abdul ‘Diamond’, Penniel Mungilwa ‘Penny’ amesema mwanamuziki huyo kwa sasa alie tu kwani ameshachumbiwa na hawezi kumpata tena.
Kauli ya mwanadada huyo ilikuja baada ya kuulizwa kama anaafikiana na kauli ya mama wa Wema Sepetu, Miriam Sepetu kwamba, kwa kuwa Wema kamuacha Diomond basi staa huyo wa Wimbo wa Mdogomdogo bora akampose yeye.
“Mmh! Hapa suala la Diamond kurudiana na mimi halipo kabisa maana simhitaji yeye wala mwanaume mwingine yeyote, mimi ninaye wangu tayari ambaye ameshanichumbia hivyo sitarajii kabisa kuwa na mwingine zaidi yake,” alisema Penny.
Penny ambaye alishawahi kuwa rafiki mkubwa wa Wema Sepetu.
Penny alipokuwa na Diamond katika mahusiano….!
0 comments:
Post a Comment